Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday 7 September 2011

Watoto wa Shule na Tamaa!!!!!

                       Hawa wanandika kwenye ubao na chaki.
                                  Hawa wanamsikiliza mwalimu kwa tabasamu.
                                Hawa wamenyoosha mkono ili wapewe nafasi ya kujibu/kuuliza.
Baadhi ya Shule  zimeshafunguliwa hapa U.k.
watoto wa shule kila kona sasa, lakini baadhi yao walivyo jiremba mmhh,
mpaka  kugundua kama ni mwanafunzi ipo kazi.

Hili pia lipo kwa baadhi ya shule Afrika/Tanzania, hasa hizi shule za kulipia.
Sijui ndiyo kwenda na wakati auu....... Ninawaza tuu!!!!!


Mpendwa unafikiri kwa nini  baadhi ya watoto wa Shule wanakuwa na Tamaa?[1].Ni utoto tuu wakikuwa wataacha,Kutoridhika na maisha yao au...?[2.] Nivyema kwa watoto wa Shule kuvaa sare za shule au kutovaa sare kila mmoja aje na nguo zake?
[3.]Kupata chakula cha aina moja Shule au kila mtu ajitegemee.

Karibuni sana kwa Maoni,Kuelimishana katika malezi ya watoto wetu!!!!!!



Tuesday 30 August 2011

Nawatakia Eid Mubarak . Tunapo kula na kunywa, Tusisahau na Wenye Shida!!!!!

Nawatakieni kheri na Baraka  wakati huu wa Eid na Siku zote!!!
Tunapokula na Kunywa, Tusiwasahau Wenye Shida na Tabu, Wagonjwa,Wajane na Yatima, Waliomagerezani pasipokuwa na Hatia.Tugawane tulichonacho ili Tufurahi pamoja!!!!!

Mungu Atubariki Sote.

Saturday 27 August 2011

Jikoni Leo ni kwa da'Maggie!!!!!!!!!

             Chapati,Maandazi,Vitumbua.
                   Kitu cha chapati.
                                Kitu cha maandazi.
                         Kitu cha Vitumbua.


Mmmmhhh Sina lakusema zaidi nakuachia wewe Mpendwa uliye Tembelea hapa, nini unapenda hapo na unapenda kushushia na nini.
Mimi zamani nilifikiri wanaojua kupika Vitumbua ni wazee tuu, kumbe laaaa.
Pia nilikuwa najua Mama yangu tuu ndiye mpishi mzuri!!!!!


Huko Ilala kuna mama alikuwa anapika Vitumbua mpaka tukamwita mama Tatu Vitumbua.


Swali kidogo, Hivi mpishi mzuri kwenye familia anaweza kurithisha na wengine?.


Karibuni Wote.

Wednesday 24 August 2011

Mswahili Wetu Leo ni Mh; Balozi Mama Mwanaidi wa Maajar!!!!!!!




Mh; Mama Mwanaidi  Maajar; Aliongea hayo kwenye Semina ya Kina mama wa THE WAY OF THE CROSS GOSPEL MINISTRIES CHURCH.
Mpendwa baada ya kumsikiliza mama Maajar, Je  umejifunza nini?.Sikiliza kwa makini sehemu ya 1 na ya 2.

Karibuni sana kwa mawazo/maoni na kuelimishana zaidi katika kipengele hiki cha, Waswahili na Maisha yao ,Kupitia hapa Swahili naWaswahili.

Habari  kwa msaada wa DjLuke wa  Vijimambo.



Saturday 20 August 2011

Miriam Atimiza Miaka 3!!!!!!!!!

                      Da'Miriam katika poziii.

                                    Keki zote za Miriam.


                       Akijaribu kuzima huku akiogopa.
                               Miriam akisaidiwa kukata keki.
                        Nakupenda sana mama chukua hii,wapambe wakishuhudia.
                            Miriam, Nami nakupenda sana mwanangu nawe kula eehh.
                        Huyu alilishwa kwa niaba ya watoto wa kiume.
                               Na kwaniaba ya watoto wa kike naye alilishwa huyu.
   Mwenyekiti wa wanaume wa Coventry Swahili Christian Fellowship,Alihakikisha kila mtoto anapata keki.
 Mwenyekiti wa watoto wa Coventry Swahili Christian Fellowship,Akishughulika.
                       Watoto wa Kiswahili wakipata chakula.


    Mama hapo akishushia na maji ,Watoto wakifurahi kwa kumaliza vyema na walifungashiwa.
Da'Miriam na mama yake wanasema Asanteni sana kwa kuungana nao katikasiku hii Muhimu kwao.
Pia Shukrani za pekee ziwaendee wana Coventry Swahili Christian Fellowship na Wageni wote.
Anawapenda sana na Mungu awabariki.


Nasi Swahili naWaswahili,Tunakutakia maisha mema na yenye Amani siku zote!!!!!!!

Thursday 18 August 2011

Jikoni Leo ni Mihogo!!!!!!!!

        Hapa ni mihogo  iliyotiwa/kuungwa nazi ipo Jikoni .
             Hapa imepakuliwa na ipo tayari kwa kuliwa.
       Hii ni Mihogo  iliyo chemshwa/ya kuchemshwa.
    Hii ni Mihogo iliyokaangwa/yakukaangwa.



Mpendwa Leo ni Mihogo,kuna mapishi mengi katika Mihogo,wengine wanapenda Kuchemsha,Kukaanga,Kutia/Kuunga nazi.
Pia hiyo ya nazi kuna wanaochanganya na Maharage au Kunde .....n.k,Pia kuna wanaokula kwa Samaki au Mchuzi wowote.


Hiyo ya kuchemsha,kuna wanaokula kwa Kachumbari.
Kuna hii ya Kukaanga duhh hii inanikumbusha sana Shule!!Kuna wanaokula kwa Chachandu,Pilipili ya Unga,Chumvi na.....


Wewe unapenda Mihogo? Je Hupendelea ya aina gani na Kula au kuongezea na nini?.
Kinywaji gani pia unapendelea kushushia?


Karibuni sana Waungwana katika Jikoni Leo.
Nanyi  pia mnaruhusiwa kutuma/kushiriki nasi, Nini unapenda au unapika.
Tuma kupitia Rasca@hotmail.co.uk.


KARIBUNI WOTE!!!!











Monday 15 August 2011

Waswahili wa Mji wa Cork,Ireland na Futari ya Pamoja!!!!!

                         Mji wa Cork katika picha.
     Wanawake wakipika na kina baba wakijiandaa kupokea wageni.
           Waandazi/waandaaji wakiwa tayari.
              Waswahili hawa nao walikuwepo.
         Watoto wa kiswahili wametulia.
   Shekhe akisisitiza Upendo na Umoja kwa Waswahili.
     Waswahili wakisaidiana ili mambo yawe sawa.
         Kina mama na kina kaka wakiendelea na maandalizi.
 Wakiendelea na Futari.
         
  Kina mama wakishughulika.
    Lete Uji hapa!
    Vipi mko sawa!
    Baada ya kumaliza msosi.
   Wakisikiliza maongezi.
    Watu wa karibu baada ya wageni kuondaka wakijipongeza!
                                      Maalim akitoa Shukrani kwa wote waliofika na wasiofika,Mungu awabariki sana na kuwaongezea kila lililo jema na Amani.Anawatakia Funga njema na anawapenda wote.

Shughuli hii ya Futari ya pamoja iliandaliwa na Maalim picha ya chini mwenye kanzu.Kwa kumshukuru Mungu na kuunagana na familia,pia kuwashukuru Wasawhili na jamaa zake kwa kuwa naye pamoja kwa kila jambo.