Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday 21 January 2019

Kikombe Cha Asubuhi ;Zaburi 43...



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Haleluyah ni siku/wiki  nyingine tena Mungu wetu ametuchagua

na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Si kwamba sisi tumetenda mema sana wala si kwa nguvu zetu
si kwa utashi wetu wala si kwa akili zetu si kwamba sisi
ni wazuri mno si kwa uwezo wetu sisi kuwa hivi tulivyo leo hii
Ni kwa rehema/neema zake ni kwa mapenzi yake Mungu wetu....

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu
Sifa na Utukufu tunakurudshia Mungu wetu....!!

Nimwendee Mwenyezi-Mungu na kitu gani, nipate kumwabudu Mungu aliye juu? Je, nimwendee na sadaka za kuteketezwa, nimtolee ndama wa mwaka mmoja? Je, Mwenyezi-Mungu atapendezwa nikimtolea maelfu ya kondoo madume, au mito elfu na elfu ya mafuta? Je, nimtolee mzaliwa wangu wa kwanza kwa ajili ya kosa langu, naam, mtoto wangu kwa ajili ya dhambi yangu?

Tazama jana imepita ee Mungu wetu leo ni siku mpya na kesho ni siku nyingine Jehovah tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
 Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Jehovah usitutie majaribu Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote
Yahweh tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona
Kwakupigwa kwake sisi tumepata kupona...

Mungu amekuonesha yaliyo mema, ewe mtu; anachotaka Mwenyezi-Mungu kwako ni hiki: Kutenda mambo ya haki, kupenda kuwa na huruma, na kuishi kwa unyenyekevu na Mungu wako. Mwenyezi-Mungu anawaita wakazi wa mji, na ni jambo la busara sana kumcha yeye: “Sikilizeni, enyi watu wa Yuda; sikilizeni enyi mliokusanyika mjini. “Je, nitavumilia maovu yaliyorundikwa nyumbani mwao, mali zilizopatikana kwa udanganyifu, na matumizi ya mizani danganyifu, jambo ambalo ni chukizo? Je, naweza kusema hawana hatia watu wanaotumia mizani ya danganyifu na mawe ya kupimia yasiyo halali? Matajiri wa miji wamejaa dhuluma, wakazi wake husema uongo, kila wasemacho ni udanganyifu.
Yahweh tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe

Baba wa Mbinguni tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu
Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu
Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...


Kwa hiyo nami, nimeanza kuwaangusha chini, na kuwaangamiza kwa sababu ya dhambi zenu. Mtakula lakini hamtashiba; ndani mwenu njaa itazidi kuwauma. Mkiweka akiba haitahifadhiwa, na mkihifadhi kitu nitakiharibu kwa vita. Mtapanda mbegu, lakini hamtavuna. Mtasindika zeituni, lakini hamtatumia hayo mafuta. Mtasindika zabibu, lakini hamtakunywa hiyo divai. Nyinyi mnafuata mfano mbaya wa mfalme Omri na mfano wa jamaa ya mfalme Ahabu na mfano mbaya wa jamaa ya mwanawe, Ahabu, na mmefuata mashauri yao. Kwa hiyo nitawaleteeni maangamizi, na kila mtu atawadharau. Watu watawadhihaki kila mahali.”

Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu,wote wanaopotia magumu/majaribu mbalimbali
watoto wako wanaokuomba kwa bidii na imani
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
 kila mmoja na mahitaji yake 
Yahweh tunaomba ukaonekane katika maisha yao
Jehovah tunaomba ukawaokoe,ukawavushe salama na  kuwalinda
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe
Baba wa Mbinguni ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako
wakasimaie Neno lako nalo likaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kuomba kwetu
Baba wa Mbinguni ukapokee sala/maombi yetu
Mungu wetu ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina...!!

Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami
Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea 
kama inavyompendeza yeye....
Nawapenda.

Sala ya mkimbizi yaendelea
(Zaburi ya 42 yaendelea)
1Onesha kuwa sina hatia ee Mungu;
utetee kisa changu dhidi ya watu wabaya;
uniokoe na watu waongo na waovu.
2Nakimbilia usalama kwako ee Mungu;
kwa nini umenitupilia mbali?
Yanini niende huko na huko nikiomboleza
kwa kudhulumiwa na adui yangu?
3Upeleke mwanga na ukweli wako viniongoze,
vinipeleke kwenye mlima wako mtakatifu,
kwenye makao yako.
4Hapo, ee Mungu, nitakwenda madhabahuni pako;
nitakuja kwako, ee Mungu, furaha yangu kuu.
Nitakusifu kwa zeze, ee Mungu, Mungu wangu.
5Mbona ninahuzunika hivyo moyoni?
Kwa nini nahangaika hivyo ndani mwangu?
Nitamtumainia Mungu,
nitamsifu tena
yeye aliye msaada wangu na Mungu wangu.


Zaburi43;1-5

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: