Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday 5 November 2018

Kikombe Cha Asubuhi ;Yobu 30...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah ni siku/wiki/mwezi  mwingine tena Mungu wetu ametuchagua
na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Si kwamba sisi tumetenda mema sana wala si kwa nguvu zetu
si kwa utashi wetu wala si kwa akili zetu si kwamba sisi
ni wazuri mno si kwa uwezo wetu sisi kuwa hivi tulivyo leo hii
Ni kwa rehema/neema zake ni kwa mapenzi yake Mungu wetu....

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu
Sifa na Utukufu tunakurudshia Mungu wetu....!!



“Mimi siwezi kufanya kitu kwa uwezo wangu mwenyewe. Mimi ninahukumu kama ninavyosikia kutoka kwa Baba, nayo hukumu yangu ni ya haki. Nia yangu si kufanya nipendavyo mwenyewe, bali apendavyo yule aliyenituma. Nikijishuhudia mimi mwenyewe, ushahidi wangu hauwezi kukubaliwa kuwa wa kweli. Lakini yuko mwingine ambaye hutoa ushahidi juu yangu, nami najua kwamba yote anayosema juu yangu ni ya kweli. Nyinyi mlituma ujumbe kwa Yohane naye aliushuhudia ukweli. Si kwamba mimi nautegemea ushahidi wa wanadamu, lakini nasema mambo haya ili mpate kuokolewa.


Tazama jana imepita ee Mungu wetu leo ni siku mpya na kesho ni siku nyingine Jehovah tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
 Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Jehovah usitutie majaribu Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote
Yahweh tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona
Kwakupigwa kwake sisi tumepata kupona...

Yohane alikuwa kama taa iliyokuwa ikiwaka na kuangaza, nanyi mlikuwa tayari kufurahia mwanga huo kwa kitambo. Lakini mimi nina ushahidi juu yangu ambao ni mkuu zaidi kuliko ule wa Yohane. Kwa maana kazi ninazofanya, kazi alizonipa Baba nizifanye, ndizo zinazonishuhudia kwamba Baba ndiye aliyenituma. Naye Baba aliyenituma hunishuhudia. Nyinyi hamjapata kamwe kusikia sauti yake, wala kuuona uso wake, na ujumbe wake haukai ndani yenu maana hamkumwamini yule aliyemtuma. Nyinyi huyachunguza Maandiko Matakatifu mkidhani kwamba ndani yake mtapata uhai wa milele; na kumbe maandiko hayohayo yananishuhudia! Hata hivyo, nyinyi hamtaki kuja kwangu ili mpate uhai.
Yahweh tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe

Baba wa Mbinguni tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu
Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu
Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...


“Shabaha yangu si kupata sifa kutoka kwa watu. Lakini nawajua nyinyi, najua kwamba upendo kwa Mungu haumo mioyoni mwenu. Mimi nimekuja kwa mamlaka ya Baba yangu, lakini hamnipokei; bali mtu mwingine akija kwa mamlaka yake mwenyewe, mtampokea. Mwawezaje kuamini, hali nyinyi mnapenda kupokea sifa kutoka kwenu nyinyi wenyewe, wala hamtafuti sifa kutoka kwake yeye aliye peke yake Mungu? Msifikiri kwamba mimi nitawashtaki kwa Baba. Mose ambaye nyinyi mmemtumainia ndiye atakayewashtaki. Kama kweli mngemwamini Mose, mngeniamini na mimi pia, maana Mose aliandika juu yangu. Lakini hamyaamini yale aliyoandika; mtawezaje basi, kuamini maneno yangu?”

Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu,wote wanaopotia magumu/majaribu mbalimbali
watoto wako wanaokuomba kwa bidii na imani
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
 kila mmoja na mahitaji yake 
Yahweh tunaomba ukaonekane katika maisha yao
Jehovah tunaomba ukawaokoe,ukawavushe salama na  kuwalinda
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe
Baba wa Mbinguni ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako
wakasimaie Neno lako nalo likaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kuomba kwetu
Baba wa Mbinguni ukapokee sala/maombi yetu
Mungu wetu ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina...!!

Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami
Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea 
kama inavyompendeza yeye....
Nawapenda.



1“Lakini sasa watu wananidhihaki,
tena watu walio wadogo kuliko mimi;
watu ambao baba zao niliwaona hawafai
hata kuwaangalia mbwa wangu wakilinda kondoo.
2Ningepata faida gani mikononi mwao,
watu ambao nguvu zao zilikuwa zimewaishia?
3Katika ufukara na njaa kali
walitafutatafuta cha kutafuna nyikani30:3 walitafutatafuta … nyikani: Tafsiri nyingine: Waliguguna huko nyikani.
sehemu tupu zisizokuwa na chakula.
4Walichuma mimea jangwani na majani msituni wakala,
walikula hata mizizi ya mti wa mfagio.
5Walifukuzwa mbali na watu,
watu waliwapigia kelele kama wezi.
6Iliwapasa kutafuta usalama mapangoni,
kwenye mashimo ardhini na miambani.
7Huko vichakani walilia kama wanyama,
walikusanyika pamoja chini ya upupu.
8Walikuwa wapumbavu wakuu na mabaradhuli
ambao walilazimika kufukuzwa nchini kwa kiboko.
9“Na sasa wamenitungia wimbo wa kunizomea,
nimekuwa kitu cha dhihaka kwao.
10Wananichukia na kuniepa;
wakiniona tu wanatema mate.
11Kwa kuwa Mungu amenidhoofisha na kuniaibisha,
wamekuwa huru kunitendea wapendavyo.
12Genge la watu lainuka kunishtaki30:12 kunishtaki: Au upande wangu wa kulia.
likitafuta kuniangusha kwa kunitegea.
Linanishambulia ili niangamie.
13Watu hao hukata njia yangu
huchochea balaa yangu,
na hapana mtu wa kuwazuia.30:13 kuwazuia: Kiebrania: Kuwasaidia.
14Wanakuja kama kwenye ufa mkubwa,
na baada ya shambulio wanasonga mbele.
15Hofu kuu imenishika;
hadhi yangu imetoweka kama kwa upepo,
na ufanisi wangu umepita kama wingu.
16“Sasa sina nguvu yoyote nafsini mwangu;
siku za mateso zimenikumba.
17Usiku mifupa yangu yote huuma,
maumivu yanayonitafuna hayapoi.
18Mungu amenikaba kwa mavazi yangu,
amenibana kama ukosi wa shati langu.30:18 aya hii ni ngumu sana kutafsiri.
19Amenibwaga matopeni;
nimekuwa kama majivu na mavumbi.
20Nakulilia, lakini hunijibu,
nasimama kuomba lakini hunisikilizi.
21Umegeuka kuwa mkatili kwangu,
wanitesa kwa mkono wako wenye nguvu.
22Wanitupa katika upepo na kunipeperusha;
wanisukasuka huku na huko katika dhoruba kali.
23Naam! Najua utanipeleka tu kifoni,
mahali watakapokutana wote waishio.
24“Je, mtu akikumbwa na maangamizi hainui mkono?
Je, mtu akiwa taabuni haombi msaada30:24 aya hii katika Kiebrania si dhahiri.
25Je, sikuwalilia wale waliokuwa na taabu?
Je, sikuona uchungu kwa ajili ya maskini?
26Lakini nilipotazamia mema, mabaya yalinipata,
nilipongojea mwanga, giza lilikuja.
27Moyo wangu wahangaika wala hautulii kamwe;
siku za mateso zimekumbana nami.
28Napitapita nikiomboleza, kwangu hamna jua.
Nasimama hadharani kuomba msaada.
29Kwa kilio nimekuwa ndugu yake mbwamwitu,
mimi na mbuni hamna tofauti.
30Ngozi yangu imebambuka
mifupa yangu inaungua kwa homa.
31Kinubi changu kimekuwa cha kufanya matanga
filimbi yangu kwa ajili ya kuomboleza.




Yobu30;1-31

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: