Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday 28 February 2018

Kikombe Cha Asubuhi ; 2 Samueli 22...Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote....

Asante Baba wa mbinguni kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwakutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu...
Utukuzwe Mungu wetu,Usifiwe Baba wa Mbinguni,Uhimidiwe Yahweh,Uabudiwe Jehovah...!!
Matendo yako ni makuu sana,Matendo yako yanatisha,Matendo yako ni ya ajabu,Neema yako yatutosha ee Baba wa Mbinguni....

Basi, tuyaache nyuma yale mafundisho ya mwanzomwanzo juu ya Kristo, tusonge mbele kwa yale yaliyokomaa, na sio kuendelea kuweka msingi kuhusu kuachana na matendo ya kifo, na juu ya kumwamini Mungu; mafundisho juu ya ubatizo na kuwekewa mikono; ufufuo wa wafu na hukumu ya milele. Hilo tutafanya, Mungu akipenda. Maana watu waliokwisha kuangaziwa, wakaonja zawadi za mbinguni, wakashirikishwa Roho Mtakatifu na kuonja wema wa neno la Mungu na nguvu za ulimwengu ujao, kisha wakaiasi imani yao, haiwezekani kuwarudisha hao watubu tena. Hao wanamsulubisha tena Mwana wa Mungu kwa makusudi na kumwaibisha hadharani.

Yahweh tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Baba wa Mbinguni
Jehovah tunaomba utusamehe makosa yetu yote tuliyotenda
kwakuwaza,kwakunena,Kwakutenda,kwakujua/kutojua...
Mungu wetu nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Yahweh tunaomba utuepushe katika majaribu Baba wa Mbinguni
utuokoe na yule mwovu  na kazi zake zote
Jehovah tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni utufunike kwa damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....


Ardhi ambayo huipokea mvua inayoinyeshea mara kwa mara na kuotesha mimea ya faida kwa mkulima imebarikiwa na Mungu. Ardhi ikiota miti ya miiba na magugu, haina faida; karibu italaaniwa na Mungu na mwisho wake ni kuchomwa moto. Ingawa twasema namna hii, wapenzi wetu, tuna uhakika wa kupewa mambo mema zaidi: Yaani wokovu. Mungu hakosi haki; yeye hataisahau kazi mliyoifanya au upendo mliyoonesha kwa ajili yake katika huduma mliyowapa na mnayowapa sasa watu wake. Hamu yetu ni kwamba kila mmoja wenu aoneshe bidii hiyohiyo mpaka mwisho, ili yale mnayotumainia yapate kutimia. Hivyo msiwe wavivu, bali muwe kama wale wanaoamini na wenye uvumilivu, wakapokea yale aliyoahidi Mungu.

Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni ukatupe maarifa na ubunifu katika utendaji
Yahweh nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako..
Mungu wetu tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Yahweh nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwabariki
wenye kuhitaji...
Jehovah tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni
ukatupe kama inavyokupendeza wewe...

Mfalme wa amani tunaomba amani yako ikatawale katika maisha yetu
Baba wa Mbinguni tuaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Baba wa Mbinguni tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote
tunavyovimiliki,Yahweh ukatamalaki na kutuatamia,Mungu wetu tukawe salama moyoni Baba wa Mbinguni ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii....
Jehovah ukaonekane  katika maisha yetu Mungu wetu popote tupitapo
na ikajulikane kwamba upo Baba wa Mbinguni...
Mungu wetu ukatubariki tuingiapo/tutokapo Yahweh ukabariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Jehovah tunaomba ukavitakase na 
kuvifunika kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo....
Jehovah tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako
siku zote za maisha yetu...
Mungu wetu ukatufanye barua njema nasi tukasomeke kama inavyokupendeza wewe..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...Mungu alipompa Abrahamu ahadi, aliapa kwa jina lake mwenyewe, maana hakuna aliye mkuu kuliko Mungu ambaye kwa huyo angeweza kuapa. Mungu alisema: “Hakika nitakubariki na nitakupa wazawa wengi.” Abrahamu alisubiri kwa uvumilivu na hivyo akapokea kile alichoahidiwa na Mungu. Watu wanapoapa, huapa kwa mmoja aliye mkuu kuliko wao, na kiapo husuluhisha ubishi wote. Naye Mungu aliimarisha ahadi yake kwa kiapo; na kwa namna hiyo akawaonesha wazi wale aliowaahidia kwamba hatabadili nia yake. Basi, kuna vitu hivi viwili: Ahadi na kiapo, ambavyo haviwezi kubadilika na wala juu ya hivyo Mungu hawezi kusema uongo. Kwa hiyo sisi tuliokimbilia usalama kwake, tunapewa moyo wa kushikilia imara tumaini lililowekwa mbele yetu. Tunalo tumaini hilo kama nanga ya maisha yetu. Tumaini hilo lapenya mpaka mahali patakatifu mbinguni. Yesu mwenyewe ametangulia kuingia humo kwa ajili yetu na amekuwa kuhani mkuu milele, kwa utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki.Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
watoto wako wanaokuita,wanaokungojea,wanaokulilia na kukuomba
kwa bidii na imani...
Yahweh ukawape neema ya kujiombea na kufuata njia zako
nazo ziwaweke huru,Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Amani ikatawale,Baba wa Mbinguni ukawasamehe wale waliokwenda kinyume nawe...
Baba wa Mbinguni tunaomba ukasikie kulia kwao
Yahweh ukawafute machozi yao Mungu wetu ukasikie 
na ukapokee sala/maombi yetu Jehova ukajibu sawasawa na mapenzi yako...
Kwakuwa ufalme ni wako Nguvu na utukufu hata Milele...
Amina..!!

Asanteni sana wapendwa katika kristo Yesu kwa kuwanami/kunisoma
Mungu wetu akawabariki nakuwatendea kama inavyompendeza yeye
Nawapenda.

Wimbo wa ushindi wa Daudi

1Daudi alimwimbia Mwenyezi-Mungu maneno ya wimbo ufuatao siku ile Mwenyezi-Mungu alipomkomboa mikononi mwa adui zake, na mkononi mwa Shauli. 2Alisema,
“Mwenyezi-Mungu ni mwamba wangu,
ngome yangu, na mkombozi wangu.
3Mungu wangu, mwamba wangu, ninayemkimbilia usalama;
ngao yangu, nguvu ya wokovu wangu,
ngome yangu na kimbilio langu.
Mwokozi wangu; unaniokoa kutoka kwa watu wakatili.
4Namwita Mwenyezi-Mungu astahiliye sifa anisaidie,
nami naokolewa kutoka kwa adui zangu.
5“Maana mawimbi ya kifo yalinizingira,
mafuriko ya maangamizi yalinivamia;
6kamba za kuzimu zilinizinga,
mitego ya kifo ilinikabili.
7“Katika taabu yangu, nilimwita Mwenyezi-Mungu;
nilimwita Mungu wangu.
Toka hekaluni mwake aliisikia sauti yangu,
kilio changu kilimfikia masikioni mwake.
8“Hapo, dunia ikatetemeka na kutikisika,
misingi ya mbinguni ikayumbayumba na kuruka,
kwani Mungu alikuwa amekasirika.
9Moshi ulifuka kutoka puani mwake,
moto uunguzao ukatoka kinywani mwake,
makaa ya moto yalilipuka kutoka kwake.
10Aliinamisha anga, akashuka chini;
na wingu jeusi chini ya miguu yake.
11Alipanda kiumbe chenye mabawa22:11 kiumbe chenye mabawa; Kiebrania: Kerubi. na kuruka,
alionekana juu ya mabawa ya upepo.
12Alijizungushia giza pande zote,
kifuniko chake kilikuwa mawingu mazito na mkusanyiko wa maji.22:12 makala ya Kiebrania si dhahiri.
13Umeme ulimulika mbele yake,
kulilipuka makaa ya moto.
14Mwenyezi-Mungu alinguruma kutoka mbinguni,
Mungu Mkuu akatoa sauti yake.
15Aliwalenga adui mishale, akawatawanya,
alirusha umeme, akawatimua.
16Mwenyezi-Mungu alipowakemea,
kutokana na pumzi ya puani mwake,
vilindi vya bahari vilifunuliwa,
misingi ya dunia ikaonekana.
17“Mungu alinyosha mkono wake toka juu, akanichukua,
kutoka kwenye maji mengi alininyanyua.
18Aliniokoa kutoka kwa adui yangu mwenye nguvu,
aliniokoa kutoka kwa hao walionichukia
maana walikuwa na nguvu nyingi kunishinda.
19Walinivamia nilipokuwa taabuni,
lakini Mwenyezi-Mungu alikuwa kinga yangu.
20Alinileta, akaniweka mahali pa usalama,
alinisalimisha, kwani alipendezwa nami.
21“Mwenyezi-Mungu alinipa tuzo kadiri ya uadilifu wangu;
alinituza kwa vile mikono yangu haina hatia.
22Maana, nimefuata njia za Mwenyezi-Mungu,
wala sikujitenga na Mungu wangu kwa uovu.
23Nimeshika maagizo yake yote,
sikuacha kufuata masharti yake.
24Mbele yake sikuwa na hatia,
nimejikinga nisiwe na hatia.
25Mwenyezi-Mungu amenituza kadiri ya uadilifu wangu,
yeye anajua usafi wangu.
26“Wewe ni mwaminifu kwa walio waaminifu,
mwema kwa wale walio wema.
27Wewe ni mkamilifu kwa walio wakamilifu,
lakini mkatili kwa watu walio waovu.
28Wewe wawaokoa walio wanyenyekevu,
lakini wawaangalia wenye majivuno kuwaporomosha.
29Ee Mwenyezi-Mungu, wewe u taa yangu,
Mungu wangu, unayefukuza giza langu.
30Kwa msaada wako, wakishambulia kikosi;
wewe wanipa nguvu ya kuruka kuta zake.
31Anachofanya Mungu hakina dosari!
Ahadi ya Mwenyezi-Mungu ni ya kuaminika;
yeye ni ngao kwa wote wanaomkimbilia.
32“Nani aliye Mungu isipokuwa Mwenyezi-Mungu?
Nani aliye mwamba wa usalama ila Mungu wetu?
33Mungu huyu ndiye kimbilio langu imara,
na ameifanya njia yangu iwe salama.22:33 makala ya Kiebrania si dhahiri.
34Ameiimarisha miguu yangu22:34 yangu: Au yake. kama ya paa,
na kuniweka salama juu ya vilele.
35Hunifunza kupigana vita,
mikono yangu iweze kuvuta upinde wa shaba.
36Umenipa ngao yako ya kuniokoa;
msaada wako umenifanya mkuu.
37Umenirahisishia njia yangu;
wala miguu yangu haikuteleza.
38Niliwafuatia adui zangu na kuwaangamiza,
sikurudi nyuma mpaka wameangamizwa.
39Niliwaangamiza, nikawaangusha chini
wasiweze kuinuka tena;
walianguka chini ya miguu yangu.
40Wewe ulinijalia nguvu ya kupigana vita;
uliwaporomosha adui chini yangu.
41Uliwafanya adui zangu wakimbie,
na wale walionichukia niliwaangamiza.
42Walitafuta msaada, lakini hapakuwa na wa kuwaokoa,
walimlilia Mwenyezi-Mungu, lakini hakuwajibu.
43Niliwatwanga na kuwaponda kama mavumbi ya nchi,
nikawaponda na kuwakanyaga kama matope barabarani.
44“Wewe uliniokoa na mashambulizi ya watu wangu,22:44 sehemu ya aya hii makala ya Kiebrania si dhahiri.
umenifanya mtawala wa mataifa.
Watu nisiowajua walinitumikia.
45Wageni walinijia wakinyenyekea,
mara waliposikia habari zangu walinitii.
46Wageni walikufa moyo;
wakaja kutoka ngome zao wakitetemeka.22:46 wakitetemeka: Kiebrania: Wamejifunga wenyewe.
47“Mwenyezi-Mungu yu hai!
Asifiwe mwamba wangu!
Atukuzwe Mungu wangu, mwamba wa wokovu wangu.
48Yeye ameniwezesha kulipiza kisasi
na kuyatiisha mataifa chini yangu.
49Ameniokoa kutoka adui zangu.
Ee Mwenyezi-Mungu, ulinikuza juu ya wapinzani wangu
na kunisalimisha mbali na watu wakatili.
50“Kwa hiyo, nitakutukuza kati ya mataifa,
ee Mwenyezi-Mungu, nitaliimbia sifa jina lako.
51Mungu humjalia mfalme wake ushindi mkubwa;22:51 Mungu … mkubwa: Au yeye ni mnara wa wokovu.
humwonesha fadhili zake huyo aliyemweka wakfu,
naam, humfadhili Daudi na wazawa wake milele.”


2Samweli22;1-51

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: