Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 27 August 2019

Kikombe Cha Asubuhi; Wimbo Ulio Bora6...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante  Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Neema yako yatutosha  Mungu wetu..!

Mungu atafanya jambo la haki: Atawalipa mateso wale wanaowatesa nyinyi na kuwapeni nafuu nyinyi mnaoteseka, na sisi pia. Atafanya jambo hilo wakati Bwana atakapotokea kutoka mbinguni pamoja na malaika wake wenye nguvu
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa  Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

na miali ya moto, kuwaadhibu wale wanaomkataa Mungu na wale wasiotii Habari Njema ya Bwana wetu Yesu. Adhabu yao itakuwa kuangamizwa milele na kutengwa mbali na utukufu wake mkuu,
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe

Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu  wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo 

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...


wakati atakapokuja siku ile kupokea utukufu kutoka kwa watu wake na heshima kutoka kwa wote wanaoamini. Nyinyi pia mtakuwa miongoni mwao, kwani mmeuamini ule ujumbe tuliowaletea.
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba
 ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....

Nawapenda.


Wanawake
1Ewe mwanamke uliye mzuri sana;
amekwenda wapi huyo mpenzi wako?
Ameelekea wapi mpenzi wako
ili tupate kushirikiana nawe katika kumtafuta?
Bibi arusi
2Mpenzi wangu amekwenda bustanini mwake,
mahali ambapo rihani hustawi.
Yeye analisha kondoo wake
na kukusanya yungiyungi.
3Mimi ni wake mpenzi wangu, naye ni wangu;
yeye huwalisha kondoo wake penye yungiyungi.
Shairi la tano
Bwana arusi
4Mpenzi wangu, wewe u mzuri kama Tirza,
wapendeza kama Yerusalemu,
unatisha kama jeshi lenye bendera.
5Hebu tazama kando tafadhali;
ukinitazama nahangaika.
Nywele zako ni kama kundi la mbuzi,
wateremkao chini ya milima ya Gileadi.
6Meno yako kama kundi la kondoo majike
wanaoteremka baada ya kuogeshwa.
Kila mmoja amezaa mapacha,
na hakuna yeyote aliyefiwa.
7Mashavu yako ni kama nusu mbili za komamanga,
nyuma ya shela lako.
8Wapo malkia sitini, masuria themanini,
na wasichana wasiohesabika!
9Hua wangu, mzuri wangu, ni mmoja tu,
na ni kipenzi cha mama yake;
yeye ni wa pekee kwa mama yake.
Wasichana humtazama na kumwita heri,
nao malkia na masuria huziimba sifa zake.
10Nani huyu atazamaye kama pambazuko?
Mzuri kama mwezi, mwangavu kama jua,
na anatisha kama jeshi lenye bendera.
11Nimeingia katika bustani ya milozi
kutazama machipuko ya bondeni,
kuona kama mizabibu imechanua,
na mikomamanga imechanua maua.
12Bila kutazamia, mpenzi wangu,
akanitia katika gari la mkuu.6:12 aya ya 12 Kiebrania si dhahiri.
Wanawake
13Rudi, rudi ewe msichana wa Mshulami.
Rudi, rudi tupate kukutazama.
Bibi arusi
Mbona mwataka kunitazama miye Mshulami
kana kwamba mnatazama ngoma
kati ya majeshi mawili?


Wimbo Ulio Bora6;1-13

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: