Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 12 March 2019

Kikombe Cha Asubuhi ;Zaburi 79...



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu katika yote....

Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana
Mungu wa walio hai,Mungu  mwenye huruma,Mungu wa upendo
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu

Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!

Hekima amejenga nyumba yake, nyumba yenye nguzo saba. Amechinja wanyama wa karamu, divai yake ameitayarisha, ametandika meza yake. Amewatuma watumishi wake wa kike mjini, waite watu kutoka kwenye vilele vya miinuko: “Yeyote aliye mjinga na aje hapa!” Na yeyote aliye mpumbavu humwambia: “Njoo ukale chakula, na unywe divai niliyotengeneza.

Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizo zifanya
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Achana na ujinga upate kuishi; fuata njia ya akili.” Anayemkosoa mwenye dharau hupata matusi, amkaripiaye mwovu huishia kwa kuumizwa. Usimwonye mwenye dharau maana atakuchukia; mwonye mwenye hekima naye atakupenda. Mfunze mwenye hekima naye atazidi kuwa na hekima; mfundishe mwadilifu naye atazidi kuelimika.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji

Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni
tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe....


Yahweh  tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni

Yahweh ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu
Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama
inavyokupendeza wewe

Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....

Kumcha Mwenyezi-Mungu ni msingi wa hekima; na kumjua yule Mtakatifu ni kupata akili. Kwa msaada wangu mimi Hekima siku zako zitaongezwa; utaongezewa miaka mingi maishani mwako. Kama una hekima, itakufaa wewe mwenyewe; kama ukiidharau, mwenyewe utapata hasara. Mwanamke mpumbavu ana kelele, hajui kitu wala hana haya. Hukaa kitako mlangoni mwa nyumba yake, huweka kiti chake mahali pa juu mjini, na kuwaita watu wapitao njiani, watu wanaokwenda kwenye shughuli zao: “Yeyote aliye mjinga na aje hapa!” Na yeyote aliye mpumbavu humwambia: “Maji ya wizi ni matamu sana; mkate unaoliwa kwa siri ni mzuri sana.” Lakini mjinga hajui kwamba humo mna wafu, wageni wa mwanamke huyo wamo chini Kuzimu.
Tazama watoto wako wanaokutafuta/kukuomba kwa bidii na imani, Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu,
wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
kila mmoja na mahitaji yake

Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe Yahweh tunaomba ukawape neema ya kujiombea
Kufuata njia zako nazo zikawaweke huru
Ukawape macho ya rohoni ee Mungu wetu na masikio ya kusikia
sauti yako,Ukawaokoe na kuwalinda,ukawaponye kimwili na kiroho
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao,Amani ikatawale katika maisha yao,Upendo ukadumu kati yao Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako,kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele...
Amina..!



Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,
Mungu Baba aendelee kuwatendea sawasawa na mapezni yake...

Nawapenda.

Wakati wa maafa ya taifa
(Zaburi ya Asafu)
1Ee Mungu, watu wasiokujua wameivamia nchi yako.
Wamelitia najisi hekalu lako takatifu,
na kuufanya mji wa Yerusalemu kuwa magofu.
2Wameacha maiti za watumishi wako ziliwe na ndege,
miili ya watu wako chakula cha wanyama wa porini.
3Damu yao imemwagwa kama maji mjini Yerusalemu,
wamelazwa humo na hakuna wa kuwazika.
4Tumekuwa aibu kwa mataifa ya jirani,
jirani zetu wanatucheka na kutudhihaki.
5Ee Mwenyezi-Mungu, je, utakasirika hata milele?
Hasira yako ya wivu itawaka kama moto hata lini?
6Uwamwagie watu wasiokujua hasira yako;
naam, tawala zote zisizoheshimu jina lako.
7Maana wamemmeza Yakobo, taifa lako,
wameteketeza kabisa makao yake.
8Usituadhibu kwa sababu ya makosa ya wazee wetu.
Huruma yako itujie haraka,
maana tumekandamizwa mno!
9Utusaidie, ee Mungu, mwokozi wetu;
kwa heshima ya jina lako
utuokoe na kutusamehe dhambi zetu,
kwa ajili ya jina lako.
10Kwa nini mataifa yatuambie:
“Yuko wapi Mungu wenu?”
Utujalie tuone ukiwalipiza watu wa mataifa
mauaji ya watumishi wako.
11Kilio cha hao wafungwa kikufikie;
kwa nguvu yako kuu uwaokoe waliohukumiwa kufa.
12Mataifa hayo yaliyokudharau, ee Bwana,
yalipizwe mara saba!
13Nasi watu wako, tulio kondoo wa kundi lako,
tutakushukuru milele,
na kukusifu nyakati zote.


Zaburi79;1-13

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: