Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday 12 December 2011

Watoto wa Kiume na Mitindo!!!!!!

                                        Kaka Mohamed kapozi
                                  hapa na Tabasam
                                              hapa katulia.
Wapendwa Watoto wa kiume na Mitindo yao!!Nakumbuka zamani kulikuwa na Kaunda Suti,Ngwabi,Mchelemchele,Jinzi za Chatu/kujikunjakunja hivi,Mashati ya drafti na nyingine nyingiii,pia watoto wengi walikuwa wanashonewa hizo Suti kwa Fundi tena SareSare,Viatu Moro shoes,Vimokasini,Raba Mtoni, Ndopa/Lakupanda.Pia kulikuwa na viatu vya Bora sijui kama bado lipo hili duka.Pia naona kama mitindo inajirudia .

Wewe unakumbuka nini/kuvutiwa na nini vya wakati ule na Wakati wa sasa jee?

Karibuni sana Waungwana!!!!!

Friday 9 December 2011

Kheri ya Miaka 50 yaUhuru,Na Siku kama ya Leo da'Halima Kiwinga Alizaliwa!!!

Nawatakia Kheri ya  Miaka 50 ya Uhuru!Pia Siku kama ya Leo Familia ya M.S.Kiwinga wa Ilala,Sharifu/Shamba,  Ilipata Mtoto wa kike na Wakamwita HALIMA!!!Leo ametimiza miaka 50!!!!!Hongera sana dada yetu mpendwa,Mungu akubariki sana katika yote,Sisi wadogo zako Tunakupenda,kukujali,kukuthamini na Tunajidai kuwa na dada kama wewe .Da'HALIMA Uwe na Wakati mzuri  Leo na siku zote za Maisha yako.MUNGU NI PENDO.Kwaniaba ya Familia ya Marehemu Mzee Kiwinga ni mimi Rachel-Siwa.

SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU JIJINI DAR PART - 2

SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU JIJINI DAR LEO PART-1

Thursday 8 December 2011

Chaguo la Mswahili Leo ;Les Wanyika : Paulina!!!!

Siku kama ya leo kaka Henry Mwana wa Kapinga Alizaliwa!!!!!!



MPIGANAJI SASA ATIMIZA MIAKA KADHAA!!!

Mpiganaji wenu Henry Kapinga wa Blog yenu ya KAPINGAZ Blog leo Tarehe 8/12 ndio siku aliyozaliwa.
Nawashukuru wale wote walionipa Hongera kwa kuukaribia uzee, sasa sijui kama ni wote mnaupenda uzee, manake fainali yake ni shughuli.
ASANTENI SANA!
Nasi Swahili na Waswahili tunakutakia kila lililojema katika maisha yako.

Monday 5 December 2011

Comment ya kaka Manyanya kwenye post ya Peter Kapinga!!!!!!

Delete
Blogger Goodman Manyanya Phiri said...
Asante Rachel Mdogo wangu kwa habari hizo.

Kwa wengine wasiejuwa jeshi, taarifa yangu ni kwamba wastani wapo aina tatu wa askari popote pale duniani.


1. WAPIGANAJI (THE MEN/TROOPS---"seamen" kama ni wa baharini, "airmen", wenye kutumia ndege). Ngazi ya chini kuliko zote. Hao ndio waliezagaa katika mambo ya filamu pale panomwagika damu. Kama anajina lake kama "fulani", Wazungu watamtambua kama "PRIVATE FULANI". Nchi nyingi watamchukua kijana yoyote yule mwenye nia kupata mafunzo katika ngazi hii.


2. WARRANT OFFICERS (au "sergeant majors"). Shughuli zao hao ni kuchunga nidhamu ya jeshi. Wapiganaji (MEN/TROOPS) hua wanawaogopa sana hawa warrant officers na ukiwa mwanajeshi na umemridhisha WARRANT OFFICER wako basi wewe unayo nidhamu ya hali ya juu. Hua wanapewa mamlaka wao na Waziri wa ulinzi katika mataifa mengi duniani, na kibali wanachopewa na Waziri kinaitwa "A WARRANT" na ndio maana wanaitwa WARRANT OFFICERS. (Kufika wa WARRANT OFFICER utakuwa wastani umepitia uKoporali, Sajenti, Staff Sajenti na kadhalika na unahitaji sana elimu kabla ya kuchaguliwa!)


3. MAAFISA WA KAMISHENI, COMMISSIONED OFFICERS (kama mhusika hapa) nao wanapewa wadhifa na Raisi wa nchi pekee! Kazi zao za msingi jeshini sio kupigana lakini NIKUIMARISHA JESHI KIMAWAZO NA KUTOA MBINU ZA KUPIGANA KWA MAFANIKIO. WANATAKIWA WAWE MFANO WA KUIGWA NA JESHI LOTE PIA NA WANANCHI WOTE! (Kwa kuwa unahitaji elimu ya juu kuwa afisa wa aina hii, nchi nyingi hutachaguliwa kama hujamaliza angalau kidato cha mwisho/Fomu 6 ya Tanzania. Baadhi ya ngazi za kupitia hapo ni CANDIDATE OFFICER, LUTENI, KAPTENI, MEJA, LUTENI KANALI, KANALI, BRIGADIER NA KADHALIKA KATIKA NYADHIFA SASA ZA UJENERALI au "u-admirali" ukiwa jeshini la maji au baharini)



Sasa tuje kwa Bw. Kapinga:


Huyu bwana usimuonee wivu KWANI ANAKAZI KWELI SASA.

Mifano:

1. Popote asipokuwepo Raisi, YEYE ANACHUKUA MAJUKUMU YA RAISI IKISTAHILI. Kwa mfano: mwiko kuumia kwa mwananchi ikiwa afisa yupo karibu na angemuokoa lakini eti afisa hakujisumbua hata kidogo!


2. Awe amevaa sare ya kijeshi au hakuvaa anatakiwa awe muungwana (GENTLEMAN) kuliko Mtanzania yoyote yule mwingine nchini !

(Hii inamaana akiwa D'salaam huyu bwana daima atakuwa amesimama kwa miguu katika usafiri wa daladala kwani si uungwana kuketi wakati mwanamama amesimama!)


3. Asije akaonekana amelewa pombe hata akiwa nyumbani kwake na ANAWEZA KUTIWA MBARONI kwani hastahili AFISA kuwa mlevi! Pia hamna ugomvi au makelele alipokuwepo yeye!


4. Hata katika mifarakano au hatari ya aina gani ya umma yeye asionekane muoga wa kijingajinga , wala asikimbie na kama anataka kujiepusha na hatari hiyo ASIJE AKAONEKANA ANAKIMBIA....huenda anaweza akatia pupa (PANIC) kwa wengine!

5. Yeye ndie wa mwisho kula jeshini na kama chakula ni kidogo watakula wanajeshi wote (TROOPS AND WARRANT OFFICERS) YEYE NDIE MWENYE KUKAA KWA NJAA!

...YOTE HAYA KUTOKANA NA KWAMBA YEYE NI AFISA , AJITOE MHANGA DAIMA!!!!! Na ukitaka kuona mfano mzuri wa afisa tena wa kuigwa: ni Kanali Gaddafi wa huko Libya yeye aliekataa katakata kukimbia mpaka kufa!




Luteni Peter Kapinga, mimi kama luteni kanali wa jeshi la hapa Afrika nakukaribisha sana katika wadhifa wa uafisa. Ninayo ndoto moja tu kwamba kabla sijaenda kaburini jeshi laTanzania, Msumbiji, Malawi, Uganda, Congo, Angola, Namibia, Swaziland, Botswana, Afrika Kusini, Lesotho na nchi zingine LITAKUWA JESHI MOJA TU LA NCHI MOJA LABDA NAWE UTAKUWA JEMEDALI AU FIELD MARSHAL WAKE!

Kazi ipo, Ndugu yangu; lakini siri kukupa mimi ziko mbili

1. Chunga afya yako
2. Chunga dhamira yako)
4 December 2011 14:57

Sunday 4 December 2011

Nawatakia j'pili Njema!!Pata kibao hiki-wakati wakuomba!!!

PETER KAPINGA SIKU ALIPOTUNUKIWA KAMISHENI NA RAIS DR JAKAYA KIKWETE.


Luteni Peter Kapinga

Tarehe 26/11/2011 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kama Amiri Jeshi Mkuu aliwatunuku Kamisheni wanachuo wa Chuo cha kijeshi cha Monduli Mkoani Arusha.

Peter akiwa mmoja wa wahitimu hao anapenda kuwashukuru wote ambao walioshiriki katika kumsaidia kwa namna moja na nyingine mpaka amefikia hapo alipofikia, zaidi anapenda kumshukuru Dada ake Esther Mbapila pamoja na Mr Mbapila kwa kushiriki katika mchakato wote mpaka akafanikisha kupata alichokihitaji.
ASANTENI
Nasi Swahili na Waswahili tunakutakia kila lililojema katika Yote.

Friday 2 December 2011

OMARY MJENGA NA SHEREHE YA MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI NCHINI SIERA LEONE.



Mwakilishi Mkazi wa UNOPS nchini Sierra Leone Bw Omary Mjenga akiwa na Mwakilishi Mkazi wa UNAIDS Bi. Mulunesh, raia wa Ethiopia, kwenye sherehe hizo, ambazo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Sierra Leone Mh Ernest Koroma. Bi Mulunesh aliwahi kuwa Mwakilishi Mkazi wa UNAIDS nchini Tanzania mwaka 1996 hadi 2000.


Thursday 1 December 2011

Jikoni Leo ni Dagaa!!pata na Burudani; Usiniseme-Ali kiba!!!!!!!

           Kitu Dagaa kipo Jikoni
Mimi Napenda zaidi na Ugali,Dagaa kila mtu anaupikaji wake, Mimi wa Chukuchuku,Mafuta Poa tuu,Lakini wa kuungwa/kuwekwa Nazi au Mawese wamenishinda!!Je wewe Mpendwa unapenda Dagaa? Unapikaje na Unapenda Kula na nini na kushushia na kinywaji gani?Karibuni sana Waungwana!!!USINISEME KAMA NAPENDA KULA!!!

Monday 28 November 2011

Wanawake na Urembo!!!!!!!!

                        Huyu kapaka sijui manjano.......
                        Huyu kawa wa pinki
                        Huyu na manyonyo
                                               Huyu kakaba shingo
                                                Huyu kachora .
Haya Wapendwa Wanawake na Urembo,kila siku yanazuka mapya,Pia ya Zamani yanarudi kama si kukumbukwa.Nao zamani kulikuwa na yao mengi tuu,Zazuu,Kuchoma nywele,Kusukia Rafya[sijui kama nimepatia]na Mengine Meeeeeeengi.

Wasasa kuna wanaopenda Maziwa makubwa mpaka kuyaongeza,Kujichubua/Mkorogo,Kujichora kwa sasa si hina tuu kuna Tattoo tena mpaka kwenye Nyusi, Wananyoa na kuweka tattoo ili wasipate shida ya kupaka Wanja.Kuna wanaoongeza Kope,Kunakuweka Vidubwasha ndani ya macho  na kubadili Lenzi kuwa kama ya Wadhungu. Na Mengine meeengi labda sikuweza kuyaandika au Siyajui Yote hayo kwa SABABU YA UREMBO!
Haya sasa  Mwanamke wewe;Katika hayo yote wewe unapenda nini ili uwe Mrembo au unaweza kuongezea ambayo hayapo hapo nasi Tufunguke,Pia unachukia kipi?

Wewe Mwanaume jee unapenda Mkeo,Mchumba,Rafiki yako wa Kike atoke vipi katika hayo na Unaweza kutujuza ambayo hayapo ili awe Mrembo na Unachukia kipi?

Duuhh Lakini Urembo mwingine unataka Moyo!!
Karibuni sana Wapendwa  kwa Mawazo/Maoni,Ushauri na Kuelimishana kwa Upendo!!!!!




Friday 25 November 2011

CITE- NA MIAKA 50 ya UHURU WA TANZANIA!!!!

Watanzania waishio Uingereza Kufanya Maombi ya Kumshukuru Mungu Kwa MIAKA 50 ya UHURU.

Waandaaji wa maombi ya ya Miaka 50 ya Uhuru chini Uingereza ”Association of Tanzanian Christians in Europe(CITE)” Wakiwa na Mwl Christopher Mwakasege wakati wa Summer Confference 2009.
Mithali 14:34 Biblia inasema Haki ya Mungu huinua Taifa na huu ndio mstari wa kusimamia katika Maombi hayo yanayowajumuisha watanzania wote waishio nchini Uingereza Hususani katika jiji la London. Kwa Mujibu Wa Mchungaji Emmanuel Chatawe ambaye ni mmoja wa waratibu wa Maombi hayo maombi hayo yatahudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali.

Pamoja na Maombi hayo pia kutakuwepo na vikundi mbalimbali vya kusifu na kuabudu.Maombi hayo yameandaliwa na Umoja wa wakristo watanzania waishio bara la Ulaya(CITE).

TAREHE:10 Dec 2011

VENUE: Vision Gospel Ministry International 68 Wallis ROAD Hackney Wick London E9 5LH

TIME :13:00 – 18:00 HRS



Wakati Watumishi wa Mungu Kutoka  Tanzania  waishio nchini Uingereza wakijipanga kwa Maombi hayo, Kwa Upande wa Wakristo wa Watanzania Waishio Nchini Marekani wao wanatarajia kufanya Maombi hayo Tarehe 10 Dec 2011 .Kwa Maelezo zaidi juu ya Kusanyiko la Maombi ya Uhuru wa miaka 50 nchini Marekani Fuata LINK hapa chini.


http://hosannainc.blogspot.com/search/label/Watanzania%20Wahudumuo%20Nje


Thursday 24 November 2011

Miaka 50 ya Uhuru - Kijitonyama Evangelical Choir!!!!!

Wanakwambia Tujibweteke aaa,Turudi Nyuma mmm,Tusonge Mbele namnamnam,
Haya wapendwa mmejiaandaje na miaka 50 ya Uhuru? Mablogger nao sijui watatoka vipi/wameandaa nini?
kwani  nimeona Vyama, Vikundi vya ngoma,Muziki,Kwaya na mengine mengi kuhusu Miaka 50 ya UHURU. Uwe Huru na mwenye Amani na kila lililo jema!!!Usisite kutujuza Nasi Umejiaandaje au Unalipi kuhusu MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA. NA VISIWANI TUUNGANE PAMOJA!!

Tuesday 22 November 2011

Siku kama ya Leo dada Akhram wa Billy Alizaliwa!!!!

Siku kama ya leo Familia ya Bibi na Bwana Billy, Walipata mtoto wa kike na wakamwita Akhram!!
dada huyu ni mtu wakucheka wakati wote mpole na mwenye heshima,Si muoengeaji sana mpaka akuzoee sana,Nakuongea kwake uwe na muda ili mmalize hayo maongezi kwani ni taratibu mnoo,Ukiona kafunga mdomo bila tabasamu ujue NJAAA Kwenye sekta ya msosi ahaaa hana Tabu kabisa!!!Usikivu,samahani na kufanya vyema darasani kwake ni maisha  ya kawaida.
Mungu awabari wazazi na awape hekima katika Malezi yenu.


Swahili na Waswahili tunakutakia kila lililo jema mwanakwetu!!!!

Thursday 17 November 2011

SHUKRANI KUTOKA KWA FAMILIA YA JUMA PENZA[JP]!!!


Marehemu JUMA PENZA enzi za uhai wake.
Familia ya Juma Penza ya Gongo la Mboto Dar es Salaam inapenda kutoa shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki walioshirikiana  nasi katika kufanikisha shughuli za msiba wa baba yetu mpendwa, aliyefariki dunia tarehe 12/10/2011 katika hospitali ya Hindu Mandal na kuzikwa tarehe 13/11/2011 katika makaburi ya Kisutu. 



Tunatoa shukrani za pekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. J.M. Kikwete, CCM Makao Makuu, ndugu, jamaa, majirani na marafiki kwa misaada yenu ya hali na mali na kwa namna mlivyoshiriki katika shughuli zote za mazishi.  Shukrani za pekee ziwaendee Dr. Macha Ocean Road, wauguzi na madaktari  wa Hindu Mandal.


Kwa kuwa ni vigumu kumshukuru  kila mtu kipekee, tunaomba shukrani hizi  mzipokee  wote kwa mikono miwili  kutokana na jinsi mlivyohusika kwa njia moja ama nyingine katika kufanikisha  shughuli nzima ya msiba wa baba yetu mpendwa Mzee JP.


Tunawashukuru kwa jinsi mlivyokuwa karibu  nasi  kwa dua  na maombi wakati wote  hadi tulipompumzisha baba yetu kipenzi .


Vilevile  tunapenda  kuwakaribisha  katika  mkesha  wa dua  itakayofanyika  Ijumaa usiku  Novemba 18 kuamkia siku ya Jumamosi Novemba 19 ambapo khitma  itasomwa  nyumbani kwa marehemu  Gongo la Mboto Dar es es Salaam wote mnakaribishwa .


Tunawakaribisha wote kwenye Arobaini ya marehemu. Mkesha na kisomo utafanyika siku ya Ijumaa tarehe 18/11/2011 na kufuatiwa na  Khitma itakayosomwa Jumamosi tarehe 19/11/2011 kuanzia saa 5:00 asubuhi nyumbani kwa marehemu Gongo la Mboto Jijini Dar es Salaam.Inna lilah Wainna Ilaih Rajiun

Wednesday 16 November 2011

Kuna Siku za Furaha na Siku za Vilio,Yote ni MaishaTusikate Tamaa!!!

                 Siku Ndugu zangu walipokuwa na Furaha.
                                        Mshumaa ulio Zimika.
                                            Mshumaa ulioZimika

Mungu awatie Nguvu katika wakati huu Mgumu na Sikuzote,Zaidi tudumishe Upendo,Umoja,Ushirikiano na Tusikate Tamaa,Wakati kama huu ndiyo utamjua Rafiki,Ndugu wa Kweli na Mengi Mema kwa Mabaya unaweza kuyasikia.Na niwakati kwa Waliopoteza Wazazi/Wapendwa wao Kuwakumbuka na Kulia tena,Nimeamini wanaosema Kilio hakiishi Utalia kila unapokumbuka.Nilitamani niwe nanyi lakini Mungu aliye nanyi ni Zaidi yetu sisi Tuliyo mbali.Mungu awalaze Mahali Pema Peponi Nduguzangu na Rafiki zangu,Jirani zangu na Wote waliotangulia.Sina Mengi ya Kusema bali nasema Asante Mungu.Wenu MWANAPENZA.

Monday 14 November 2011

Wanawake Waswahili wa Coventry wanakutakia,Kila la kheri da'May!!!!!!!!

                                        Mwenyewe da'May.
                                           Kekiiiii
                                               Kata mwanangu kataaa Keki
             May akilishwa na dada yake Esther,dada huyu ndiyo chanzo cha shughuli hii
                       May akimlisha dada yake kwa Furaha
             Da'May baada ya kumlisha dada yake wakaangaliana,May akasema Asante dada yangu
                   May na Mswahili wa Congo
                Mama mwenye nyumbaaa alilishwa pia
                    dada akisogea kutoa Nasaha zake mambo ya Tanga hayo
                           Heheheheee da'Stellah Akitoa Nasaha zake
                   Weshuuu!! da'Tina akitoa Nasaha zake
                           Wamama wakifuatilia Nasaha mbalimbali
                        Waswahili kutoka Milton nao walikuwepo
                          Da'Edna alikuwa MC siku hiyo, Yupo sambamba na mwali
                           Da'Asha mwenye furaha akifuatilia mapango mzima wa Nasaha
                              Wamama hawa wameguswa na Nasaha
                          Da'Bai yupo makini na kamera yake,lakini sikio lipowazi Kusikiliza Nasaha
                     Da'Sarah,Mamie na Stellah,Shughuli ilikamalika
                                 Da'Tinna alikuwepo
                        Dadazzzz walikuwepo,Neema,Maggie na Vick
                           Penye Wanawake Waswahili hakukosi Mila babuu Mtu kwako yakheeee
                         Haya funga Vibwebwe jamaniiiii!!!!Twende sasa!!
                                Hahhahahha Mwali kakuaaaaaaaaaaa,Swahili na Waswahili Wapendwaaaa


                         Nyanyuka sasa Mdogo wangu ya Coventry yameisha Subiri ya Dar na  Tangaaa

                    Mpango mzima wa muziki na Ngoma ulisababishwa na da'Chikuuuu huyo wa Mwisho


Shughuli hii ndogo ya Kumtakia Ndoa Njema dada May,Iliandaliwa na da'Esther,yeye ni dada wa bi Arusi mtarajiwa, Wanawake Waswahili wa Coventry U.K,[WWCU]Walikuwa bega kwa bega na da'Esther kufanikisha jambo hili.
Wanawake Coventry mpo juu na Mungu awabariki sana!!!


Dada May anatarajia kufunga Ndoa hivi karibuni,Ndoa hiyo itakuwa Nyumbani Tanzania[Bongo].
Kwaniaba ya Wanawake wenzangu;Da'May Tunakutakia Safari njema,Ndoa njema yenye baraka na Mungu akutangulie kwa kila jambo wewe na Mume wako Mtarajiwa pamoja na Familia na Wote watakaofanikisha.
Mengi yalishasemwa  pale kwenye sherehe,Hatuna la zaidi sisi TUNAKUPENDA SANA!!!!!!!