Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday 9 November 2011

DR. REGINA KAPINGA AIPEPERUSHA VEMA BENDERA YA TANZANIA NDANI YA BILL AND MELINDA GATE FOUNDATION.



DR. Regina Kapinga

Mama Regina (Program Officer of Bill & Melinda Gate Foundation) ni Mtanzania wa kwanza kuchaguliwa kuwa Staff wa Bill and Melinda Gate Foundation.

kutokana na Elimu na uzoefu aliokuwa nao katika kufanya kazi kwenye Taasisi za kimataifa, Taasisi ya kimataifa inayomilikiwa na Tajiri mkubwa Duniani Bill Gate ambaye ni mmiliki wa kampuni kubwa ya technolojia ya Microsoft ikaona imtumie katika kuweza kusimamia shughuli zote zinazohusu misaada mbali mbali katika mabara maskini Duniani, yaani Afrika na Asia.

Watanzania tunakutakia afya njema ili uweze kuitangaza zaidi Nchi yetu, tunaamini kupitia wewe Taifa letu litafaidika na misaada mbali mbali kutoka kwenye Foundation hiyo.
        
Habari hii nimetumiwa na KapingaZ Blog
Asante sana.

Monday 7 November 2011

Da'Arianna Atimiza Miaka 3!!!!!!!

                     da'Arianna  kasimama tayari.
                           Kitu  cha kekiii.
              Mwenyekiti da'Mija akiandaa kekii.
                                 Arianna na mama'ke wakifurahia.
                          Mama Arianna akimsaidia kukata keki.
                              Kula mwanangu weee.
                                Dadazzzzz wakitabasamu.
               watoto wakibadilishana mawazo.
                  dada unajua mchezo huu?
                 Watoto wa Swahili Fellowship, wakisubiri kekii.
                  wametulia wenyewe.
                                    Watoto wanatabasamu naona mambo yalianza kusogea.
                       Watoto waliitikia mwaliko.
                        Mama kula eehhh,mama alikula mwishoni baada ya kuhakikisha watoto wote wamepata keki.

Familia ya bibi na bwana  Jonathan Mbwambo wa Coventry U.K.
Wanamshukuru sana Mungu kwa Mema mengi aliyo watendea, Moja  kati ya hayo ni kumlinda mtoto wao mpendwa da'Ariann mpaka leo Ametimiza miaka 3, Mungu ni Mwema sana.
Pia wanapenda kutoa Shukrani kwa Wazazi  na Watoto wa Coventry Christian Swahili Fellowship,na Wote waliojumuika nao.Shukrani za Pekee zimwendee Mwenyekiti wa Watoto da'Mija na Kamati Yake.
Mungu awabariki wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine.
Familia tunasema Asanteni sana kwa Moyo wenu na Mungu awe nanyi daima.


WENU KATIKA YOTE NA TUNAWAPENDA SANA.



         NASI SWAHILI NA WASWAHILI TUNAMTAKIA ARIANNA MAISHA MEMA YENYE AMANI NA FURAHA TELEEEEEEE.





Sunday 6 November 2011

ALFEO SILUNGWE AKIITANGAZA TANZANIA KATIKA MOJA YA PRESENTATION ZAKE INDIA.




Alfeo Silungwe Mtanzania anaye piga Nondo ya Masters of Statistic ndani ya Nchi ya India akiwa anafanya presentation katika moja ya kozi anayo isomea chuoni hapo.





                                                   Habari hii nimetumiwa na KapingaZ Blog.
                          Asante sana.
                                  


Trehe:5/11 NI SIKU ALIYOFARIKI BIBI TITI MOHAMED, MMOJA WA WANAWAKE WALIOKUWA WANAHARAKATI WA UKOMBOZI WA TAIFA LETU.


Bibi Titi Mohamed enzi za uhai wake.



Hapa akiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Bibi Titi Mohammed (1926 - 5 Novemba, 2000) alikuwa mmoja wa wanawake wa kwanza kushika nafasi za ubunge na uwaziri nchini Tanzania. Pia alikuwa kati ya wanawake wa kwanza kujiunga na harakati za kugombea uhuru wa Tanganyika.
Mwaka 1969 Bibi Titi Mohammed alikamatwa na mwaka uliofuata alifikishwa mahakamani kwa kosa la kula njama ya kutaka kupindua serikali. Katika kesi hiyo, Bibi Titi alikuwa ni mwanamke pekee katika washtakiwa 7. Baada ya kesi hiyo kusikilizwa alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha. Hata hivyo, mwaka 1972 alisamehewa na rais Julius Nyerere.

