Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 21 November 2017

Jikoni Leo;Kunde na Rachel-siwa..Wapendwa/waungwana natumaini hamjambo na mnaendelea vyema na majukumu yenu ya kila
siku,Pamoja na hayo siku haipiti na wala mambo hayatoenda sawa kama ukiwa na njaa..
ni "Jikoni Leo"mimi leo nimeandaa/pika KUNDE je wewe leo unapika/umepika nini?
Kunde hizi nimepewa zawadi kutoka Nyumbani Tanzania [Bongo]
Nimezichagua na nikaziacha/loweka kwenye maji usiku mzima,Asubuhi nikaziweka/bandika/tereka..... ok
jikoni kwa kuzichemsha mpaka zilivyoiva,nikakatia/weka Kitunguu maji na chumvu zikachemka kidogo
nikaongezea/unga nazi tuu sikuweka viuongo vingi...

Mimi hupenda kula na maandazi[zege kibongobongo/kiswazi] pia wali/ubwabwa...!
jee wewe unapenda kunde na je unapikaje? na unapenda kula na nini?
Karibuni sana...

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

No comments: