Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday 5 February 2020

Kikombe Cha Asubuhi; Yeremia 49....


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante  Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Neema yako yatutosha  Mungu wetu..!

Kisha Mafarisayo na waalimu wa sheria wakafika kutoka Yerusalemu, wakamwendea Yesu, wakamwuliza, “Kwa nini wanafunzi wako hawajali mapokeo tuliyopokea kwa wazee wetu? Hawanawi mikono ipasavyo kabla ya kula!”
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,
tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako

Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa  Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Yesu akawajibu, “Kwa nini nanyi hamjali sheria ya Mungu ila mnapendelea mapokeo yenu wenyewe? Mungu amesema: ‘Waheshimu baba yako na mama yako,’ na ‘Anayemtukana baba yake au mama yake, lazima auawe.’
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe



Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu  wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo 

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

Lakini nyinyi mwafundisha ati mtu akiwa na kitu ambacho angeweza kumsaidia nacho baba yake au mama yake, lakini akasema: ‘Kitu hiki nimemtolea Mungu,’ basi, hapaswi tena kumheshimu baba yake! Ndivyo mnavyodharau neno la Mungu kwa kufuata mafundisho yenu wenyewe. Enyi wanafiki! Isaya alitabiri sawa kabisa juu yenu:
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba
 ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....

Nawapenda.


Waamoni

1Kuhusu Waamoni.
Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Je, Israeli hana watoto?
Je, hana warithi?
Mbona basi mungu Milkomu amemiliki Gadi
na watu wake kufanya makao yao mijini mwake?
2Basi, wakati unakuja kweli, siku zaja,
nasema mimi Mwenyezi-Mungu,
ambapo nitavumisha sauti ya vita
dhidi ya Raba mji wa Waamoni.
Raba utakuwa rundo la uharibifu,
vijiji vyake vitateketezwa moto;
ndipo Israeli atakapowamiliki wale waliomiliki.
Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
3“Ombolezeni, enyi watu wa Heshboni,
maana mji wa Ai umeharibiwa!
Lieni enyi binti za Raba!
Jifungeni mavazi ya gunia viunoni
ombolezeni na kukimbia huko na huko uani!
Maana mungu Milkomu atapelekwa uhamishoni,
pamoja na makuhani wake na watumishi wake.
4Mbona mnajivunia mabonde yenu, enyi msioamini,
watu mliotegemea mali zenu, mkisema:
‘Nani atathubutu kupigana nasi?’
5Basi, mimi nitawaleteeni vitisho
kutoka kwa jirani zenu wote,
nanyi mtafukuzwa nje kila mtu kivyake,
bila mtu wa kuwakusanya wakimbizi.
Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.
6Lakini baadaye nitawarudishia Waamoni fanaka yao.
Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Edomu
7Kuhusu Edomu.
Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi:
“Je, hakuna tena hekima mjini Temani?
Je, wenye busara wao hawana shauri tena?
Hekima imetoweka kabisa?
8Kimbieni enyi wakazi wa Dedani;
geukeni mkaishi mafichoni!
Maana nitawaleteeni maangamizi
enyi wazawa wa Esau;
wakati wa kuwaadhibu umefika.
9Wachuma zabibu watakapokuja kwenu
hawatabakiza hata zabibu moja.
Usiku ule wezi watakapofika,
wataharibu kila kitu mpaka watosheke.
10Lakini nimemnyanganya Esau kila kitu,
naam, nimeyafunua maficho yake,
wala hawezi kujificha tena.
Watoto, ndugu na jirani zake wameangamizwa;
hakuna hata mmoja aliyebaki.
11Niachieni watoto wenu yatima nami nitawatunza;
waacheni wajane wenu wanitegemee.”
12Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Ikiwa wale ambao hawakustahili kunywa kikombe cha adhabu ni lazima wanywe, je, wewe utaachwa bila kuadhibiwa? La! Hutakosa kuadhibiwa; ni lazima unywe hicho kikombe! 13Maana nimeapa kwa nafsi yangu kwamba mji wa Bosra utakuwa kioja na kichekesho, utakuwa uharibifu na laana; vijiji vyote vitakuwa magofu daima. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
14Nimepata habari kutoka kwa Mwenyezi-Mungu,
mjumbe ametumwa ayatangazie mataifa:
“Jikusanyeni pamoja dhidi ya Edomu;
inukeni mwende kuushambulia!
15Mimi Mwenyezi-Mungu nitakufanya wee Edomu
kuwa mdogo kuliko mataifa yote.
Ulimwengu wote utakudharau.
16Vitisho unavyotoa na kiburi chako vimekudanganya,
ewe ukaaye katika mapango ya miamba,
unayeishi juu ya kilele cha mlima!
Ingawa unaweka makao yako juu kama ya tai,
mimi nitakuporomosha kutoka huko uliko.
Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
17“Edomu itakuwa kitisho na kila mtu atakayepita karibu yake atashangaa, na kuizomea kwa sababu ya maafa yatakayoipata. 18Kama vile Sodoma na Gomora na miji jirani yake ilivyoangamizwa, mimi Mwenyezi-Mungu nasema, hakutakuwa na mtu yeyote atakayeishi Edomu wala kufanya mashauri humo. 19Kama vile simba anavyochomoza kutoka msitu wa mto Yordani na kuingia kwenye malisho mazuri, ndivyo nitakavyowafukuza ghafla Waedomu kutoka nchi yao. Nami nitamweka huko kiongozi yeyote nitakayemchagua. Maana, ni nani anayeweza kulinganishwa nami? Nani awezaye kunishtaki? Ni mchungaji gani awezaye kunipinga? 20Kwa hiyo, sikilizeni mpango ambao mimi Mwenyezi-Mungu nimepanga dhidi ya Edomu pamoja na mambo niliyokusudia kuwafanyia wakazi wa Temani: Hakika, watoto wao wadogo wataburutwa na kuchukuliwa; kweli kutakuwa na mshangao mkubwa katika makao yao! 21Kwa kishindo cha kuanguka kwao, dunia itatetemeka; sauti ya kilio chao itasikika mpaka bahari ya Shamu. 22Tazama, adui atapanda juu na kuruka kama tai na kutandaza mabawa yake juu ya Bosra. Siku hiyo moyo wa mashujaa wa Edomu utakumbwa na hofu kama ya mwanamke anayejifungua.”
Damasko
23Kuhusu Damasko:
“Miji ya Hamathi na Arpadi, imejaa wasiwasi
kwa kufikiwa na habari mbaya;
mioyo ya watu wake inayeyuka kwa hofu,
imefadhaika kama bahari isiyoweza kutulia.
24Watu wa Damasko wamekufa moyo;
wamegeuka wapate kukimbia;
hofu kubwa imewakumba,
uchungu na huzuni vimewapata,
kama mwanamke anayejifungua
25Ajabu kuachwa kwa mji maarufu,
mji uliokuwa umejaa furaha!49:25 Baadhi ya tafsiri za zamani: Umejaa furaha: Kiebrania furaha yangu.
26Basi vijana wake wataanguka viwanjani mwake,
askari wake wote wataangamizwa siku hiyo.
Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.
27Nitawasha moto katika kuta za Damasko,
nao utateketeza ngome za mfalme Ben-hadadi.”
Makabila ya Kedari na Hazori
28Kuhusu Kedari na falme za Hazori ambazo Nebukadneza mfalme wa Babuloni, alizishambulia na kuzishinda, Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Inuka uende kulishambulia kabila la Kedari!
Waangamize watu wa mashariki!
29Hema zao na kondoo wao vitachukuliwa,
kadhalika mapazia yao na mali yao yote;
watanyanganywa ngamia wao,
na kilio kitasikika: ‘Kitisho kila upande!’
30Kimbieni, nendeni mbali, kaeni mashimoni.
Enyi wakazi wa Haziri,
kimbieni mtangetange na kukaa mafichoni!
Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Maana Nebukadneza mfalme wa Babuloni,
amefanya mpango dhidi yenu,
amepania kuja kuwashambulia.
31Inuka uende kulishambulia taifa linalostarehe,
taifa linaloishi kwa usalama.
Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Taifa hilo halina malango wala pao za chuma;
ni taifa ambalo liko peke yake.
32“Ngamia wao watatekwa
mifugo yao itachukuliwa mateka.
Nitawatawanya kila upande,
watu wale wanaonyoa denge.
Nitawaletea maafa kutoka kila upande.
Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
33Mji wa Hazori utakuwa makao ya mbweha,
utakuwa jangwa daima;
hakuna mtu atakayekaa humo,
wala atakayeishi humo.”
Elamu
34Neno la Mwenyezi-Mungu lililomjia nabii Yeremia kuhusu Elamu, mwanzoni mwa utawala wa Sedekia, mfalme wa Yuda. 35Mwenyezi-Mungu wa majeshi, asema hivi: “Nitavunja upinde wa watu wa Elamu ulio msingi wa nguvu zao. 36Nitaleta upepo kutoka pande zote za mbingu; nitawatawanya kila mahali, wala hapatakuwa na taifa lolote ambalo halitakuwa na wakimbizi wa Elamu. 37Nitawafadhaisha watu wa Elamu mbele ya maadui zao na mbele ya wale wanaotaka kuyaangamiza maisha yao. Nitawaletea maafa na hasira yangu kali. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Nitawaletea upanga kuwafuata mpaka niwaangamize kabisa. 38Nitaweka kiti changu cha enzi huko Elamu na kumwangamiza mfalme wao pamoja na wakuu wao. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. 39Lakini katika siku za mwisho, nitaurudishia mji wa Elamu fanaka yake. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”


Yeremia49;1-39

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: