Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday 14 March 2019

Kikombe Cha Asubuhi ;Zaburi 81...



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu katika yote....

Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana
Mungu wa walio hai,Mungu  mwenye huruma,Mungu wa upendo
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..
Yahweh..!Jehovah..! Adonai..!Elohim..!El Olam..!El Qanna..!
El Elyon..!El shaddai..!Emanueli...!-Mungu pamoja nasi...
Unastahili sifa Mungu wetu,Unastahili kuabudiwa Jehovah,
Unastahili kuhimidiwa Yahweh,Unastahili Kutukuzwa Baba wa Mbinguni....!


Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu

Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!

Mungu alitekeleza kile alichonuia, akatujulisha mpango wake uliofichika, ambao alikuwa ameazimia kuutekeleza kwa njia ya Kristo. Mpango huo ambao angeutimiza wakati utimiapo ni kukusanya pamoja viumbe vyote, kila kitu mbinguni na duniani, chini ya Kristo.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizo zifanya
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Usitutie majaribu Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Katika kuungana na Kristo, sisi tumerithishwa wokovu kama tulivyopangiwa kadiri ya azimio lake Mungu atekelezaye kila kitu kulingana na uamuzi na matakwa yake. Basi, sisi tuliotangulia kumtumainia Kristo tunapaswa kuusifu utukufu wa Mungu!
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji

Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni
tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe....


Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,

watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka...
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Yahweh ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu...
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahwe tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu
ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe
Roho 
akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

Nanyi pia watu wa mataifa mengine, mliusikia ujumbe wa kweli yaani Habari Njema iliyowaletea wokovu, mkamwamini Kristo; naye Mungu, ili kuonesha kuwa nyinyi ni wake, akawapiga mhuri kwa kuwapeni yule Roho Mtakatifu aliyetuahidia. Huyu Roho ni dhamana ya kupata yote yale Mungu aliyowaahidia watu wake, na jambo hili latuhakikishia kwamba Mungu atawakomboa kabisa wote walio wake. Tuusifu utukufu wake!
Tazama watoto wako wanaokutafuta/kukuomba kwa bidii na imani, Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu,
wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
kila mmoja na mahitaji yake
 Yahweh tunaomba ukawape neema ya kujiombea
Kufuata njia zako nazo zikawaweke huru
Ukawaokoe na kuwalinda,ukawaponye kimwili na kirohoNuru yako ikaangaze katika maisha yao,Amani ikatawale katika....

Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako tukiamini Mungu wetu utawatendea sawasawa na mapenzi yako 
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
 Amina...!!


Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwanami/kunisoma Mungu Baba aendelee
kuwabariki na kuwatendea kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na Upendo wa Mungu wa Mungu Baba ukae nanyi daima
Nawapenda.


Wimbo wa sikukuu
(Kwa Mwimbishaji: Mtindo wa Gitithi. Zaburi ya Asafu)
1Mwimbieni kwa sauti Mungu, nguvu yetu,
mshangilieni Mungu wa Yakobo;
2vumisheni wimbo wa shangwe, pigeni ngoma,
chezeni zeze na kinubi cha sauti nzuri.
3Pigeni tarumbeta kutangaza mwezi mwandamo,
na pia mwezi mpevu, wakati wa sikukuu yetu.
4Hiyo ndiyo kanuni katika Israeli;
hilo ndilo agizo la Mungu wa Yakobo.
5Aliwapa watu wa Israeli agizo hilo,
alipoishambulia nchi ya Misri.
Nasikia sauti nisiyoitambua ikisema:
6“Mimi nilikutua mizigo yako mabegani,
nilikuondolea matofali uliyochukua mikononi.
7Ukiwa shidani uliniita, nami nikakuokoa.
Nilikujibu nikiwa mafichoni katika ngurumo.
Nilikujaribu kwenye maji ya Meriba.
8Enyi watu wangu, sikieni onyo langu.
Laiti ungenisikiliza, ee Israeli!
9Asiwepo kwako mungu wa kigeni;
usiabudu kamwe mungu mwingine.
10Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako,
niliyekutoa katika nchi ya Misri.
Fumbua kinywa chako, nami nitakulisha.
11“Lakini watu wangu hawakunisikiliza;
Israeli hakunitaka kabisa.
12Hivyo, nikawaacha wabaki na ukaidi wao;
wafuate mashauri yao wenyewe.
13Laiti watu wangu wangenisikiliza!
Laiti Israeli angefuata njia yangu!
14Ningewashinda maadui zao haraka;
ningenyosha mkono dhidi ya wadhalimu wao.
15Wanichukiao wangenipigia magoti kwa hofu,
na adhabu yao ingekuwa ya milele.
16Lakini wewe ningekulisha kwa ngano bora,
ningekushibisha kwa asali ya mwambani.”



Zaburi81;1-16

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: