Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday 3 April 2020

Kikombe Cha Asubuhi; Ezekieli 33...




Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu katika yote....

Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana
Mungu wa walio hai,Mungu  mwenye huruma,Mungu wa upendo
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu

Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!




Kutokana na hayo, mimi Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu kwa ajili yenu, namwomba Mungu. Bila shaka mmekwisha sikia kwamba Mungu, kwa neema yake, alinikabidhi kazi hii niifanye kwa faida yenu.

Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako,
Tukijinyenyekeza,tukijiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunamomba utusamehe dhambi zetu
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
 ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea

Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Mimi nilijulishwa kwa njia ya ufunuo mpango wake uliofichika. (Nimeandika kwa ufupi juu ya jambo hili, nanyi mkiyasoma maneno yangu mtaweza kujua jinsi ninavyoielewa siri hiyo ya Kristo).
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomna ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe...


Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Yahwe ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii..
Baba wa Mbinguni  tunaomba ukatupe neema ya kufuata
njia zako,tukasimamie Neno lako,amri na sheria zako
siku zote za maisha yetu...
Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukatufanye chombo chema
ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....


Zamani watu hawakujulishwa siri hiyo; lakini sasa Mungu amewajulisha mitume na manabii wake watakatifu kwa njia ya Roho. Siri yenyewe ni hii: Kwa njia ya Injili watu wa mataifa mengine wanapata sehemu yao pamoja na Wayahudi katika zile baraka za Mungu; wao ni viungo vya mwili uleule, na wanashiriki ahadi ileile aliyofanya Mungu kwa njia ya Kristo Yesu.
Tazama watoto wako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
kila mmoja na mahitaji yake
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipo kwenda kinyume nawe
Yahweh tunaomba ukawape neema ya kuweza kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru...
Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele...
Amina...!!


Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake...

Nawapenda.

Ezekieli atakuwa mlinzi

1Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia: 2“Wewe mtu! Ongea na wananchi wenzako, uwaambie hivi: Kama nikizusha vita katika nchi fulani, na watu wa nchi hiyo wakamchagua mmoja wao awe mlinzi wao, 3huyo anapoona maadui wanakuja, atapiga tarumbeta na kuwaonya watu. 4Mtu akisikia sauti ya tarumbeta lakini akapuuza onyo hilo, maadui wakaja na kumuua, yeye mwenyewe atawajibika kwa kifo chake. 5Aliisikia sauti ya tarumbeta, akapuuza onyo; basi lawama ya kifo chake itakuwa juu yake mwenyewe. Lakini kama angejali hilo onyo, angeyaokoa maisha yake.
6“Lakini kama yule mlinzi akiona adui wanakuja asipige tarumbeta na watu wakawa hawakuonywa juu ya hatari inayokuja, maadui wakaja na kumuua mtu yeyote miongoni mwao; huyo mtu aliyekufa, atakuwa amekufa kwa kosa lake. Lakini mimi nitamdai mlinzi kifo cha mtu huyo.
7“Basi, ewe mtu, nimekuweka kuwa mlinzi wa Waisraeli. Utakaposikia neno kutoka kwangu utawapa onyo langu. 8Nikimwambia mtu mwovu: ‘Wewe mtu mwovu hakika utakufa’; lakini wewe husemi chochote ili kumwonya yule mtu mwovu aachane na mwenendo wake; mtu huyo hakika atakufa kwa kosa lake; walakini nitakudai wewe kifo chake. 9Lakini ukimwonya mwovu aachane na mwenendo wake, naye haachani na mwenendo wake mbaya, yeye atakufa kwa kosa lake; lakini wewe utakuwa umeyaokoa maisha yako.
Kuwajibika
10“Ewe mtu! Waambie Waisraeli jambo hili: Nyinyi mwasema, ‘Tumezidiwa na makosa na dhambi zetu. Tunadhoofika kwa sababu yake! Tutawezaje basi, kuishi?’ 11Basi, waambie: Kama niishivyo mimi Bwana Mwenyezi-Mungu naapa kwamba, mimi sikifurahii kifo cha mtu mwovu, bali napenda mtu mwovu aachane na mwenendo wake mbaya, apate kuishi. Tubuni, achaneni na mwenendo wenu mbaya, enyi Waisraeli! Kwa nini mwataka kufa?
12“Basi, ewe mtu, waambie wananchi wenzako hivi: Mtu mwadilifu akitenda uovu, uadilifu wake hautamwokoa. Na mtu mwovu akiacha kutenda dhambi hataadhibiwa. Mtu mwadilifu akianza kutenda dhambi uadilifu wake hautamsalimisha. 13Mimi namwahidi mwadilifu kwamba ataishi; lakini yeye akiamini kwamba uadilifu wake watosha, akaanza kutenda uovu, matendo yake yote mema ya hapo awali hayatakumbukwa; atakufa kwa uovu wake. 14Tena, nikimwambia mtu mwovu kuwa hakika atakufa naye akaiacha dhambi yake, akaanza kutenda yaliyo ya haki na sawa, hatakufa; 15kama akirudisha rehani na kurudisha alichoiba, akafuata kanuni ziletazo uhai bila kutenda uovu, mtu huyo hakika ataishi; hatakufa. 16Dhambi zake zote alizotenda hapo awali hazitakumbukwa; yeye ametenda yaliyo ya haki na mema; kwa hiyo hakika ataishi.
17“Lakini wananchi wenzako wasema ati: ‘Anachofanya Mwenyezi-Mungu si sawa!’ Kumbe kwa kweli wao ndio hawafanyi kilicho sawa. 18Mtu mwadilifu akiacha uadilifu wake, akaanza kutenda uovu, atakufa kwa sababu ya uovu wake. 19Na mtu mwovu akiacha uovu wake, akaanza kutenda mambo ya haki na mema ataishi kwa sababu ya matendo yake mema. 20Lakini, nyinyi mwasema ati: ‘Anachofanya Mwenyezi-Mungu si sawa!’ Enyi Waisraeli, mimi nitamhukumu kila mmoja wenu kadiri ya matendo yake.”
Kutekwa kwa Yerusalemu
21Siku ya tano ya mwezi wa kumi, mwaka wa kumi na mbili wa uhamisho wetu, mtu mmoja aliyetoroka kutoka Yerusalemu alinijia, akasema: “Mji wa Yerusalemu umetekwa!” 22Wakati alipofika huyo mtu ilikuwa asubuhi kumbe jana yake jioni mimi nilisikia uzito wa nguvu yake Mwenyezi-Mungu. Basi, huyo mkimbizi alipowasili kwangu kesho yake asubuhi, nikaacha kuwa bubu,33:22 nikaacha kuwa bubu: Taz 3:26; 24:27. nikaanza kuongea tena.
Dhambi za watu
23Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia: 24“Wewe mtu! Wakazi waliobaki katika miji iliyoharibiwa nchini Israeli wanasema, ‘Abrahamu alikuwa peke yake, hata hivyo, alipata kuimiliki nchi hii. Lakini sisi ni wengi; ni dhahiri tumepewa nchi hii iwe yetu!’ 25Basi, waambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nyinyi mnakula nyama yenye damu, mnaziabudu sanamu za miungu yenu na kuua! Je, mnadhani mtapewa nchi hii iwe yenu? 26Mnategemea silaha zenu, mnafanya mambo ya kuchukiza na kila mwanamume miongoni mwenu anatembea na mke wa jirani yake! Je, mnadhani mtapewa nchi hii iwe yenu? 27Waambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Kama niishivyo mimi naapa kwamba hao wanaokaa katika miji hiyo iliyo magofu, wataangamia kwa upanga; aliye uwanjani nitamtoa aliwe na wanyama wakali; na wale walio ndani ya ngome na mapangoni watakufa kwa maradhi mabaya. 28Nitaifanya nchi kuwa jangwa na tupu. Mashujaa wake wenye kiburi nitawaua. Milima ya Israeli itakuwa jangwa na hakuna mtu atakayepita huko. 29Naam, nitakapoifanya hiyo nchi kuwa jangwa na tupu kwa sababu ya mambo yote ya kuchukiza waliyotenda, ndipo watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.”
Matokeo ya mahubiri ya nabii
30Mwenyezi-Mungu aliniambia, “Wewe mtu! Wananchi wenzako wanazungumza juu yako, wameketi kutani na milangoni mwa nyumba zao na kuambiana: ‘Haya! Twende tukasikie neno alilosema Mwenyezi-Mungu!’ 31Basi, hukujia makundi kwa makundi na kuketi mbele yako kama watu wangu, wasikie unachosema, lakini hawafanyi unachowaambia wafanye. Wanasema kwamba wana upendo, lakini hayo ni maneno matupu; wanachotafuta kwa moyo ni faida yao tu. 32Kwao, wewe umekuwa tu kama mwimbaji wa kutumbuiza mwenye sauti nzuri ikiandamana na muziki safi! Wanayasikia yale unayosema, lakini hawatekelezi hata mojawapo. 33Lakini hayo unayosema yatakapotukia – nayo kweli yatatukia – basi, ndipo watakapotambua kuwa nabii amekuwapo miongoni mwao.”


Ezekieli33;1-33

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)


"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: