Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday 29 December 2011

Ulale kwa Amani da'Halima Mchuka!!!!!

DADA HALIMA WAKATI WA UHAI WAKE.

Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania, TBC – HALIMA MCHUKA amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya MUHIMBILI Jijini DSM alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa kiharusi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa TBC CLEMENT MSHANA, HALIMA MCHUKA alikimbizwa katika hospitali ya DAR GROUP na baadae katika hospitali ya Taifa ya MUHIMBILI hapo jana baada ya kuanguka ghafla akiwa katika kituo chake cha kazi eneo la PUGU ROAD Jijini DSM.
MCHUKA alikuwa mtangazajii wa kwanza wa kike wa mpira AFRIKA MASHARIKI.

               Poleni sana Familia ya Mchuka kwa wakati huu mgumu kwenu.


                                                       R.I.P. DA'HALIMA.

No comments: