Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Saturday 27 August 2011

Jikoni Leo ni kwa da'Maggie!!!!!!!!!

             Chapati,Maandazi,Vitumbua.
                   Kitu cha chapati.
                                Kitu cha maandazi.
                         Kitu cha Vitumbua.


Mmmmhhh Sina lakusema zaidi nakuachia wewe Mpendwa uliye Tembelea hapa, nini unapenda hapo na unapenda kushushia na nini.
Mimi zamani nilifikiri wanaojua kupika Vitumbua ni wazee tuu, kumbe laaaa.
Pia nilikuwa najua Mama yangu tuu ndiye mpishi mzuri!!!!!


Huko Ilala kuna mama alikuwa anapika Vitumbua mpaka tukamwita mama Tatu Vitumbua.


Swali kidogo, Hivi mpishi mzuri kwenye familia anaweza kurithisha na wengine?.


Karibuni Wote.

7 comments:

mamii said...

mpendwa kwanza umeni furahisha sana na vitafundwa maana kwetu wengine adimu sana ninge bahatika kuvipata na chai ya maziwa, pili ulidhani wapishi wa vitumbua ni wabibi tu ha ha ha,nikutupie swali kwako tena umesema ulikuwa una jua mama ndiye mpishi mzuri sasa je umerithi?kama umerithi basi inawezekana ikarithishwa kwenye familia sijui nimejibu swali ubarikiwe sana

mamii said...

ha ha ha ni vitafunwa samahani mate yalikuwa yameni jaa kwa uroho wa mahanjumati

Simon Kitururu said...

Mie hapoo kwenye vitumbua ndiko nilikodakwa!:-(

Rachel Siwa said...

hahahah @Mamii mmhh sijui kama nimerithi,sasa nimegundua si wazee tuu wangu!!.hapo ndipo diet inaponishinda mwehh.

Yasinta Ngonyani said...

Hapa kuchagua itakuwa ngumu...cha kutemshia ni chai bila sukari bila maziwa:-) sidhani kama upishi unarithishwa..Rachel unajua kutamanisha watu wewe....
Mtakatifu! wewe na vitumbua tu? je unatemshia nini?..:-)

emu-three said...

Mhh, jamani mimi badi nimefunga...nitasema nikifuturu. TUPO PAMOJA NDUGU YANGU

EDNA said...

yam yam udenda unanidondoka.