Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Watoto na Mitindo. Show all posts
Showing posts with label Watoto na Mitindo. Show all posts

Friday 13 June 2014

Watoto Na Mitindo,Michezo;Summer Collection;[Maandalizi Ya Familly Fun Day]!!!!!!






Hamjambo Wazazi/Walezi na Watoto wangu Wapendwa?  Summer Time....Wakati wa Jua umewadia,Hiki ni kipindi kizuri sana hapa Ng'ambo kwa Michezo ya Nje,Unaweza kuvaa vizuri na si nguo nyiingi yaani makoti,Masweta na.......Pia kunakuwa na Likizo[Summer Holiday].

Maandalizi Ya  "Family Fun Day" zaidi itakuwa Michezo;Kuchora,Kuimba,Kucheza,Mitindo,Kuangalia Vipaji vya Watoto wetu,Nyama Choma na VyaKula vingine,  Kufurahi Pamoja... na Watoto.

Wengi huwa wanakwenda Likizo Afrika na sehemu nyingine kwa wale watakao kuwepo kwa mwaka huu tutafanya tukutane na kucheza pamoja.
Itakuwa baada ya mfungo wa Ramadhani ili  wote tufurahi pamoja.
  Tarehe 02/08 panapo Majaaliwa.


Kama kuna Ushauri,Msaada katika kuandaa na Mengine yote,Usisite kuwasiliana nami.
Email;rasca@hotmail.co.uk.
Simu;0750 44 100 40.


Wote Mnakaribishwa katika Yote.

kuhusu mambo ya Watoto zaidi;http://watotonajamii.blogspot.co.uk/

Swali;Kwanini watoto wetu ni waoga?

Kwanini Hawajiamini?
Kwanini wana Aibu?

Wednesday 30 January 2013

Watoto Na Mitindo;Pata na Video Hairstyle Slideshow!!!!


Aliye msuka huyu  ndiyo aliyekuwa akiwasuka watoto wangu..Nimefurahi kusikia bado yupo na anaendelea vyema na kazi zake kwa watoto...tena anawezana nao haswa...

Waungwana; Mimi naamini watoto wana Mitindo yao..pia wakipendeza wao wenyewe na wazazi tunakuwa na furaha sana..

Si Lazima au si wote wanapenda  watoto wasukwe..basi hata kama ana Nywele fupi..kuna Vibanio vyao pia wanapendeza sana......

Nao Watoto  kuna Umri wewe mzazi utamchagulia Mitindo ya Nywele lakini kuna Umri mwingine Mmmhh !!...inakuwa kazi ya ziada, Yeye/Wao hutaka hivi nawe unataka hivi..basi ni mabishano tuu..kama wapo wawili huwa wanaangaliana wao na kucheka au kuguna....hahahhaahhah imeshakukuta hii?

Karibuni sana kwa Maoni/Ushauri na Kuelimishana kwa Upendo.....

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.





Thursday 5 April 2012

Watoto na Mitindo,Kutoboa/Kutoga Masikio!!!!

Haya Waungwana;Wazazi/Walezi Unaonaje watoto kutoboa/kutoga masikio wakiwa Wadogo?jee Tunawafurahisha au Tunajifurahisha?ni vyema atoboe/kutoga yeye mwenyewe akikua au bora tuwafanyie labda wakikua watatulaum?
Karibuni Sana kwa Maoni na Ushauri.Pamoja!!!!!!

Monday 12 December 2011

Watoto wa Kiume na Mitindo!!!!!!

                                        Kaka Mohamed kapozi
                                  hapa na Tabasam
                                              hapa katulia.
Wapendwa Watoto wa kiume na Mitindo yao!!Nakumbuka zamani kulikuwa na Kaunda Suti,Ngwabi,Mchelemchele,Jinzi za Chatu/kujikunjakunja hivi,Mashati ya drafti na nyingine nyingiii,pia watoto wengi walikuwa wanashonewa hizo Suti kwa Fundi tena SareSare,Viatu Moro shoes,Vimokasini,Raba Mtoni, Ndopa/Lakupanda.Pia kulikuwa na viatu vya Bora sijui kama bado lipo hili duka.Pia naona kama mitindo inajirudia .

Wewe unakumbuka nini/kuvutiwa na nini vya wakati ule na Wakati wa sasa jee?

Karibuni sana Waungwana!!!!!

Tuesday 25 October 2011

Watoto wa Kike na Mitindo!!!!!!

                                 da'Nadia na poziiiii.
                              da'Nadia na Tabasam...
                                     da'Ester kapoziiii....
                                   da'Ester yupo makini....
                                         da'Miriam na poziiii....
                                 da'Naomi  dadalao kwa mitindo sijui Jina.....

Waungwana mnasemaje? Watoto wetu wakipendeza nasi pia roho nyeupeeeee!!!
Mpendwa wewe unapendelea watoto wakitoka vipi/wakivaa vipi?
Nini wewe ulikuwa Unapenda kutinga/kuvaa ulipokuwa mdogo?

Wengi enzi za Utoto kulikuwa na nguo maalum, yaani ya Kanisani/Jumapili, Hospitali,Siku Kuu,Yakutokea kwenda kwa ndugu na jamaaa na yaKushindia/ukiwa nyumbani au kuchezea Rede kama si mpira wa Miguuu!!!!Hahahahhha Tumetokambali mwehhhh.

Lakini Watoto wa Leo wengi wao hakuna Masharti sana kila wakati Wamependeza tuu.

Karibuni Sana Tukumbushane ya Utoto na kutoa Maoni/Mawazo yako kwani Yanathamani kwetu!!!