Juu ya kutolewa kwake, Mohammed aliongoza maisha yake akiwa mpweke. Mume wake alimtelekeza wakati wa kesi, ushirika wake wa kisiasa ukanyang'anywa, na marafiki zake wengi wakamlani.
Mnamo mwaka wa 1991, wakati Tanzania ikisherekea miaka 30 ya uhuru, Bibi Titi ameonekana kwenye makaratasi ya chama tawala kama "Shujaa wa Kike Aliyepigania Uhuru".
Mnamo tar. 5 Novemba, 2000 Mohammed amekufa kwenye hospitali ya Net Care Hospital mjini Johannesburg ambapo alikuwa akitibiwa.
Moja kati ya mabarabara makubwa ya mjini Dar es Salaam yamepewa jina la Mohammed kwa heshima ya mafaniko makubwa aliyoyafanya wakati wa mbio za kutafuta uhuru wa Mtanzania.


Habari hii nimetumiwa na Kabipingaz Blog
Asante sana.

Saturday 5 November 2011

Nawatakia Eid Njema Wapendwa!!!!!

                   Eid yenye FURAHA.
                        Eid yenye UPENDO.
    Eid yenye AMANI. da'Sabrina Kiwinga anatuwakilisha Swahili na Waswahili.

Muwe na Eid njema yenye Furaha,Upendo na Amani !kwa watu wote.
Tupate kusameheana na Tushirikianae vyema siku zote.




Nakumbuka nyumbani Eid kama hii, vyakula vilikuwa vinatembea tuu,vya Nyumba hii vinaliwa na Nyumba nyingine, Nyumba za Waislam kupelekea hata wasio waislam au kula nao pamoja.na Ikiwa Christmas nayo vivo hivyo,kulikuwa hakuna cha Udini wala nini wote Mnafurahi pamoja, kuoga na kuvaa nguo nzuri[za Sikukuu].
Sijui huu Upendo kama upo.Mungu atubariki na kutupa upendo wa Kweli.


EID NJEMA KWA WOTEEEE.






HATARI ILIYO MBELE KWA WAMACHINGA WANAOONGEZEKA KWA KASI KATIKA MATAA YA UBUNGO SERIKALI MNAIONA?

Trafiki Polisi akiongoza magari katika junction kubwa ya Ubungo, maarufu kama Ubungo Mataa.

Fuso ikiwa imeingia katika moja ya mtaro mkubwa ulioko bara bara ya Ubungo karibu na Ubungo mataa.

Kwa kipindi kirefu sasa eneo la Ubungo karibu na Mataa ya kuongozea magari yanayo ingia Jijini au yale yanayotoka pande mbili, mengine yakitokea Mwenge na mengine yakitoke Buguruni na kwenda sehemu mbali mbali za jiji limevamiwa na wafanya biashara ndogo ndogo maarufu kama Wamachinga.

Nimejaribu kulifuatilia kwa kipindi kirefu ili kuweza kujiridhisha kujua kama wamepewa ruhusa na nani kufanya biashara katika eneo lisilo rasmi, nilijaribu kuongea na wamachinga wachache; wa kwanza anaitwa Salum Ramadhan anauza taa za kichina katika eneo hilo, yeye alidai hawajaruhusiwa na mtu kufanya biashara hapo ila ni kutokana na ugumu wa maisha ndio umewapelekea kufanya biashara katika eneo hilo na wa pili naye Ndg. Deogratius Shirima akasema maneno hayo hayo ambayo hayapishani maana na huyu wa kwanza.

Sikuishia hapo nikataka kujua je kuna mtu yeyote ambaye anakuja kukusanya japo ushuru kutoka kwao? nao kwa pamoja wakasema kuna mtu huwa anakuja kukusanya ushuru lakini wao hawana uhakika kama ni kutoka Serikali za mitaa au la! nikawauliza swali jingine, huyu jamaa ambaye ameweka jenereta hapa na kuwapa huduma ya Umeme mnamlipa Sh. ngapi? wakasema kila taa 1 ni Sh. 1000/- nikapenda nijue sasa swali langu la msingi, wanajua HATARI iliyo mbele yao kutokana na kufanya biashara kando kando ya bara bara kubwa kama hii ambayo inapitisha magari mengi na hasa mengine yanakuwa yako kwenye mwendo wa kasi! wakasema wanaifahamu ila hawana jinsi wataenda wapi na maisha yenyewe ni magumu!
Kwa kweli nilitoka bila kuwa na jibu sahihi nini hatma yao kama gafla gari likitoka kwenye bara bara na kuwavama. 
Tatizo hili naamini serikali wanaliona ila wanalifumbia macho na pindi ajali itakapo tokea ndio wanafumbua macho na kujua sehemu sio halali, ni vema serikali ikalichukulia hatua mapema kabla halija tokea la kutokea. Tumekua tukiona sehemu mbali mbali ajali zinatokea na kuua watu wengi ambao wapo kando kando ya bara bara kwa hiyo ni vema Serikali ikachukua tahadhari mapema.

             Habari hii nimetumiwa na KapingaZ Blog.
Asante sana.

Tuesday 1 November 2011

Mimba Inavituko au Kujiendekeza????

Wapendwa!!Umeshawahi kukutana na Baadhi ya Wanawake wenye Mimba za Vituko?
Wengine hawapendi kuoga,Kuchana/kusuka Nywele, yaani hawajipendiiii,Wengine wanakula Sabuni,Udongo na Vingi visivyolika na Watu wa kawaida, Wengine Visirani,Jeuri,Matusi,Kususa[Kuzila],Kudeka na ....,Wengine hawalali/Kulala sana,Wavivu,Hawapendi watu hata WAUME ZAO!!.
Wengine wao wanapeta tuu/hawana tatizo, hawana tofauti za Mjamzito na akiwa kawaida, tofauti ni Tumbo tuu Limejazika/kuwa kubwa, wanajiremba /kuwa wasafiiii mpaka wanapo JIFUNGUA!!!


Jee Sababu ni Mimba au Kiejendekeza?
Wewe Mpendwa msomaji ulishapata Mimba ya hivyo au kuwa karibu na Mtu mwenye Mimba ya VITUKO?
Nasikia Wababa wengine wanakimbia nyumba zao kwa sababu ya Mimba za Vituko, au nao Wanatafuta Sababu ya kuondokea tuu? Sasa  wewe uliyempa Mimba unakimbia jee nani amkimbilie/kumsaidia?


KARIBUNI SANA WAUNGWANA KWA MAONI/USHAURI WENU!!!!!





Monday 31 October 2011

COVENTRY NA EID PARTY!!!!!!!!


EID PARTY EID PARTY EID PARTY COVENTRY, U.K.!!!
KARIBUNI SANA WASWAHILI WOTE KATIKA KUSHEHEREKEA EID!!
Party hii ni ya kina MAMA na  WATOTO tuu.


Tarehe  12.11. Itakuwa jumamosi,Itaanza saa 9:00 Mchana [3:00.pm],Mpaka saa 3:00 za Usiku[9:00.pm].

Mahali ni; Moat House Leisure and Neighbourhood Centre,
                  Winston  Avenue,Coventry,Cv2 1EA.

Tiketi zimesha anza kuuzwa!!Wahi Tiketi yako Mapema!!
Bei £5 kwa Mtu mmoja.Watoto chini ya mwaka mmoja wataingia Bure!!Chakula Bure!!Kinywaji 50p.
Pia kutakuwa na michezo  ya Watoto,kama Bouncy Castle na Mingine Mingiiii!!

Kwa Maelezo zaidi na manunuzi ya Tiketi
Wasiliana na;Bi ZAYANA Kwa namba 07889257308.

UKIPATA UJUMBE HUU WAJULISHE NA WENGINE.
KARIBUNI SANA!!!!!!.

Friday 28 October 2011

Mama mkwe Kuvunja Nyumba/Ndoa,ni Mapenzi kwa Mwanawe?Kwani ni Yeye Mama!!

 Wapendwa, hivi kwa nini MAMA MKWE/WAKWE;Hasa  Mama wa MUME.Mara nyingi wanapenda kuiingilia nyumba/Ndoa za watoto wao, Mpaka wengine kufanikiwa kuvunja/kuharibu Mahusiano/Ndoa hizo.Je wanataka mke wanaompenda wao/ kukuchaguli wao au Mapenzi tuu ya Mtoto wake tangu mdogo mpaka Akioa ndiyo yanamfanya aone/waone WIVU?Na JE nini kifanyike ili hali hiyo isitokee?.

Mimi Rachel nasema;Kina mama wakwe watarajiwa na mliokuwa na wakwe tayari,Jamani Taratibu waacheni watoto wajinafasi,Bali pale watakapotaka Ushauri au inapobidi.
Haya nawe Mpenzi Msomaji unalipi la kuongezea au Ushauri,Maoni gani kwa mama Wakwe wa Aina hii?

Karibuni sana Wababa,Wamama,Wanawake na Wanaume,mliokuwa ndani ya ndoa na mliokuwa bado!!!!!!!.

PATA NA BURUDANI YA IJUMAA HII KUTOKA KWA KAKA; MRISHO MPOTO!.

Thursday 27 October 2011

ANGALIZO KWA WATANZANIA WOTE, UTAPELI HUU UNAANZA KUOTA MIZIZI.






KUNA TAARIFA ZA WANIGERIA AMBAO WAMEWEKA MASKANI MAENEO YA SINZA, SHUGHULI AMBAZO WANAFANYA WANAIGERIA HAWA BADO HAZIELEWEKI, NI TATA.
MUDA MWINGI HASA VIPINDI VYA JIONI WANAPENDA KUSHINDA KATIKA BAA KADHAA AMBAZO ZINA AMBAA AMBAA NA BARA BARA YA SHEKILANGO, KUANZIA MAENEO YA URAFIKI MPAKA BAMAGA.

HIVI KARIBUNI WATUMIAJI WENGI WA SIMU ZA KIGANJANI NA INTERNET WAMEKUWA WAKITUMIWA MESEJI MBALI MBALI ZA KUSHINDA ZAWADI FLANI, MFANO WATUMIAJI WA SIMU ZA KIGANJANI WAMEKUWA WAKIPATA MSG AMBAYO INAWAONYESHA WAMESHINDA ZAWADI KUTOKA KAMPUNI YA NOKIA, WAKATI UNAKUTA ULIOTUMIWA MSG HIYO MUDA HUO UNATUMIA SIMU YA MCHINA AMBAYO HAINA HATA JINA, NA WALE WATUMIAJI WA INTERNET WANAPATA EMAIL ZA KUTAKA WAINGIZE DETAIL ZAO ZA AKAUNTI ZAO ZA BENKI, HIYO EMAIL INAKUONYESHA KAMA VILE ULICHEZA BAHATI NASIBU FLANI.

WATANZANIA WOTE KAENI CHONJO, KAPINGAZ Blog BADO INAWAFUATILIA HAWA JAMAA ILI KUWEZA KUJUA UNDANI WAO, NA VILE VILE TUNAVIOMBA VYOMBO VYA USALAMA NAVYO VIWEZE KUJUA HAWA JAMAA WANAFANYA NINI, HOFU YETU INAWEZEKANA WAO NDIO WANAJIHUSISHA NA UTAPELI HUU AMBAO NAAMINI WATANZANIA WENGI BADO HAWAJAUJUA VIZURI WIZI HUU WA KUTUMIA MITANDAO.
  
  Habari hii nimetumiwa na Kapingaz Blog

Asante sana.

Tuesday 25 October 2011

Watoto wa Kike na Mitindo!!!!!!

                                 da'Nadia na poziiiii.
                              da'Nadia na Tabasam...
                                     da'Ester kapoziiii....
                                   da'Ester yupo makini....
                                         da'Miriam na poziiii....
                                 da'Naomi  dadalao kwa mitindo sijui Jina.....

Waungwana mnasemaje? Watoto wetu wakipendeza nasi pia roho nyeupeeeee!!!
Mpendwa wewe unapendelea watoto wakitoka vipi/wakivaa vipi?
Nini wewe ulikuwa Unapenda kutinga/kuvaa ulipokuwa mdogo?

Wengi enzi za Utoto kulikuwa na nguo maalum, yaani ya Kanisani/Jumapili, Hospitali,Siku Kuu,Yakutokea kwenda kwa ndugu na jamaaa na yaKushindia/ukiwa nyumbani au kuchezea Rede kama si mpira wa Miguuu!!!!Hahahahhha Tumetokambali mwehhhh.

Lakini Watoto wa Leo wengi wao hakuna Masharti sana kila wakati Wamependeza tuu.

Karibuni Sana Tukumbushane ya Utoto na kutoa Maoni/Mawazo yako kwani Yanathamani kwetu!!!









Sunday 23 October 2011

Mwanamke na Kujiamini!!!!

Wanawake Tufunguke,Tujitoe,Tuamke,Tushikamane,Tupendane,Tuelimishane,Tujifunze na Tujiamini,
Hakuna kitu rahisi, Lakini ukiamua na kujituma utafanikiwa, Hatua moja huanzisha na nyingine,Tusisite kuulizana na kuomba Ushauri pale unapoona umekwama.Pale ulipo na unaweza kufanya kitu ili kusaidiana na kina baba pamoja na Familia,Jamii. Kila mmoja anamuhitaji mwenzie kwanamna moja au nyingine,Kama wewe unafanya kazi na kuna mwingine anafanya biashara.Unaweza kutamani Vitumbua na pengine unajua kupika lakini umechoka au hujui basi kuna mama yupo nyumbani yeye anapika na akakuuzia nayeakapata pesa kidogo nawe umepata mlo,Binadamu kila mmoja anajua hiki na mwingine anajua kile.WANAWAKE TUSILALE.

Nawatakia Jumapili Njema!!!.


Wednesday 19 October 2011

Nimekumbuka Kwetu,Nyumbani ni Nyumbani!!!!!!!!!!!!

                Nimewakumbuka Rafiki Zangu.
               Nimewakumbuka wa kaka wa Mitaa ya Kwetu.
                           Nimewakumbuka Ndugu zangu.
          Nimewakumbuka Vijana wa Mitaa ya Kwetu.
      Nimekumbuka hata Usafiri Wetu.
Nimekumbuka  Maembe,Mabungo na Matunda yote na Wauzaji wake.Hasa Magenge ya Karibu!!!!!

Wapendwa mimi Leo nimekumbuka Kwetu/Nyumbani, yaani ukiniuliza sana machozi yanaweza kunitoka.
Nanimekumbuka meeeeengiiiiii yakwetu.

Zamani ikiwa Likizo tunapelekwa kwa bibi mzaa mama[bi' Mwalimu], sasa ukiona naanza kuandika majina ya ndugu zangu,marafiki na wazazi wangu ujue kumekucha, nikimaliza kuandika bibi ajiandae kunirudisha.Na kila j'Mosi tunapelekwa kwa bibi mzaa baba[bi'MwanaPenza],yeye alikuwa mzee kidogo hawezi kutuhudumia, Hatukai sana huko, nae akiona narudi rudi ndani kunywa maji ajiandae na maswali baba alisema atakuja saangapi?akizugazuga tuu nitamuangushia kilioooo mpaka atuja kwanini tulienda.

Duuhhhh sasa huku nilipo sasa na Ukubwa huu sijui nifanye nini??
Nimeimba leo kuanzia Nyimbo za mchakamchaka,za mwalimu Kachale,Kibuzi,Ukuti na zote za utoto,
Nikahamia Youtube na Cd zote za Nyumbani, lakini nikaona Haitoshi ngoja nishiriki nanyi.

Jee Mpendwa nawe kunasiku yanakukuta haya na je unafanya nini ili kusahau?au unajifariji vipi?

Karibuni sana kwa mchango wa mawazo na Ushauri!!!!!!!!!


Tuesday 18 October 2011

AIBU GANI HII BADO INAENDELEA KULIKUMBA TAIFA LETU!!




Jeshi la Polisi nchini (PT) kupitia Inspekta Generali wake Said Mwema(Pichani) imetangaza dau la Shilingi Milioni 5 kwa mtu yeyote atakaefanikisha kupatikana kwa mtu aliyemjeruhi mtoto Adam Robert (14) ambaye ni Albino huko Geita ambapo mtu asiyejulikana alimvamia mtoto huyo na kuanza kumkata kata mikono na kisha kutoweka na vidole vya Albino huyo.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia mwishoni mwawiki katika Kijiji cha Nyaruguguna, Kata na Tarafa ya Nyang'hwale ambapo mlemavu huyo, Adam Robert (14), mwanafunzi wa darasa la nne, alivamiwa na kukatwa mkono wa kulia na kisha kunyofolewa vidole vitatu vya mkono wa kushoto.
Ni jambo la kusikitisha sana kuona vitendo hivi vinaendelea kutokea na mwisho wa siku jeshi linataka kutumia fedha za walipa kodi kwa ajili ya kuwapata wahalifu hao, mi nadhani hii njia sio sahihi, sidhani kama Jeshi la polisi wanashindwa kuwapata hawa wanaowatuma wahalifu kwenda kuwadhuru maalbino hawa. Jambo la msingi hapa sio kutangaza dau ni kuhakikisha wale wanaowatuma ndio wanakamatwa na ninaamini jeshi la polisi likishirikiana na usalama wa Taifa inawezekana kuwakamata hawa na kuwatokomeza kabisa, usalama wa Taifa wanafanya kazi gani kama sio pia na kuangalia usalama wa Watanzania hawa!
Ni aibu kubwa kwa Taifa letu vitendo hivi vinavyoendelea.
                                                            
                                                                          Habari hii nimetumiwa na KapingaZ Blog
                                                             Asante sana kaka Kapinga.

YUSTA MSOKA, MWANASHERIA ALIYEFANIKIWA KUTIMIZA MOJA YA NDOTO ZAKE.




Advocate Yusta Msoka

Yusta Msoka akiwa amesimama nyuma, mbele ya dirisha la pili upande wa kulia, akiwa katika picha ya pamoja na Wanasheria wenzake baada ya kula kiapo cha kuwa Advocate (Wakili)

KAPINGAZ Blog inapenda kumpongeza sana Dada Yusta kwa kufanikiwa kufika hapo alipofikia, vile vile inamshauri asiishie hapo aendelee zaidi mpaka aweze kufikia level ambayo ni ya kimataifa.

Kwa kutambua uhaba mkubwa wa Mawakili katika Taifa letu tunapenda kuwapongeza wale wote walioweza kufanikiwa kuwa Mawakili, tunawaomba wakafanye kazi zao kwa uadilifu na kuliletea sifa na mafanikio mazuri taifa letu, hasa hasa kuwa makini katika mikataba mikubwa ambayo taifa letu sasa linaangamia kutokana na mikataba hiyo.
                                                                             Habari hii nimetumiwa na Kapingaz Blog
                                                              Hongera da' Yusta.

SAKATA LA MGOMO WA WANACHUO WA IMTU UNIVERSITY HATMA YAKE LINI?




Geti kuu la kuingia Chuo kikuu cha Afya IMTU kilichopo Mbezi Beach.

Wanachuo hao hapa wakiwa katika moja ya maandamano ya mgomo huo.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr Shukuru Kawambwa

Sakata hili lilitolewa miezi michache iliyopita na vyombo mbali mbali vya habari kuhusu mgomo huu wa wanachuo hawa.

Ni jambo la kusikitisha sana kuona nchi ambayo ina upungufu mkubwa wa Madaktari, kushindwa kuumaliza mgomo wa Madaktari Wanafunzi ambao sasa umekamilisha miezi miwili, kundi hili la wanachuo limekuwa likikusanyika nje ya Makao Makuu ya Wizara ya Elimu kwa vipindi tofauti bila hitimisho la mgomo huu.

Kwa kutambua umuhimu wa wataalam hawa tunaziomba mamlaka zilizopewa dhamana ya kusimamia na kuongoza  ziumalize mzozo huu ambao madai yao ya msingi ni kulipa Ada kwa Tshs na si US Dollar na pia kulipa ada kubwa tofauti na vyuo vingine vya binafsi (private).

Sisi kama wanafunzi ambao tunaathirika na mgomo huu Bado tuna imani na Serikali ya Mh.Jakaya kikwete na watendaji wake wote, Katibu Mkuu Wizara ya elimu,Tanzania Commision of Universties na Higher Education Student Loan Board tunawaomba waumalize mzozo huu.
Pesa nyingi zimetumika za walipa kodi kupitia loan board kuwakopesha wanafunzi hawa Tunahitaji sasa wote kwa pamoja kulishughulikia hili tatizo ili tuweze kuendelea na Masomo na mwisho tuende kujenga taifa letu changa lenye upungufu mkubwa wa Madaktari.


Habari hii nimetumiwa na Kapingaz Blog.
Asante.

Thursday 13 October 2011

Mazishi ya Mpendwa Wetu; Baba Mzee Juma Penza, katika Picha

                       Marehemu Mzee Penza wakati wa Uhai wake.
     Kaka Mashaka akiweka Mchanga wa Mwisho.
       Kaka Mustapha akiweka Mchanga wa Mwisho.
               Kaka Iddy akiweka Mchanga wa Mwisho.
                   Rais Jakaya Kikwete akiweka Mchanga wa Mwisho.
               Mzee Janguo akiweka Mchangawa Mwisho.
             Meya wa Ilala Mstahiki Jerry Silaa, akiweka Mchanga wa Mwisho.
       Wajukuu nao hawakuwa nyuma kufanikisha Mazishi ya babu yao.


Shukrani kwa Wote Mliofanikisha Mazishi ya Mpendwa baba Yetu Mzee Juma Penza[JP].
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI;AMINA.


Rachel-siwa[Mwanapenza]na Timu Yote ya SwahilinaWaswahili;MAJONZINI.




picha kwa hisani ya Michuzi blog,Asante sana.