Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday 7 March 2019

Kikombe Cha Asubuhi ;Zaburi 76...



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu katika yote....

Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana
Mungu wa walio hai,Mungu  mwenye huruma,Mungu wa upendo
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..
Yahweh..!Jehovah..! Adonai..!Elohim..!El Olam..!El Qanna..!
El Elyon..!El shaddai..!Emanueli...!-Mungu pamoja nasi...
Unastahili sifa Mungu wetu,Unastahili kuabudiwa Jehovah,
Unastahili kuhimidiwa Yahweh,Unastahili Kutukuzwa Baba wa Mbinguni....!


Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu

Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!

Kisha Elihu akaendelea kusema: “Nivumilie kidogo, nami nitakuonesha kitu; maana bado ninacho cha kusema kwa niaba ya Mungu. Nitaleta hekima yangu kutoka mbali sana, na kuonesha kwamba Muumba wangu ni mwadilifu. Kweli maneno yangu si ya uongo; mwenye elimu kamili yuko hapa nawe.

Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizo zifanya
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Usitutie majaribu Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

“Sikiliza Mungu ni mwenye nguvu wala hamdharau mtu yeyote; uwezo wa akili yake ni mkuu mno! Hawaachi waovu waendelee kuishi; lakini huwapatia wanaodhulumiwa haki zao. Haachi kuwalinda watu waadilifu; huwatawaza, wakatawala na kutukuka.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji

Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni
tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe....


Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,

watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka...
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Yahweh ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu...
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahwe tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu
Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu Baba wa Mbinguni tukanene yaliyo yako
ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe
Roho 
akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

Lakini kama watu wamefungwa minyororo, wamenaswa katika kamba za mateso, Mungu huwaonesha matendo yao maovu, na kwamba wao ni watu wenye kiburi. Huwafungua masikio wasikie mafunzo, na kuwaamuru warudi na kuacha uovu.
Tazama watoto wako wanaokutafuta/kukuomba kwa bidii na imani, Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu,
wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukaonekane katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe Yahweh tunaomba ukawape neema ya kujiombea
Kufuata njia zako nazo zikawaweke huru
Ukawape macho ya rohoni ee Mungu wetu na masikio ya kusikia
sauti yako,Ukawaokoe na kuwalinda,ukawaponye kimwili na kiroho
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao,Amani ikatawale katika maisha yao,Upendo ukadumu kati yao...

Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako tukiamini Mungu wetu utawatendea sawasawa na mapenzi yako 
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
 Amina...!!


Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwanami/kunisoma Mungu Baba aendelee
kuwabariki na kuwatendea kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na Upendo wa Mungu wa Mungu Baba ukae nanyi daima
Nawapenda.


Mungu mshindi
(Kwa Mwimbishaji: Na ala za nyuzi za muziki. Zaburi ya Asafu. Wimbo)
1Mungu anajulikana katika Yuda;
jina lake ni kuu katika Israeli.
2Makao yake yamo huko Salemu;76:2 Salemu: Jina la zamani la Yerusalemu.
maskani yake huko Siyoni.
3Huko alivunja mishale ya adui;
alivunja ngao, panga na silaha za vita.
4Wewe, ee Mungu, watukuka mno;
umejaa fahari kuliko milima ya milele.76:4 milima ya milele: Kulingana na tafsiri ya Kigiriki. Kiebrania ni: Milima ya mawindo.
5Wenye nguvu walipokonywa nyara zao,
sasa wamelala usingizi wa kifo,
mashujaa wa vita hawakuweza kutumia mikono yao.
6Ulipowakemea, ee Mungu wa Yakobo,
farasi na wapandafarasi walikufa ganzi.
7Wewe, ee Mungu, ni wa kutisha mno!
Nani awezaye kustahimili mbele yako ukikasirika?
8Ulijulisha hukumu yako toka mbinguni;
dunia iliogopa na kunyamaza;
9wakati ulipoinuka kutekeleza hukumu,
kuwaokoa wote wanaodhulumiwa duniani.
10Ghadhabu ya watu husababisha tu sifa kwako;
na waliookoka vitani watafanya sikukuu zako.76:10 watafanya sikukuu zao: Makala moja ya kale; maana katika Kiebrania si dhahiri.
11Mtimizieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu ahadi zenu;
enyi mlio karibu mpeni zawadi Mungu wa kutisha.
12Yeye huzitoa roho za wakuu;
huwatisha wafalme wa dunia.



Zaburi76;1-12

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: