Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday 10 September 2012

KHADIJA MNOGA AKA KIMOBITEL AWABIP WAPENZI NA WASHABIKI WA EXTRA BONGO KWA WIMBO WAKE MPYA ALIOUPA JINA LA "MGENI" NDANI YA MEEDA.!!!


Kimobitel akiimba wimbo wake aliyeutunga mwenyewe unaojulikana kwa jina la "MGENI" ndani ya Meeda Sinza Usiku wa kuamkia leo.
Kulia ni Mkurugenzi wa Extra Bongo Ally Choki akiimba wimbo mpya wa Kimobitel ndani ya Meeda Sinza
Banza Stone AKA Generale akifurahi pamoja na Khadija Mnoga AKA Kimobitel wakati wa utambulisho usio rasmi wa ujio wa Kimobitel
Kushoto ni Athanas mwanamuziki anayekuja kwa kasi ndani ya Extra Bongo, akishoo luv na Kimobitel ndani ya Meeda Sinza.
Safu ya wanamuziki nguli wa Extra Bongo walioimba wimbo mpya wa Kimobitel (Mgeni) wakiongozwa na Ally Choki wa pili kutoka kushoto, wa kwanza kulia ni Rogert Hega Katapila, anafuatiwa na Banza Stone na Kushoto ni Kimobitel.

Kimobitel akiwa na nyuso ya furaha baada ya wapenzi na wadau mbali mbali kumpongeza na kumpokea kwa mikono miwili ujio wake.

Khadija Mnoga "Kimobitel" hivi majuzi alitangaza rasmi kuihama Bendi yake ya Twanga Pepeta ambayo aliitumikia kwa miezi kadhaa na kuhamia Extra Bongo, sababu za kuhama Kimobitel alisema ameamua kurudi Extra Bongo kwa sababu kuna mipango yake ambayo aliianzisha kwa hiyo amekuja kuimalizia kama wimbo ambao aliwahi kuimba wakati anaiimbia bendi hiyo unaotambulika kwa jina la "MJINI MIPANGO" kwa hiyo ameamua kurudi kuja kuikamilisha mipango hiyo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki amesema KIMO KIMO kama wengine wanavyomuita atatambulishwa rasmi siku ya Ijumaa ya tarehe 14/09/2012 katika ukumbi wao wa nyumbani New White House uliyopo Kimara Korogwe jijini Dar es salaam.

No comments: