Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday 27 September 2019

Kikombe Cha Asubuhi;Isaya 21....



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante  Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Neema yako yatutosha  Mungu wetu..!

Miujiza na maajabu mengi yalifanyika kwa njia ya mitume hata kila mtu akajawa na hofu. Waumini wote waliendelea kuwa kitu kimoja na mali zao waligawiana.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa  Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Walikuwa wakiuza mali na vitu vyao kisha wakagawana fedha kadiri ya mahitaji ya kila mmoja. Waliendelea kukutana pamoja kila siku hekaluni. Lakini wakati wa kumega mkate, walikutana katika nyumba zao na wakakishiriki chakula hicho kwa furaha na moyo mkunjufu.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe



Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu  wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo 

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

Walimtukuza Mungu, wakapendwa na watu wote. Kila siku Bwana aliwaongezea idadi ya watu waliokuwa wakiokolewa.
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba
 ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....

Nawapenda.

Maono juu ya kuangamizwa kwa Babuloni
1Kauli ya Mungu dhidi ya jangwa kando ya bahari.21:1 jangwa kando ya bahari: Pengine Babuloni.
Kama vimbunga vinavyovuma kutoka kusini,
wavamizi wanakuja kutoka jangwani,
kutoka katika nchi ya kutisha.
2Nimeoneshwa maono ya kutisha,
maono ya watu wa hila watendao hila,
maono ya watu waangamizi wafanyao maangamizi.
Pandeni juu vitani enyi Waelamu;
shambulieni enyi Wamedi!
Mungu atakomesha mateso yote
yaliyoletwa na Babuloni.
3Kwa maono hayo nimeingiwa na hofu kubwa,
uchungu mwingi umenikumba;
kama uchungu wa mama anayejifungua.
Maumivu yamenizidi hata siwezi kusikia;
nimefadhaika hata siwezi kuona.
4Moyo unanidunda na woga umenikumba.
Nilitamani jioni ifike
lakini ilipofika ikawa ya kutetemesha.
5Chakula kimetayarishwa,
shuka zimetandikwa,
sasa watu wanakula na kunywa.
Ghafla, sauti inasikika:
“Inukeni enyi watawala!
Wekeni silaha tayari!”
6Maana Bwana aliniambia,
“Nenda ukaweke mlinzi;
mwambie atangaze atakachoona.
7Akiona kikosi, wapandafarasi wawiliwawili,
wapandangamia na wapandapunda,
na awe macho;
naam, akae macho!”
8Kisha huyo mlinzi21:8 mlinzi: Kwa kubadili konsonanti na kupatana na hati ya Kumrani na tafsiri ya Peshita. Kiebrania: Simba. akapaza sauti:
“Bwana, nimesimama juu ya mnara wa ulinzi mchana kutwa,
nimeshika zamu usiku kucha!”
9 21:9 Taz Ufu 14:8; 18:2. Tazama, kikosi kinakuja,
wapandafarasi wawiliwawili.
Wanasema: “Babuloni umeanguka! Umeanguka!
Sanamu zote za miungu yake
zimetupwa chini na kuvunjwavunjwa!”
10Ewe Israeli, watu wangu,
enyi mliotwangwa na kupurwa kama nafaka.
Sasa nimewaambieni mambo niliyoyasikia
kwa Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli.
Ufunuo kuhusu Edomu
11Kauli ya Mungu dhidi ya Duma.
Ninasikia mtu ananiita kutoka Seiri:
“Mlinzi, nini kipya leo usiku?
Kuna kipya chochote leo usiku?”
12Nami mlinzi nikajibu:
“Asubuhi inakuja, kadhalika na usiku;
ukitaka kuuliza, uliza tu;
nenda urudi tena.”
Ufunuo kuhusu Arabia
13Kauli ya Mungu dhidi ya Arabia.
Enyi misafara ya Dedani,
pigeni kambi leo usiku kwenye nyika za Arabia.
14Enyi wakazi wa nchi ya Tema,
wapeni maji hao wenye kiu;
wapelekeeni chakula hao wakimbizi.
15Maana wamekimbia mapanga,
mapanga yaliyochomolewa,
pinde zilizovutwa na ukali wa mapigano.
16Maana Bwana aliniambia hivi: “Katika muda wa mwaka mmoja, bila kuzidi wala kupungua, fahari yote ya Kedari itakwisha. 17Wapiga upinde wachache kati ya mashujaa wa watu wa Kedari ndio watakaosalia. Mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nimenena.”

Isaya21;1-17

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: