Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 19 October 2011

Nimekumbuka Kwetu,Nyumbani ni Nyumbani!!!!!!!!!!!!

                Nimewakumbuka Rafiki Zangu.
               Nimewakumbuka wa kaka wa Mitaa ya Kwetu.
                           Nimewakumbuka Ndugu zangu.
          Nimewakumbuka Vijana wa Mitaa ya Kwetu.
      Nimekumbuka hata Usafiri Wetu.
Nimekumbuka  Maembe,Mabungo na Matunda yote na Wauzaji wake.Hasa Magenge ya Karibu!!!!!

Wapendwa mimi Leo nimekumbuka Kwetu/Nyumbani, yaani ukiniuliza sana machozi yanaweza kunitoka.
Nanimekumbuka meeeeengiiiiii yakwetu.

Zamani ikiwa Likizo tunapelekwa kwa bibi mzaa mama[bi' Mwalimu], sasa ukiona naanza kuandika majina ya ndugu zangu,marafiki na wazazi wangu ujue kumekucha, nikimaliza kuandika bibi ajiandae kunirudisha.Na kila j'Mosi tunapelekwa kwa bibi mzaa baba[bi'MwanaPenza],yeye alikuwa mzee kidogo hawezi kutuhudumia, Hatukai sana huko, nae akiona narudi rudi ndani kunywa maji ajiandae na maswali baba alisema atakuja saangapi?akizugazuga tuu nitamuangushia kilioooo mpaka atuja kwanini tulienda.

Duuhhhh sasa huku nilipo sasa na Ukubwa huu sijui nifanye nini??
Nimeimba leo kuanzia Nyimbo za mchakamchaka,za mwalimu Kachale,Kibuzi,Ukuti na zote za utoto,
Nikahamia Youtube na Cd zote za Nyumbani, lakini nikaona Haitoshi ngoja nishiriki nanyi.

Jee Mpendwa nawe kunasiku yanakukuta haya na je unafanya nini ili kusahau?au unajifariji vipi?

Karibuni sana kwa mchango wa mawazo na Ushauri!!!!!!!!!


16 comments:

Anonymous said...

pole dada kwakukumbuka nyumbani ninaswali la kizushi hivi dada wewe unaishi nchi gani ni hayo tu

Maggie said...

Dadake yaani nimelia machozi ya furaha picha zime nikumbusha mbali jamani uwii umezitoa chimbo gani jamani asante sana dadake

Rachel Siwa said...

Anonymous:Asante,Nipo U.K.

Maggie; pole dadake siunanijua mimi kwa machimbo, poa basi tukutane Bonga, Club ya Wazee.Camp David au Amana? Tuanze safari mdogo wangu!!

sam mbogo said...

sasa da wewe uko uk, sasa sipanda tu katereni/garimoshi uje kwangu Bristol tulie pamoja,tuimbe pamoja!!.pole sana kukumbuka nyumbani ni muhimu kiaina, mimi kuna kitu huwa nakumbuka sana kiko huko nyumbani ila nisiri yangu.........? ndiyo maana kila mwaka lazima nitunge wimbo wakuondokea si unajuwa tena baba!? amasivyo inakuwa ngumu.kaka s

Yasinta Ngonyani said...

Rachel! kukumbuka nyumbani ni lazima hata kama ungekuwa unaishi Kigoma na umezaliwa Arusha UNGEKUMBUKA NYUMBANI tu...mwenzio huwa nacheza lizombe nachukua albamu naangalia na pia huwa naimba nyimbo na halafu labda napika vyakula vya nyumbani kama ninavyo kama sina basi. Sasa umenifanya na mimi nianze kulia...Kunyumba nga kunyumba mlongo wangu...

EDNA said...

Mimi nimeyakumbuka hayo maembe,yaani hapa udenda unanitoka.

Rachel Siwa said...

Ahsante kaka Sam,ipo siku nitakuja kaka yangu, hhaahhaha kaka hako kakitu unkofata kila mwaka huko bongo siri yakoMmmmmhhhhh wifi anakajua?

Ohhh dada wa mimi Yasinta Pole, sasa tukilia wote nani atamnyamazisha mwenzie?ahsante kwa Ushauri wako dada basi nyamaza mtu wangu.

Da'Edna pole kwa udendaaaaa!

Yasinta Ngonyani said...

Rachel! sijui kwa nini wakati mwingine nakuwa kipofu LOL kweli kaka S Wifi anajua ako kasiri?...na halafu Rachel Labda tusilie sana kwani...hapo jaza wewe. kaaaaaaaziiii kwelikweli

emuthree said...

lAKINI hujanikumbuka mimi ndugu yako, tupo tupo ....tupo pamoja ndugu yangu

Yasinta Ngonyani said...

Ila emu-3 amenena Rachel. Sisi wengine sio ndugu zako..LOL

Rachel Siwa said...

Ohhhh nikweli ninyi ni ndugu zangu haswaaaa lakini huyo amewawakilisha, tena nyie kila leo mkiona mlango hapa haujafunguliwa mtagonga mpaka mjue kulikoni, mimi nawajali sana na kuwapendaaaa, ninao kina kaka, kina dada, wadogo na ...........pia sijutii kamwe kujuana nanyi kwani mnanifariji vya kutosha,nikiwa na kijiUtata kidogo tuu, nikiandika hapa napata jibu, nacheka, na nafarijikaaaaaa nawapenda Wooooooooooteee na Mungu atuwezeshe siku tukutane sijui wapi, labda kwa HARUSI YA KAKA KITURURU!!!!!! AU NYUMBANI KWANI IPO SIKU MUNGU AWEZA KUTUKUTANISHA@@@!!nI MIMI NDUGUYENU MPENDWA RACHEL.

chib said...

Mimi na basi tu! Tuliyakuwa tunayaita mabasi mkate LOL!

Mija Shija Sayi said...

Mimi nimekumbuka sana Nganza sekondari, ni juzi tu nilikuwa namsimulia mwanangu jinsi fimbo zilivyokuwa zikitembea kama ukiingiza chakula bwenini, usipokimbia mchakamchaka saa kumi na moja alfajiri na jinsi tulivyokuwa tukinywa uji bila sukari...

Aisee siku zile zilikuwa ni raha sana..

Vipi Rachel umesoma boarding?

Rachel Siwa said...

Walikuwa wanataka wote mle mlo mmoja, Boarding ilinishinda dadake.Lakini ni maisha mazuri sana nayakujifunza mengi.

Mija Shija Sayi said...

Yaani ungangali wote huo Rachel Boarding ilikushinda??... nakwambia haya maneno asiyasikie kakako Kitururu..

Rachel Siwa said...

hahahhhahha dadake yaani ficha hivyohivyo asiyasikie, maana mimi nilimwambia mnyela Mmbwa wa moro walimtoa nishai.