Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday 8 February 2018

Kikombe Cha Asubuhi ; 2 Samueli 8...Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Mungu wetu yu mwema sana tumshukuru katika yote..
Asante Mungu wetu Baba yetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwakutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu..
Mungu wetu ni Mungu wa walio hai,Baba wa upendo,Baba wa faraja,Mungu mwenye kuokoa,Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo,Mungu mwenye huruma,Unatosha ee Mungu wetu,Utukuzwe daima,Usifiwe Baba wa Mbinguni,Uhimidiwe Jehovah,Uabudiwe Yahweh
Matendo yako ni makuu mno,Matendo yako ni ya ajabu,Neema yako yatutosha ee Mungu wetu,Hakuna kama wewe Mungu wetu,Hakuna lisilowezekana mbele zako..!

Nakupenda, ee Mwenyezi-Mungu, nguvu yangu! Mwenyezi-Mungu ni mwamba wangu, ngome yangu na mkombozi wangu; Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia usalama; ngao yangu, nguvu za wokovu wangu na ngome yangu.


Sifa na Utukufu tunakurudshia Baba wa Mbinguni..!!

Tunakuja mbele zako Baba wa Mbinguni tukijinyenyekeza,tukijishusha na kjiachilia mikononi mwako..
Jehovah tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Yahweh nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea..
Mungu wetu tunaomba utuepushe katika majaribu Baba wa Mbinguni utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu Yahweh utufunike kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazareti,yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona...

Huyu Mungu matendo yake hayana dosari! Ahadi ya Mwenyezi-Mungu ni ya kuaminika; yeye ni ngao kwa wote wanaomkimbilia usalama. Nani aliye Mungu isipokuwa Mwenyezi-Mungu? Nani aliye mwamba wa usalama ila Mungu wetu? Mungu ndiye anijaliaye nguvu kila upande; ndiye anayeifanya salama njia yangu. Ameiimarisha miguu yangu kama ya paa, na kuniweka salama juu ya vilele. Hunifunza kupigana vita, mikono yangu iweze kuvuta upinde wa shaba. Umenipa ngao yako ya kuniokoa; mkono wako wa kulia umenitegemeza; wema wako umenifanikisha. Umenirahisishia njia yangu; wala miguu yangu haikuteleza.
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Yahweh tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Mungu wetu nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Jehovah tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji...

Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka..
Baba wa Mbinguni tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki,Yahweh ukatamalaki na kutuatamia,Mungu wetu ukatuongoze tuingiapo/tutokapo Jehovah ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu Yahweh tukawe salama moyoni Baba wa Mbinguni ukatupe macho ya rohoni Jehovah ukatupe masikio ya kusikia sauti yako na kuitii
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Baba wa Mbinguni upendo ukadumu kati yetu,Mungu wetu ukatufanyie njia pasipo na njia,Yahweh ukatuokoe na yote yanayokwenda kinyume nawe,Mungu wetu tukatende yanayokupendeza wewe,Jehovah ukaonekane katika maisha yetu,Mungu wetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo Baba wa Mbinguni..
Yahweh tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako Jehovah tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu
Ukatufanye barua njema Mungu wetu nasi tukasomeke kama inavyokupendeza wewe..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..

Mwenyezi-Mungu ni mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu. Hunipumzisha kwenye malisho mabichi; huniongoza kando ya maji matulivu, na kuirudishia nafsi yangu nguvu mpya. Huniongoza katika njia sawa kwa hisani yake. Nijapopita katika bonde la giza kuu la kifo, sitaogopa hatari yoyote, maana wewe ee Mwenyezi-Mungu u pamoja nami; gongo lako na fimbo yako vyanilinda. Umeniandalia karamu mbele ya maadui zangu; umenipaka mafuta kichwani pangu; kikombe changu umekijaza mpaka kufurika. Kweli wema wako na fadhili zako zitakuwa pamoja nami, siku zote za maisha yangu; nami nitakaa nyumbani mwa Mwenyezi-Mungu milele.

Baba wa Mbinguni tunarudisha sifa,shukrani na utukufu una wewe
Asante kwa matendo yako makuu uliyotutendea/unayoendelea kututendea
Mungu wetu asante kwa uwepo wako katika maisha yetu
Yahweh mkono wako wenye nguvu tumeuona,Mungu wetu Baraka zako na uaminifu wako umeonekana,Mungu wetu asante kwakutujibu na kutupa kile ulichoona kinafaa na siyo tulichoona sisi kinafaa
Jehovah umegusa maisha ya watoto wako waliokuomba na kukufuata
Mungu wetu umeponya Baba wa Mbinguni umetenda,Yahweh umejibu,Jehovah umefungua palipo fungwa,Yahweh umesikia kilio cha watoto wako...
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
na wengine wanaokuomba,wanaokuita,wanaokufuata ,wanaoamini..

Baba wa Mbinguni ukawape neema ya kujiombea na kukujua wewe
Mungu wetu Nuru yako ikaangaze katika maisha yao..
Mungu wetu ukawatendee sawasawa na mapenzi yako..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina!!

Wapendwa katika Bwana Yesu asanteni sana kwakuwa nami
Mungu mwenye nguvu na rehema/neema akaonekane katika maisha yenu
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo ikawe nanyi daima..
Nawapenda.

Ushindi wa kijeshi wa Daudi

(1Nya 18:1-17)

1Baada ya hayo, Daudi aliwapiga, akawashinda Wafilisti. Akauteka mji wa Metheg-ama kutoka utawala wa Wafilisti. 2Kisha aliwashinda Wamoabu. Aliwapanga katika mistari mateka hao, na kuwalaza chini. Aliamuru wale waliokuwa katika mistari miwili wauawe na wale wa mstari wa tatu waachwe hai. Hivyo, Wamoabu wakawa watumishi wake Daudi na wakawa wanamlipa kodi.
3Daudi pia alimshinda Hadadezeri mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba. Daudi alipata ushindi huu wakati Hadadezeri alipokuwa njiani kwenda kulirudisha eneo la mto Eufrate kuwa chini ya utawala wake. 4Daudi aliteka wapandafarasi 1,700, na askari wa miguu 20,000. Kisha Daudi alikata mishipa ya miguu ya nyuma ya farasi wote wa magari, ila alibakiza farasi wa kutosheleza magari 100.
5Nao Waaramu wa Damasko walipokwenda kumsaidia Hadadezeri, mfalme wa Soba, Daudi aliwashambulia na kuwaua watu 22,000. 6Halafu Daudi aliweka kambi za kijeshi katika mji wa Waaramu wa Damasko. Basi, Waaramu wakawa watumishi wake na wakawa wanamlipa kodi. Mwenyezi-Mungu alimpa Daudi ushindi kokote alikokwenda. 7Daudi alizichukua ngao za dhahabu walizobeba wanajeshi wa Hadadezeri na kuzipeleka Yerusalemu. 8Pia alichukua shaba nyingi sana kutoka miji ya Beta na Berothai, iliyokuwa miji ya Hadadezeri.
9Wakati Toi, mfalme wa Hamathi, aliposikia kwamba Daudi amelishinda jeshi lote la Hadadezeri, 10alimtuma mwanawe Yoramu kwa mfalme Daudi kumpelekea salamu na pongezi kwa sababu alikuwa amepigana na Hadadezeri na kumshinda. Maana Hadadezeri alipigana na Toi mara nyingi. Yoramu alimpelekea Daudi zawadi za vyombo vya fedha, dhahabu na shaba. 11Zawadi hizo, pamoja na fedha na dhahabu alizokuwa ameziteka kwa mataifa yote aliyoyashinda, aliziweka wakfu kwa Mwenyezi-Mungu, 12yaani kutoka Edomu,8:12 Edomu: Katika makala ya Kiebrania: Aramu. Moabu, Amoni, Filistia, Amaleki, pamoja na nyara alizoteka kwa mfalme Hadadezeri, mwana wa Rehobu mfalme wa Soba.
13Daudi alijiongezea umaarufu wake. Alipokuwa anarudi baada ya kumshinda Hadadezeri, aliwaua Waedomu 18,000, katika Bonde la Chumvi. 14Akaweka kambi za kijeshi katika Edomu yote. Nao Waedomu wote wa huko wakawa watumishi wake. Mwenyezi-Mungu alimpa Daudi ushindi kokote alikokwenda. 15Hivyo, Daudi akatawala juu ya Israeli yote, akahakikisha watu wake wote wanatendewa haki ipasavyo. 16Yoabu mwana wa Seruya, alikuwa mkuu wa majeshi. Yehoshafati mwana wa Ahiludi, alikuwa mweka kumbukumbu. 17Sadoki mwana wa Ahitubu na Ahimeleki mwana wa Abiathari, walikuwa makuhani. Seraya alikuwa katibu. 18Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa kiongozi wa Wakerethi na Wapelethi,8:18 Wakerethi na Wapekethi walikuwa walinzi binafsi wa Daudi. nao wana wa Daudi wakawa makuhani.


2Samweli8;1-18

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: