Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday 12 April 2018

Kikombe Cha Asubuhi ; 2 Wafalme 6......



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah Mungu wetu yu mwema sana
Tumshukuru Mungu wetu katika yote....

Mtakatifu Mtakatifu Mtakatifu....!!
Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyooneka
Jehovah Niss,Jehovah Rapha,Jehovah Raah,Jehovah Shammah,
Jehovah Shalom...!!
Mungu  mwenye nguvu,Mungu wa walio hai,Mungu mwenye huruma
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo....!!

Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea
kuiona leo hii...
Asante kwa kuwanasi/uwepo wako,pumzi/uzima,afya na kuwatayari
kwa majukumu yetu....
Sifa na Utukufu tunakurudishia ee Baba wa Mbinguni...!!


Vitu vyote ni halali, lakini si vyote vinafaa. Vitu vyote ni halali lakini si vyote vinajenga. Mtu asitafute faida yake mwenyewe, ila faida ya mwenzake. Kuleni chochote kile kiuzwacho sokoni bila ya kuulizauliza kwa sababu ya dhamiri zenu; maana Maandiko yasema: “Dunia na vyote vilivyomo ni mali ya Bwana.” Kama mtu ambaye si mwaamini akiwaalikeni nanyi mkakubali kwenda, basi, kuleni vyote atakavyowaandalieni bila kuulizauliza kwa sababu ya dhamiri zenu. Lakini mtu akiwaambieni: “Chakula hiki kimetambikiwa sanamu,” basi, kwa ajili ya huyo aliyewaambieni hivyo na kwa ajili ya dhamiri, msile. Nasema, “kwa ajili ya dhamiri,” si dhamiri yenu, bali dhamiri yake huyo aliyewaambieni. Mtaniuliza: “Kwa nini uhuru wangu utegemee dhamiri ya mtu mwingine?

Mungu wetu tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na
kujiachilia mikononi mwako
Jehovah tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya
kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe
wale wote waliotukosea
Yahweh tunaomba usitutie katika majaribu Mungu wetu utuokoe
na yule mwovu na kazi zake zote
Mungu wetu tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni utufunike kwa Damu ya Bwana na mwokozi wetu
Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona.....


Ikiwa mimi nashiriki chakula hicho huku namshukuru Mungu, kwa nini nilaumiwe kwa chakula ambacho kwa ajili yake nimemshukuru Mungu?” Basi, chochote mfanyacho iwe ni kula au kunywa, fanyeni yote kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Msiwe kikwazo kwa Wayahudi au kwa Wagiriki au kwa kanisa la Mungu. Muwe kama mimi; najaribu kuwapendeza wote kwa kila njia, bila kutafuta faida yangu mwenyewe ila faida ya wote, wapate kuokolewa.

Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Mungu wetu tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Yahweh nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Jehovah tunaomba ukabariki  ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Yahweh nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwabariki
wenye kuhitaji
Mungu wetu tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Baba wa Mbinguni ukatupe kama inavyokupendeza wewe...

Mungu wetu tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki
Mungu wetu tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Yahweh 
tunaomba ukabariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Jehovah
ukatavitakase na kuvifunika kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu tunaomba ukatamalaki na kutuatamia
Jehovah tukawe salama rohoni Mungu wetu tunaomba ukatupe
macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii
Yahweh tunaomba ukatupe neema ya kutambua mema na mabaya
Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu Baba wa Mbinguni
tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako Jehovah tukasimamie
Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu...
Yahweh neema yako na Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Mafalme wa amani amani yako ikatawale na upendo ukadumu kati yetu
Mungu wetu  tunaomba ukatufanye chombo chema Baba wa Mbinguni nasi 
tukatumike kama inavyokupendeza wewe...
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...


Basi, ikiwa mmefufuka pamoja na Kristo, panieni mambo ya juu, kule Kristo aliko, ameketi upande wa kulia wa Mungu. Muwe na hamu ya mambo ya huko juu, na siyo mambo ya hapa duniani. Maana nyinyi mmekufa na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. Uhai wenu halisi ni Kristo, na wakati atakapotokea ndipo nanyi pia mtakapotokea pamoja naye katika utukufu.

Yahweh tazama wenye shida/tabu,wagonjwa,wenye njaa,wanaopitia
magumu/majaribu mbalimbali,walio katika vifungo vya yule mwovu,
walio magerezani pasipo na hatia,walio kataliwa,waliokata tamaa,
wenye hofu na mashaka,walipoteza matumaini,waliokwama kibiashara,
waliokwama kimasomo,walio umizwa na kujeruhiwa rohoni,wenye visasi
na wanaoshidwa kusamehe,walioelemewa na mizigo mizito,wafiwa na
ukaewe mafariji wao Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako
wenye nguvu,Baba wa Mbinguni tunaomba ukawaponye kimwili na kiroho
pia Yahweh tunaomba ukawatue mizigo yao na ukawafungue, Mungu wetu tunaomba 
ukabariki mashamba yao na kazi zao/biashara zao Baba wa Mbinguni
ukawape maarifa na ubunifu Jehovah ukawaokoe na kuwavusha salama
Mungu wetu ukawe tumaini lao Jehovah ukawape neema ya kusamehe
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe na ukawape neema ya kujiombea
kufuata njia zako wakasimamie Neno lako nalo likwawaweke huru
Baba wa Mbinguni ukaonekane katika maisha yao Mungu wetu ukawatendee kila mmoja na hitaji lake Yahweh tunaomba ukasikie
na ukapokee sala/maombi yetu Mungu wetu ukajibu kama inavyokupendeza wewe..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu Hata Milele..
Amina..!!

Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami/kunisoma
Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea sawasawa na mapenzi yake..
Nawapenda.


Shoka lapatikana

1Siku moja, wanafunzi wa manabii walimlalamikia Elisha wakisema, “Mahali hapa tunapokaa ni padogo sana kwetu! 2Turuhusu twende Yordani tukate miti ili tujijengee mahali patakapotutosha.” Elisha akawajibu, “Nendeni.”
3Mmoja wao akamwomba akisema, “Tafadhali uwe radhi uende na watumishi wako.” Naye akajibu, “Nitakwenda.” 4Hivyo akaenda pamoja nao, na walipofika mtoni Yordani wakaanza kukata miti. 5Mmoja wao alipokuwa anakata miti, shoka lake likachomoka na kuanguka majini; akalia, akisema, “Sasa bwana wangu nitafanya nini? Shoka hili tulikuwa tumeliazima!” 6Elisha akauliza, “Liliangukia wapi?” Mtu huyo akamwonesha. Elisha akakata kijiti na kukitupa majini na papo hapo shoka likaelea juu ya maji. 7Elisha akamwamuru alichukue naye akanyosha mkono, akalichukua.

Jeshi la Waaramu lashindwa

8Wakati mmoja kulikuwa na hali ya vita kati ya Aramu na Israeli. Basi, mfalme wa Aramu akashauriana na maofisa wake kuhusu mahali watakaposhambulia. 9Lakini Elisha akampelekea habari mfalme wa Israeli ajihadhari na mahali hapo, kwa kuwa Waaramu walikuwa tayari kupashambulia. 10Basi, mfalme wa Israeli akapeleka askari wake karibu na mahali alipoambiwa. Elisha aliendelea kumwonya mfalme naye mfalme alijiweka katika hali ya tahadhari. Jambo hilo lilifanyika mara nyingi.
11Mfalme wa Aramu akafadhaishwa sana na hali hiyo; akawaita maofisa wake, akawauliza, “Niambieni nani kati yenu anayetusaliti kwa mfalme wa Israeli?”
12Mmoja wao akajibu, “Hakuna anayetusaliti, ee mfalme. Anayehusika ni Elisha, nabii aliyeko huko Israeli. Yeye humwambia mfalme wa Israeli chochote unachosema hata ukiwa katika chumba chako cha kulala.”
13Mfalme akawaambia, “Nendeni mkapeleleze mjue mahali alipo nami nitawatuma watu wamkamate.” Basi, wakamwarifu kwamba Elisha alikuwa huko Dothani. 14Kwa hiyo mfalme akapeleka huko jeshi kubwa pamoja na farasi na magari ya kukokotwa. Jeshi hilo likafika huko wakati wa usiku na kuuzingira mji.
15Mtumishi wa Elisha alipoamka mapema kesho yake na kutoka nje, akaona jeshi pamoja na farasi na magari ya kukokotwa limeuzingira mji. Akarudi ndani akasema, “Ole wetu, ee, Bwana wangu! Sasa tutafanya nini?”
16Elisha akamjibu, “Usiogope kwa sababu walio pamoja nasi ni wengi kuliko walio pamoja nao.” 17Kisha Elisha akaomba, “Ee Mwenyezi-Mungu, umfumbue macho ili apate kuona!” Basi, Mwenyezi-Mungu akamfumbua macho huyo kijana, akaona farasi na magari ya moto yakiwa kila mahali katika mlima wote, kumzunguka Elisha.
18Waaramu waliposhambulia, Elisha alimwomba Mwenyezi-Mungu akisema, “Nakuomba uwafanye watu hawa wawe vipofu!” Mwenyezi-Mungu akasikiliza ombi lake na kuwafanya vipofu. 19Ndipo Elisha akawaendea na kuwaambia, “Mmepotea njia. Huu siyo mji ambao mnautafuta. Nifuateni nami nitawapeleka kwa yule mnayemtafuta.” Naye akawaongoza mpaka Samaria.
20Mara walipoingia mjini, Elisha akaomba, akisema, “Ee Mwenyezi-Mungu, wafumbue macho ili waone.” Mwenyezi-Mungu akasikia ombi lake, akawafumbua macho. Nao wakajikuta wako katikati ya mji wa Samaria. 21Mfalme wa Israeli alipowaona Waaramu, alimwuliza Elisha, “Je, baba, niwaue?” 22Elisha akajibu, “La, usiwaue. Kwani hawa unaotaka kuwaua uliwateka kwa upanga wako na mshale wako? Wape chakula na maji, wale na kunywa kisha uwaache warudi kwa bwana wao.” 23Mfalme wa Israeli akawafanyia karamu kubwa; walipomaliza kula na kunywa, akawarudisha kwa bwana wao. Toka wakati huo, Waaramu hawakuishambulia tena nchi ya Israeli.

Mji wa Samaria wazingirwa

24Baadaye, mfalme Ben-hadadi wa Aramu akakusanya jeshi lake lote akatoka na kuuzingira mji wa Samaria. 25Matokeo yake ilikuwa njaa kali katika mji wa Samaria. Kichwa cha punda kiligharimu vipande themanini vya fedha, na gramu 100 za mavi ya njiwa ziligharimu vipande vitano vya fedha.
26Siku moja mfalme wa Israeli alipokuwa anatembea juu ya ukuta wa mji, alisikia mwanamke mmoja akimwita, “Nisaidie, ee bwana wangu mfalme!” 27Mfalme akamwambia, “Mwenyezi-Mungu asipokusaidia, mimi nitakupa msaada kutoka wapi; kutoka katika kiwanja cha kupuria au kutoka katika shinikizo? 28Shida yako ni nini?” Akamjibu, “Juzi mwanamke huyu alinishauri tumle mwanangu na kesho yake tumle wake. 29Tukampika mwanangu, tukamla. Kesho yake nikamwambia tumle mwanawe, lakini alikuwa amemficha!”
30Mara mfalme aliposikia maneno ya mwanamke huyo alirarua nguo zake kwa huzuni, na watu waliokuwa karibu na ukuta waliona kwamba alikuwa amevaa vazi la gunia ndani yake. 31Naye akasema, “Mungu aniue, Elisha mwana wa Shafati asipokatwa kichwa leo!” 32Ndipo akatuma mjumbe kwenda kumleta Elisha.
Wakati huohuo Elisha alikuwa nyumbani pamoja na wazee waliomtembelea. Kabla ya mjumbe wa mfalme kufika, Elisha akawaambia wazee, “Yule muuaji amemtuma mtu kuja kunikata kichwa! Atakapofika hapa, fungeni mlango, wala msimruhusu aingie. Pia bwana wake anamfuata nyuma.” 33Kabla hata hajamaliza kusema, mfalme akafika, akasema, “Msiba huu umetoka kwa Mwenyezi-Mungu! Kwa nini niendelee kumngojea tena?”




2Wafalme6;1-33


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: