Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 29 January 2019

Kikombe Cha Asubuhi ;Zaburi 49...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante

 kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Jehovah  Jireh..!Jehovah Nissi..!Jehovah Raah..!
Jehovah Rapha..!Jehovah Shammah..!Jehovah Shamlom..!
Emanuel-Mungu pamohja nasi..!!
Neema yako yatutosha Baba wa Mbinguni..!


Wakati Yesu alipokuwa akifundisha hekaluni, aliuliza, “Mbona waalimu wa sheria wanasema ya kwamba Kristo ni mwana wa Daudi? Daudi mwenyewe akiongozwa na Roho Mtakatifu alisema: ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti upande wangu wa kulia, mpaka niwaweke maadui zako chini ya miguu yako.’ “Daudi mwenyewe anamwita Kristo Bwana. Basi, Kristo atakuwaje mwanawe?” Umati wa watu ulikuwa ukimsikiliza kwa furaha.

Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa  Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona.....

Katika mafundisho yake, Yesu alisema, “Jihadharini na waalimu wa sheria ambao hupenda kupitapita wamejivalia kanzu ndefu na kusalimiwa na watu kwa heshima sokoni; hupenda kuketi mahali pa heshima katika masunagogi, na kuchukua nafasi za heshima katika karamu. Huwadhulumu wajane huku wakijisingizia kusali sala ndefu! Siku ya hukumu watapata adhabu kali.”

Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe



Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu wetu tunaomba ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Baba wa Mbinguni ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo Mungu wetu

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...


Yesu alikuwa ameketi karibu na sanduku la hazina. Akawa anatazama jinsi watu wengi walivyokuwa wakitoa fedha na kuzitia katika hazina ya hekalu. Matajiri wengi walitoa fedha nyingi. Hapo akaja mama mmoja mjane maskini, akatoa sarafu mbili ndogo za fedha. Hapo Yesu akawaita wanafunzi wake, akawaambia, “Kweli nawaambieni, mama huyu mjane maskini ametia katika sanduku la hazina kiasi kikubwa kuliko walichotia wengine wote. Maana wengine wote walitoa kutokana na ziada ya mali zao, lakini huyu mama, ingawa ni maskini, ametoa yote aliyokuwa nayo, ametoa kila kitu alichohitaji kwa kuishi.”

Tazama wenye shida/tabu,watoto wako wanaokutafuta kwa bidii na imani
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
Yahweh tunaomba  ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Mungu wetu  unajua haja za mioyo ya kila mmoja
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Jehovah ukaonekane katika maisha yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....
Nawapenda.


Upumbavu wa kutegemea mali
(Kwa Mwimbishaji. Zaburi ya Wakorahi)
1Sikieni jambo hili enyi watu wote!
Tegeni sikio enyi wakazi wote wa dunia;
2sikilizeni nyote, wakubwa kwa wadogo,
matajiri na maskini kwa pamoja.
3Maneno yangu yatakuwa mazitomazito;
mimi nitasema maneno ya hekima.
4Nitatega sikio nisikilize methali,
nitafafanua kitendawili kwa muziki wa zeze.
5Ya nini niogope siku mbaya,
wakati nizungukwapo na uovu wa adui?
6Watu waovu hutegemea mali zao,
hujisifia wingi wa utajiri wao.
7Lakini binadamu hawezi kamwe kujikomboa mwenyewe;
hawezi kumlipa Mungu bei ya maisha yake,
8maana fidia ya maisha ni kubwa mno.
Hawezi kutoa kitu chochote kinachotosha,
9kimwezeshe aendelee kuishi daima,
asipate kuonja kaburi.
10Yeye afahamu kuwa hata wenye hekima hufa,
wapumbavu hali kadhalika na watu wajinga.
Wote hao huwaachia wengine mali zao.
11Makaburi ni makao yao hata milele;
ni makao yao vizazi hata vizazi,
ingawa hapo awali walimiliki ardhi.
12Binadamu hatadumu katika fahari yake;
atakufa tu kama mnyama.
13Hayo ndiyo yawapatao wanaojiamini kipumbavu,
ndio mwisho wa wale wanaojivunia mali zao.
14Wataongozwa kama kondoo hadi kuzimu,
kifo kitakuwa mchungaji wao.
Watashuka moja kwa moja kaburini.
Miili yao itaozea huko,
Kuzimu kutakuwa makao yao.49:14 maana katika Kiebrania si dhahiri.
15Lakini Mungu ataniokoa na kuzimu.
Atanisalimisha kutoka huko.
16Usihangaike ukiona mtu anatajirika,
wala mali yake ikiongezeka zaidi na zaidi.
17Maana atakapokufa hatachukua chochote,
mali yake haitashuka huko chini pamoja naye.
18Ajapojikuza katika maisha haya,
na kusifiwa kwa sababu ya kufanikiwa,
19atajiunga na wazee waliomtangulia kufa,
ambao hawawezi kuona tena mwanga.
20Binadamu hatadumu milele katika fahari yake,
atakufa tu kama mnyama.


Zaburi49;1-20

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: