Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday 1 August 2011

Siku kama ya Leo Rachel-Siwa Alizaliwa!!!!!!!!

Siku kama ya leo, Familia ya Bibi na Bwana M.S. Kiwinga walibahatika kupata mtoto  wa kike ;Rachel-siwa.
Nawashukuru sana Wazazi wangu kwa Malezi yenu mema na  yote mliyonitendea.
Pia nakushukuru sana kaka yangu R.Kiwinga kwa kupokea ulezi na kunitunza, Tangu pale Baba alipofariki mpaka pale uliponikabidhi kwa Mume,Sina cha kukulipa bali sitoacha kukuombea.


Ahsante sana Mume wangu Issac kwa yote na kuwapamoja siku zote mpaka 27/07/11 yaani j'tano iliyopita tumetimiza miaka 15 ya ndoa yetu,Mungu atubariki sana katika maisha yetu.

Basi niwashukuru Ndugu,Jamaa,Marafiki zangu woooooteee, kwa Yote,kwani nikiandika hapa hapatatosha.


NENO LA LEO; Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika,kama sina Upendo,nimekuwa shaba iliyo na upatu uvumao.Tena nijapokuwa na unabii,na kujua siri zote na maarifa yote,nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina Upendo,si  kitu mimi.Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina Upendo, hainifaidii kitu. Upendo Hufadhili; Upendo Hauhusudu; Upendo Hautakabari; Haujivuni; Haukosi kuwa na adabu; Hautafuti mambo yake; Hauoni uchungu; Hauhesabu mabaya; Haufurahii udhalimu,bali Hufurahia pamoja na kweli.!!!


MUNGU ATUBARIKI SOTE!!!!!!!!!

11 comments:

Anonymous said...

Ghawiza sana mayo wane, sebha akujiwe sana yaani kabisa kabisa.

Anonymous said...

Iii! Mayo, tuli basukuma bose

Goodman Manyanya Phiri said...

Karibu, tena, Duniani Hapa, Dada Rachel!

Siku tena 365 zijazo mimi nakutakia UPEWE MAWILI TU:

1. Uwezo wa kutahamaki Ardhi hii ndio mama yako kwa sasa hivi: UKILILIA WEMBE MAMA ATAKUPA TU, NA UKILILIA MEMA NA YA BUSARA UTAPEWA VILE-VILE.


2. Binadamu wote, wazuri kwa wabaya, ni watoto wa Ardhi hii moja na wote umepewa ili wakutumikie WEWE MALKIA RACHEL mradi tu unawaheshimu wote sawasawa bila kuwabagua kwa uzuri au ubaya wao, utajiri au umaskini vilevile uwerevu kwa ujinga wao KWANI MBELE ZAKE MOLA HAKUNA MJINGA, MASKINI AU MBAYA WA KUPINDUKIA.

BARAKA HIZO KUTOKA HAPA BONDENI, PRETORIA (HAPPY BIRTHDAY)!

chib said...

Hongera sana kwa kumbukumbu nzuri kama hii

Mija Shija Sayi said...

Hongera sana Da' Rachel kwa kutimiza miaka ya kuzaliwa na ya ndoa, mimi na familia yangu tunakuombea kila la heri, Mungu akupe miaka mingi tena yenye furaha na zaidi akuwezeshe kutimiza ndoto zako kwani kila jambo linawezekana ukinia...

Ngoja nikuache msukuma wewe.. Take Care!!

God Bless!!

emu-three said...

Tunakupa hongera sana kwa siku yako ya kuzaliwa, mungu akuzidishie umri,afya na baraka tele...!

EDNA said...

Hongera sana Mdada Mungu akuzidishie miaka mingi duniani.

Rachel Siwa said...

Ahsante sana Wapendwa wangu kwa yote nimeyapoke, Mungu atubariki sote, Wasukuma nyie manamambo sana, nawaandalieni kitu si muda marefu nitawarusha, hahahhhaa.

kaka Manyanya, neno hilo;Binadamu wote wazuri kwa wabaya ni watoto.....

Simon Kitururu said...

Mungu akubariki sana Da Rachel!

Anonymous said...

ameen kwa sote inshallah kwa barka za mwezi mtukufu wa ramadhan ..mungu akubariki da rachel siwa na akupe maisha marefu

Rachel Siwa said...

Amina kaka wamimi @Kituru.

Aonymous;Aminaaaa Asanteni sana.