Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 15 July 2018

Natumaini Jumapili ni Nejma;Burudani-MKONO WA BWANA by Zabron singers kahama ,WALTER CHILAMBO - ONLY YOU..
Hamjambo Juma pili yako ilikuwaje/inaendeleaje?
Hapa kwetu ni salama kabisa Mungu yu mwema..
hali ya hewa ni joto kijua kinawaka ni shangwe tuu....!!
Niwatakie kila lililojema na mapumziko mema tayari kwa kujiandaa na 
pilika za juma tatu.....

Neno La Leo Methali 30;1-14Mawaidha ya Aguri

1Maneno ya Aguri, mwana wa Yake. Mawaidha ambayo mtu huyu alimwambia Ithieli, naam, Ithieli na Ukali.30:1 Ithieli, Ukali: Majina hayo yaweza kumaanisha Nimechoka ee Mungu; nimechoka na sina nguvu.
2Mimi ni mpumbavu mno, wala si mtu;
nayo akili ya binadamu sina.
3Sijajifunza hekima,
wala sijui kitu juu ya Mungu Mtakatifu.
4Ni nani aliyepanda juu mbinguni akashuka chini?
Ni nani aliyekamata upepo mkononi?
Ni nani aliyefunga maji katika kitambaa?
Ni nani aliyeiweka mipaka yote ya dunia?
Jina lake ni nani? Na ni nani jina la mwanawe?
Niambie kama wajua!
5Maneno yote ya Mungu ni ya kuaminika;
yeye ni ngao yao wote wanaomkimbilia.
6Usiongeze neno katika maneno yake,
asije akakukemea, nawe ukaonekana mwongo.
7Mambo haya mawili nakuomba ee Mungu,
wala usinikatalie kabla sijafa:
8Uniondolee uongo na udanganyifu;
usinipe umaskini wala utajiri;
unipatie chakula ninachohitaji,
9nisije nikashiba nikakukana;
nikasema, “Mwenyezi-Mungu ni nani?”
Au nisije nikawa maskini nikaiba,
na kulikufuru jina lako ee Mungu wangu.
10Usimchongee mtumwa kwa bwana wake,
asije akakulaani, ukaonekana una hatia.
11Kuna watu ambao huwalaani baba zao,
wala hawana shukrani kwa mama zao.
12Kuna watu ambao hujiona kuwa wema,
kumbe bado hawajatakaswa uchafu wao.
13Kuna na wengine – kiburi ajabu!
Hudharau kila kitu wanachokiona.
14Kuna watu ambao meno yao ni kama upanga,
na magego yao ni kama visu.
Wako tayari kuwatafuna maskini wa nchi,
na wanyonge walio miongoni mwa watu!"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe sana.

No comments: