Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday 21 March 2019

Kikombe Cha Asubuhi ;Zaburi 86...



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu katika yote....

Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana
Mungu wa walio hai,Mungu  mwenye huruma,Mungu wa upendo
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu

Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!

Mimi Simoni Petro, mtumishi na mtume wa Yesu Kristo, nawaandikia nyinyi ambao, kwa wema wake Mungu wetu na Mwokozi Yesu Kristo, mmejaliwa imani ileile ya thamani kuu tuliyojaliwa sisi. Nawatakieni neema na amani tele katika kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizo zifanya
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Usitutie majaribu Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Kwa uwezo wake wa kimungu, Mungu ametujalia mambo yote tunayohitaji ili tuishi maisha ya kumcha Mungu kwa kumjua yeye aliyetuita tuushiriki utukufu na wema wake yeye mwenyewe. Kwa namna hiyo ametujalia zawadi kuu na za thamani ambazo alituahidia, ili kwa zawadi hizo mpate kuziepa kabisa tamaa mbaya zilizomo duniani, na kuishiriki hali yake ya kimungu.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatuope neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji...
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu,Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe
Yahweh  tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni

Yahweh ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu
Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetuBaba wa Mbinguni tukanene yaliyo yako
Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama
inavyokupendeza wewe

Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

Kwa sababu hiyo, fanyeni bidii ya kuongeza imani yenu kwa fadhila, fadhila yenu kwa elimu, elimu yenu kwa kuwa na kiasi, kuwa na kiasi kwa uvumilivu, uvumilivu wenu kwa uchaji wa Mungu, uchaji wenu kwa urafiki wa kindugu, na urafiki wenu wa kindugu kwa mapendo. Mkiwa na sifa hizo zote kwa wingi, zitawawezesheni kuwa watendaji na kupata faida katika kumjua Bwana wetu Yesu Kristo. Lakini mtu asiye na sifa hizo ni kipofu, hawezi kuona na amesahau kwamba alikwisha takaswa dhambi zake za zamani.
Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu,
wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
kila mmoja na mahitaji yake..
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe
Yahweh tunaomba ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako
nazo zikawaweke huru
Ukawaokoe na kuwalinda,ukawaponye kimwili na kiroho pia..
Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!


 Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,
Mungu Baba aendelee kuwatendea sawasawa na mapezni yake...

Nawapenda.

Kuomba msaada
(Sala ya Daudi)
1Unitegee sikio, ee Mwenyezi-Mungu, unijibu,
maana mimi ni fukara na mnyonge.
2Uyahifadhi maisha yangu maana mimi ni mchaji wako;
uniokoe mimi mtumishi wako ninayekutegemea.
3Wewe ni Mungu wangu;
basi, unionee huruma,
maana nakulilia mchana kutwa.
4Uifurahishe roho yangu mimi mtumishi wako,
maana sala zangu nazielekeza kwako ee Bwana.
5Wewe, ee Bwana, u mwema na mwenye kusamehe;
mwingi wa fadhili kwa wote wakuombao.
6Ee Mwenyezi-Mungu, uitegee sikio sala yangu;
ukisikie kilio cha ombi langu.
7Siku za taabu nakuita,
maana wewe waniitikia.
8Ee Bwana, hakuna Mungu aliye kama wewe;
hakuna awezaye kufanya unayofanya wewe.
9 Taz Ufu 15:4 Mataifa yote uliyoyaumba, yatakuja kukuabudu, ee Bwana;
yatatangaza ukuu wa jina lako.
10Wewe ndiwe mkuu, wafanya maajabu;
wewe peke yako ndiwe Mungu.
11Unifundishe njia yako, ee Mwenyezi-Mungu,
nipate kuwa mwaminifu kwako;
uongoze moyo wangu nikuheshimu.
12Ee Bwana, Mungu wangu, nitakusifu kwa moyo wote;
nitatangaza ukuu wa jina lako milele.
13Fadhili zako kwangu ni nyingi mno!
Umeniokoa kutoka chini kuzimu.
14Ee Mungu, watu wenye kiburi wamenikabili;
kundi la watu wakatili wanataka kuniua,
wala hawakujali wewe hata kidogo.
15Lakini wewe Bwana, ni Mungu wa rehema na huruma;
wewe ni mvumilivu, mwingi wa fadhili na uaminifu.
16Unigeukie, unihurumie;
unijalie nguvu yako mimi mtumishi wako,
umwokoe mtoto wa mjakazi wako.
17Unioneshe ishara ya wema wako, ee Mwenyezi-Mungu,
ili wale wanaonichukia waaibike,
waonapo umenisaidia na kunifariji.



Zaburi86;1-17

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: