Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday 8 November 2018

Kikombe Cha Asubuhi ;Yobu 33...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah Mungu wetu yu mwema sana..
Tumshukuru Mungu wetu katika yote....

Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Baba wa Upendo,Baba wa faraja,Baba wa huruma,Baba wa Baraka
Mungu mwenye nguvu,Mungu mwenye kuponya
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo,Muweza wa yote
Wewe ni mwanzo na wewe ni mwisho,Alfa na Omega...!!


Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii




Sasa, Wafilisti walikusanya majeshi yao huko Soko, mji ulioko katika Yuda, tayari kwa vita. Walipiga kambi katika sehemu moja iitwayo Efes-damimu kati ya Soko na Azeka. Shauli pamoja na Waisraeli walikusanyika, na kupiga kambi katika bonde la Ela. Wakajipanga tayari kupigana na Wafilisti. Wafilisti walisimama mlimani upande mmoja na Waisraeli walisimama mlimani upande mwingine, katikati yao kulikuwa na bonde.

Tazama Jana imepita ee Mungu wetu Leo ni siku mpya na kesho ni siku nyingineJehovah...
Yahweh tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha
na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizo zifanya
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Usitutie majaribu Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti

yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona

Kutoka kwenye kambi ya Wafilisti, alijitokeza shujaa mmoja aitwaye Goliathi, mwenyeji wa mji wa Gathi. Urefu wake ulikaribia mita tatu. Kichwani alivaa kofia ya shaba, na deraya ya shaba kifuani yenye uzito wa kilo 57. Miguu yake pia ilikuwa na kinga ya shaba na mabegani pake alibeba mkuki wa shaba. Mpini wa mkuki wake ulikuwa kama mti wa mfumanguo, na chembe cha mkuki huo, kilikuwa na uzito wa kilo saba. Ngao yake ilibebwa na mtu mwingine aliyemtangulia. Goliathi alisimama na kuwapigia kelele wanajeshi wa Israeli, akisema, “Mnafanya nini hapo? Je, mmekuja kupigana vita? Mimi ni Mfilisti, nyinyi ni watumwa wa Shauli. Chagueni mtu mmoja wenu aje kupigana nami. Akinishinda na kuniua, sisi tutakuwa watumwa wenu. Lakini nikimshinda na kumuua basi, nyinyi mtakuwa watumwa wetu na kututumikia.”

Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni
tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe....



Baba wa Mbinguni tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii

 Mungu wetu ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu

Baba wa Mbinguni tukanene yaliyo yako
Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Tukawe barua njema  ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

Kisha Mfilisti huyo aliendelea kusema kwa majivuno, “Nawataka wanajeshi wa Israeli siku hii kumtoa mtu mmoja aje kupigana nami.” Shauli pamoja na wanajeshi wote wa Israeli walipoyasikia maneno hayo ya Mfilisti huyo, walifadhaika na kuogopa sana.

Mungu Baba tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabuwote wanaopotia magumu/majaribu mbalimbali
watoto wako wanaokuomba kwa bidii na imani
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
 kila mmoja na mahitaji yake 
Yahweh tunaomba ukaonekane katika maisha yao
Jehovah tunaomba ukawaokoe,ukawavushe salama na  kuwalinda
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe
Baba wa Mbinguni ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako
wakasimaie Neno lako nalo likaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kuomba kwetu
Baba wa Mbinguni ukapokee sala/maombi yetu
Mungu wetu ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina...!!

Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami
Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea 
kama inavyompendeza yeye....
Nawapenda.







1“Sasa, Yobu, sikiliza hoja yangu;
sikiliza maneno yangu yote.
2Tazama, nafumbua kinywa changu,
naam, ulimi wangu utasema.
3Nitasema kadiri ya unyofu wa moyo wangu;
ninayoyajua nitayasema kwa uaminifu.
4Roho ya Mungu iliniumba,
nayo pumzi ya Mungu Mwenye Nguvu yanipa uhai.
5Nijibu, kama unaweza.
Panga hoja zako vizuri mbele yangu,
ushike msimamo wako.
6Wewe na mimi ni sawa mbele ya Mungu;
mimi pia niliumbwa kwa sehemu ya udongo.
7Kwa hiyo huna sababu ya kuniogopa;
maneno yangu mazito hayatakulemea.
8Kweli umesema, nami nikasikia;
nimeyasikia yote uliyosema.
9Wewe umesema, u safi na wala huna kosa,
u safi kabisa na huna hatia;
10umesema kwamba Mungu anakutafutia kisa,
na kukuona kama adui yake.
11 Taz Yobu 13:27 Anakufunga miguu minyororo,
na kuchunguza hatua zako zote.
12“Lakini Yobu, nakuambia hapo umekosea.
Mungu ni mkuu kuliko binadamu.
13Kwa nini unashindana naye,
ukisema hatajibu swali lako moja?
14Mungu anaposema hutumia njia moja,
au njia nyingine lakini mtu hatambui.
15 Taz Yobu 4:13 Mungu huongea na watu katika ndoto na maono,
wakati usingizi mzito unapowavamia,
16wanaposinzia vitandani mwao.
Hapo huwafungulia watu masikio yao;
huwatia hofu kwa maonyo yake,
17wapate kuachana na matendo yao mabaya,
na kuvunjilia mbali kiburi chao.
18Hivyo humkinga mtu asiangamie shimoni,
maisha yake yasiangamie kwa upanga.
19“Mungu humrudi mtu kwa maumivu yamwekayo kitandani,
maumivu hushika viungo vyake bila kukoma;
20naye hupoteza hamu yote ya chakula,
hata chakula kizuri humtia kinyaa.
21Mwili wake hukonda hata asitambuliwe,
na mifupa yake iliyofichika ikatokeza nje.
22Yuko karibu sana kuingia kaburini,
na maisha yake karibu na wale waletao kifo.
23Lakini malaika akiwapo karibu naye,
mmoja kati ya maelfu ya watetezi wa Mungu,
ili kumwonesha lililo jema la kufanya,
24akamwonea huruma na kumwambia Mungu;
‘Mwokoe asiingie Shimoni,
ninayo fidia kwa ajili yake.’
25Hapo mwili wake utaweza kuwa tena kama kijana,
ataweza kurudia tena nguvu zake za ujana.
26Kisha atamwomba Mungu na kukubaliwa,
atakuja mbele yake kwa furaha,
na Mungu atamrudishia fahari yake.
27Atashangilia mbele ya watu na kusema:
‘Nilitenda dhambi na kupotosha haki,
nami sikuadhibiwa kutokana na hayo.
28Mungu aliniokoa nisiangamie Shimoni;
nimebaki hai na ninaona mwanga.’
29“Tazama Mungu humfanyia binadamu haya yote,
tena mara mbili, mara tatu.
30Humwokoa binadamu asiangamie Shimoni,
aweze kuona mwanga wa maisha.
31Sikia Yobu, nisikilize kwa makini;
kaa kimya, nami nitasema.
32Kama una la kusema, nijibu;
sema, maana nataka kukuona huna hatia.
33La sivyo, nyamaza unisikilize,
kaa kimya nami nikufunze hekima.”



Yobu33;1-33

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: