Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday 30 November 2018

Kikombe Cha Asubuhi ;Zaburi 7...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante

 kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Jehovah  Jireh..!Jehovah Nissi..!Jehovah Raah..!
Jehovah Rapha..!Jehovah Shammah..!Jehovah Shamlom..!
Emanuel-Mungu pamohja nasi..!!
Neema yako yatutosha Baba wa Mbinguni..!
“Nimekuja kuwasha moto duniani; laiti ungekuwa umewaka tayari! Ninao ubatizo ambao inanipasa niupokee; jinsi gani ninavyohangaika mpaka ukamilike! Mnadhani nimekuja kuleta amani duniani? Hata kidogo; si amani bali utengano. Na tangu sasa, jamaa ya watu watano itagawanyika; watatu dhidi ya wawili, na wawili dhidi ya watatu. Baba atakuwa dhidi ya mwanawe, mwana dhidi ya baba yake; mama dhidi ya bintiye, binti dhidi ya mama yake; mamamkwe dhidi ya mke wa mwanawe na huyo dhidi ya mamamkwe wake.”

Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha
na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizo zifanya
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Usitutie majaribu Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona...

Yesu akayaambia tena makundi ya watu, “Mnapoona mawingu yakitokea upande wa magharibi, mara mwasema: ‘Mvua itanyesha,’ na kweli hunyesha. Mnapoona upepo wa kusi unavuma, mwasema ‘Kutakuwa na joto,’ na ndivyo inavyokuwa. Enyi wanafiki! Mnajua kutabiri hali ya hewa kwa kuangalia hali ya nchi na anga; kwa nini, basi, hamwezi kujua maana ya nyakati hizi?

Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe



Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu wetu tunaomba ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Baba wa Mbinguni ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo Mungu wetu

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

“Na kwa nini hamwezi kujiamulia wenyewe jambo jema la kufanya? Maana kama mshtaki wako anakupeleka mahakamani, ingekuwa afadhali kwako kupatana naye mkiwa bado njiani, ili asije akakupeleka mbele ya hakimu, naye hakimu akakutoa kwa polisi, nao wakakutia ndani. Hakika hutatoka huko, nakuambia, mpaka utakapomaliza kulipa senti ya mwisho.”

Tazama wenye shida/tabu,watoto wako wanaokutafuta kwa bidii na imani
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
Yahweh tunaomba  ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Mungu wetu  unajua haja za mioyo ya kila mmoja
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Jehovah ukaonekane katika maisha yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....
Nawapenda.

Sala ya mtu anayedhulumiwa
(Ombolezo la Daudi kwa sababu ya Kushi wa kabila la Benyamini)
1Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, nakimbilia usalama kwako;
uniokoe na wote wanaonidhulumu, unisalimishe.
2La sivyo, watakuja kunirarua kama simba,
wakanivutia mbali, pasiwe na wa kuniokoa.
3Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu!
Kama nimetenda moja ya mambo haya:
Kama nimechafua mikono yangu kwa ubaya,
4kama nimemlipa rafiki yangu mabaya badala ya mema,
au nimemshambulia adui yangu bila sababu,
5basi, adui na anifuatie na kunikamata;
ayakanyage maisha yangu;
na kuniulia mbali.
6Inuka ee Mwenyezi-Mungu, kwa hasira yako,
uikabili ghadhabu ya maadui zangu.
Inuka, ee Mungu wangu,7:6 ee Mungu wangu: Au Kwa ajili yangu.
wewe umeamuru haki ifanyike.
7Uyakusanye mataifa kandokando yako,
nawe uyatawale kutoka juu.
8Wewe, ee Mwenyezi-Mungu, wayahukumu mataifa;
unihukumu kadiri ya uadilifu wangu,
kulingana na huo unyofu wangu.
9 Taz Ufu 2:23 Uukomeshe uovu wa watu wabaya,
uwaimarishe watu walio wema,
ee Mungu uliye mwadilifu,
uzijuaye siri za mioyo na fikira za watu.
10Mungu ndiye ngao yangu;
yeye huwaokoa wanyofu wa moyo.
11Mungu ni hakimu wa haki;
kila siku hulaumu maovu.
12Watu wasipoongoka,
Mungu atanoa upanga wake;
atavuta upinde wake na kulenga shabaha.
13Atatayarisha silaha zake za hatari,
na kuipasha moto mishale yake.
14Tazama! Mtu mbaya hutunga uovu,
hujaa uharibifu
na kuzaa udanganyifu.
15Huchimba shimo, akalifukua,
kisha hutumbukia humo yeye mwenyewe.
16Uharibifu wake utamrudia yeye mwenyewe;
ukatili wake utamwangukia yeye binafsi.
17Nitamshukuru Mwenyezi-Mungu kwani ni mwema;
nitaimba sifa za jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu Mkuu.


Zaburi7;1-17

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: