Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday 18 August 2011

Jikoni Leo ni Mihogo!!!!!!!!

        Hapa ni mihogo  iliyotiwa/kuungwa nazi ipo Jikoni .
             Hapa imepakuliwa na ipo tayari kwa kuliwa.
       Hii ni Mihogo  iliyo chemshwa/ya kuchemshwa.
    Hii ni Mihogo iliyokaangwa/yakukaangwa.Mpendwa Leo ni Mihogo,kuna mapishi mengi katika Mihogo,wengine wanapenda Kuchemsha,Kukaanga,Kutia/Kuunga nazi.
Pia hiyo ya nazi kuna wanaochanganya na Maharage au Kunde .....n.k,Pia kuna wanaokula kwa Samaki au Mchuzi wowote.


Hiyo ya kuchemsha,kuna wanaokula kwa Kachumbari.
Kuna hii ya Kukaanga duhh hii inanikumbusha sana Shule!!Kuna wanaokula kwa Chachandu,Pilipili ya Unga,Chumvi na.....


Wewe unapenda Mihogo? Je Hupendelea ya aina gani na Kula au kuongezea na nini?.
Kinywaji gani pia unapendelea kushushia?


Karibuni sana Waungwana katika Jikoni Leo.
Nanyi  pia mnaruhusiwa kutuma/kushiriki nasi, Nini unapenda au unapika.
Tuma kupitia Rasca@hotmail.co.uk.


KARIBUNI WOTE!!!!10 comments:

Anonymous said...

mimi napenda mihogo ya kukaanga halafu ukute mihogo yenyewe ni ile enyeungaunga basi nile na kachumbari na mishikaki niteremshiee na juice

Yasinta Ngonyani said...

Kwanza napenda kusema nimeipenda picha yako ya prof. Kuhusu mihogo mimi huwa napenda kwanza kabisa kutafuna kama ilivyo na kutelmshia na maji...pia napenda ya kuchemsha pia kutelemshia maji au chai..bila sukari. Rachel hata mimi nimekumbuka shulenipia ..mweeehh kaaaazi kwelikweli

Simon Kitururu said...

Mi udenda tu unanitoka!Mie kama muhogo ni mzuri vyovyote uandaliwavyo huwa napenda

Yasinta Ngonyani said...

nIMEKUMBUKA ...muhogo wa kuchoma nao uko juu....Pia tusisahu ugali wake:-)

John Mwaipopo said...

futari ya 'ze hogoz' hapo juu inanivutia. mapichi mengine yanayonitia raha ni 'ze hogoz' ya kuchoma na kachumbari yenye limao. utamu wake balaa!!

Rachel Siwa said...

Da'Yasinta ahsante sana uzalendo!

Duhhh mliokumbusha mihigo ya kuchoma yaani nimeimithi sana, ngoja siku nijaribu.

kweli kila mtu anapenda mihigo na vikorombwezo vyake, tena iwe imeiva na ungaunga kama alivyosema mchangiaji wa 1,

Tena sikuhizi hiyo mibichi inauzwa imekatwa vipande tayari kwa kutafunwa,
Eti mihogo Mibichi inasaidia majambothiiii? kaka Kitururu pole kwa udenda.

Asanteni wote kwa kuchangia na tuendelee na swali hilo la mihogo mibichi!!!!!!!!

Simon Kitururu said...

Katika MAJAMBOTHI kuna wadaio miogo mibichi ni viagra ila mie naamini ni kisaikolojia tu!

Si unajua ukiamini chochote ni dawa na ndio maana kikombe cha babu nacho nasikia kinatibu mpaka majambothi?

Rachel Siwa said...

Ahsante sana kaka kwajibu la mihogo na majambothi....

mumyhery said...

mwanangu muhogo wa nazi na ramadhani hii we acha tuu!!!

Anonymous said...

bampari kwa wale wa tanga school wanaijua hii lugha