Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday 1 August 2019

Kikombe Cha Asubuhi ; Methali 31...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu katika yote....

Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana
Mungu wa walio hai,Mungu  mwenye huruma,Mungu wa upendo
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu

Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!

Basi, popote mnapokutana kufanya ibada nataka wanaume wasali, watu waliojitolea kweli na ambao wanaweza kuinua mikono yao wakisali bila hasira wala ubishi. Hali kadhalika, nawataka wanawake wawe wanyofu na wenye busara kuhusu mavazi yao; wavae sawasawa na si kwa urembo wa mitindo ya kusuka nywele, kujipamba kwa dhahabu, lulu au mavazi ya gharama kubwa, bali kwa matendo mema kama iwapasavyo wanawake wamchao Mungu.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote 
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Wanawake wanapaswa kukaa kimya na kuwa wanyenyekevu wakati wa kujifunza. Mimi simruhusu mwanamke amfundishe au amtawale mwanamume; anapaswa kukaa kimya. Maana Adamu aliumbwa kwanza, halafu Hawa.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomna ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe...

Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Yahwe ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii..
Baba wa Mbinguni  tunaomba ukatupe neema ya kufuata
njia zako,tukasimamie Neno lako,amri na sheria zako
siku zote za maisha yetu...
Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukatufanye chombo chema
ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....

Na wala si Adamu aliyedanganywa; bali mwanamke ndiye aliyedanganywa, akaivunja sheria ya Mungu. Hata hivyo, mwanamke ataokolewa kwa kupata watoto, kama akidumu katika imani, upendo, utakatifu na unyofu.
Tazama watoto wako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
kila mmoja na mahitaji yake
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipo kwenda kinyume nawe
Yahweh tunaomba ukawape neema ya kuweza kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru...
Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele...
Amina...!!


Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake...
Nawapenda.

Mawaidha kwa mfalme
1Maneno ya mfalme Lemueli. Mawaidha aliyofundishwa na mama yake:
2Nikuambie nini mwanangu?
Nikuambie nini mwanangu niliyekuzaa?
Nikuambie nini wewe niliyekuomba kwa Mungu?
3Usimalize nguvu zako kwa wanawake,
usiwape mali yako hao wanaoangamiza wafalme.
4Haifai ee Lemueli, haifai wafalme kunywa divai,
wala wakuu kutamani vileo.
5Wakinywa watasahau maagizo ya sheria,
na kuwanyima haki wenye taabu.
6Mpe kileo mtu anayekufa,
wape divai wale wenye huzuni tele;
7wanywe na kusahau umaskini wao,
wasikumbuke tena taabu yao.
8Lakini wewe, lazima useme kwa ajili ya wote walio bubu;
na kutetea haki za wote wasiojiweza.
9Sema kwa ajili yao na kuamua kwa haki,
linda haki za maskini na fukara.
Mke mwema
10Mke mwema kweli, apatikana wapi?
Huyo ana thamani kuliko johari!
11Mumewe humwamini kwa moyo,
kwake atapata faida daima.
12Kamwe hamtendei mumewe mabaya,
bali humtendea mema maisha yake yote.
13Hutafuta sufu na kitani,
na kufanya kazi kwa mikono yake kwa bidii.
14Yeye ni kama meli za biashara:
Huleta chakula chake kutoka mbali.
15Huamka kabla ya mapambazuko,
akaitayarishia jamaa yake chakula,
na kuwagawia kazi watumishi wake.
16Hufikiria kununua shamba, kisha hulinunua,
na kulima zabibu kwa faida ya jasho lake.
17Huwa tayari kufanya kazi kwa nguvu
na kuiimarisha mikono yake.
18Hutambua kwamba shughuli zake zina faida;
hufanya kazi hata usiku kwa mwanga wa taa yake.
19Husokota nyuzi kwa mikono yake mwenyewe,
kwa vidole vyake mwenyewe husuka nguo zake.
20Huufungua mkono wake kuwapa maskini,
hunyosha mkono kuwasaidia fukara.
21Hawahofii watu wake ijapo baridi ya kipupwe,
maana kila mmoja anazo nguo za kutosha.
22Hujitengenezea matandiko,
mavazi yake ni ya zambarau ya kitani safi.
23Mume wake ni mtu mashuhuri barazani,
anakoshiriki vikao vya wazee wa nchi.
24Mwanamke huyo hutengeneza nguo na kuziuza,
huwauzia wafanyabiashara mishipi.
25Nguvu na heshima ndizo sifa zake,
hucheka afikiriapo wakati ujao.
26Hufungua kinywa kunena kwa hekima,
huwashauri wengine kwa wema.
27Huchunguza yote yanayofanyika nyumbani mwake,
kamwe hakai bure hata kidogo.
28Watoto wake huamka na kumshukuru,
mumewe huimba sifa zake.
29Husema, “Wanawake wengi wametenda mambo ya ajabu,
lakini wewe umewashinda wote.”
30Madaha huhadaa na uzuri haufai,
bali mwanamke amchaye Mwenyezi-Mungu atasifiwa.
31Jasho lake lastahili kulipwa,
shughuli zake hazina budi kuheshimiwa popote.

Methali31;1-31

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: