Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday 29 January 2020

Kikombe Cha Asubuhi; Yeremia 43....


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu katika yote....

Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana
Mungu wa walio hai,Mungu  mwenye huruma,Mungu wa upendo
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu

Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!

Wayahudi wengi walisikia kwamba Yesu alikuwa Bethania. Basi, wakafika huko si tu kwa ajili ya kumwona Yesu, ila pia wapate kumwona Lazaro ambaye Yesu alimfufua kutoka kwa wafu. Makuhani wakuu waliamua pia kumwua Lazaro, maana kwa sababu ya Lazaro Wayahudi wengi waliwaasi viongozi wao, wakamwamini Yesu.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote 
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Kesho yake, kundi kubwa la watu waliokuja kwenye sikukuu walisikia kuwa Yesu alikuwa njiani kuja Yerusalemu. Basi, wakachukua matawi ya mitende, wakatoka kwenda kumlaki; wakapaza sauti wakisema: “Sifa! Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana. Abarikiwe mfalme wa Israeli.”
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomna ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe...


Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Yahwe ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii..
Baba wa Mbinguni  tunaomba ukatupe neema ya kufuata
njia zako,tukasimamie Neno lako,amri na sheria zako
siku zote za maisha yetu...
Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukatufanye chombo chema
ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....

Yesu akampata mwanapunda mmoja, akapanda juu yake kama yasemavyo Maandiko: “Usiogope mji wa Siyoni! Tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwanapunda!”
Tazama watoto wako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
kila mmoja na mahitaji yake
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipo kwenda kinyume nawe
Yahweh tunaomba ukawape neema ya kuweza kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru...
Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele...
Amina...!!


Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake...
Nawapenda.

Yeremia apelekwa Misri
1Yeremia alipomaliza kuwaambia watu wote maneno yote ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, alimwamuru awatangazie, 2Azaria mwana wa Hoshaia, Yohanani mwana wa Karea na watu wote mafidhuli, walimwambia Yeremia: “Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, hakukutuma wewe utuambie tusiende Misri, tukaishi huko. 3Baruku mwana wa Neria, amekuchochea dhidi yetu ili tutiwe mikononi mwa Wakaldayo watuue au watupeleke uhamishoni Babuloni.” 4Basi, Yohanani mwana wa Karea na makamanda wote wa majeshi pamoja na watu wote hawakutii aliyosema Mwenyezi-Mungu, kwamba wabaki katika nchi ya Yuda. 5Hapo Yohanani mwana wa Karea na makamanda wote wa majeshi waliwachukua watu wote wa Yuda waliosalia ambao walikuwa wamerudi nchini Yuda kutoka mataifa yote ambako walikuwa wametawanywa; 6wanaume, wanawake, watoto, binti za mfalme na kila mtu ambaye Nebuzaradani, kapteni wa walinzi, alikuwa amemwachia Gedalia mwana wa Ahikamu, mjukuu wa Shafani, wakamchukua pia nabii Yeremia na Baruku mwana wa Neria, 7wakaenda nchini Misri, wakawasili mjini Tahpanesi. Ndivyo walivyokataa kutii alichosema Mwenyezi-Mungu
8Basi neno la Mwenyezi-Mungu likamjia Yeremia huko Tahpanesi: 9“Chukua mawe makubwa, ukayafiche katika chokaa ya matofali kwenye lango la ikulu ya Farao mjini Tahpanesi, watu wa Yuda wakiwa wanaona. 10Kisha waambie hivi: Tazameni mimi nitamtuma na kumleta Nebukadneza, mfalme wa Babuloni, mtumishi wangu, naye ataweka kiti chake cha enzi juu ya mawe haya ambayo nimeyaficha hapa, na kutandaza paa la kifalme juu yake. 11Atakapofika ataiangamiza nchi ya Misri. Hapo waliopangiwa kufa kwa maradhi watakufa kwa maradhi, waliopangiwa kuchukuliwa mateka, watachukuliwa mateka; waliopangiwa kufia vitani watafia vitani. 12Mimi nitawasha moto katika mahekalu ya miungu ya Misri; naye Nebukadneza ataiteketeza miungu hiyo kwa moto au kuichukua mateka mpaka Babuloni. Ataisafisha nchi ya Misri kama mchungaji atoavyo kupe katika vazi lake na kuondoka Misri akiwa mshindi. 13Ataivunja minara ya ukumbusho iliyoko huko Heliopoli nchini Misri, na mahekalu ya miungu ya Misri atayateketeza kwa moto.”


Yeremia43;1-13

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: