Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Saturday 12 March 2011

Wanaume Wanaopigwa na Wake zao!!!!!!!!!!!

Hivi  kuna Wanaume  wanaopigwa  na  kunyanyaswa  na  Wake zao? Je nao wanakitengo cha kuwasaidia kama vile Tamwa na kwingine? Kwanini  kelele nyingi/mashitaka mengi  niyasikiayo  ni ya Wanawake,Au Wanaume ni wavumilivu,wanaona aibu,wanajikaza kiume au wao hawaumizwi na wakiumizwa wanayamaliza wenyewe? Karibu tuelimishane wapendwa!!!!!!!!.

Tuesday 8 March 2011

Siku ya Wanawake!!! Mshindi wa Shindano la Wanawake wenye HIV!!!!!!!!!

Mwanamke kutoka Botswana, Anaeishi  na  virusi  vya  Ukimwi. Mashindo hayo ya Wanawake yaliyo fanyika  2007 , Wanawake walijitokeza ili kuifaamisha jamii kwamba  kuwa na Ukimwi siyo mwisho wa Maisha!!!!!!!!Je wewe unamaoni gani katika hili? Tuungane pamoja katika kuelimishana na kusaidia Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI!!!!!!!!.

Thursday 3 March 2011

Mtoto wetu leo ni Naomi Nyembo!!!!!Mswahili anayeishi Holland!!!!!!!!


Naomi ni mtoto mcheshi na mdadisi mwenye vituko vingi sana , Anayependa shule, picha,kula,kupendeza wakati  wowote na  kupati!!.Je wapendwa matendo ya watoto wetu ni urithi kutoka kwetu,Au ni matokeo ya utandawazi? Nasubiri  maoni yako/yenu ili tuelimishane zaidi,Karibuni  wapendwa!!!!!!!!.

Saturday 26 February 2011

Zilipendwa!!!!!!!!

Haya wapendwa vipi mitindo ya zamani  bado inamvuto?.Je wewe  unaikubali, unaweza kuirudia au itabaki kwenye kumbukumbu!!! karibuni sana  waungwana!!!!!!

Monday 21 February 2011

Wanaume na Majukumu!!!!!!!!

Wanaume wanaokaa vijiweni(maskani), wanaocheza bao siku nzima, wanao shinda vilabuni,wapambe na wengine.Je niukosefu wa kazi,mitaji,ubunifu,uvivu,kuchagua kazi au kukimbia Majukumu yao?Wewe msomaji  unamawazo/ushauri gani?.Tuungane pamoja katika kujifunza karibu sana!!!!!!!

Monday 14 February 2011

Watoto na Uhuru!!!!!!!!

Wazazi /Walezi wenzangu.Wewe una  mawazo  gani  kwa watoto chini ya miaka 15,kupewa uhuru wa kusheherekea  siku zao za kuzaliwa na rafiki zao nje ya nyumbani,tena bila ya usimamizi wetu?.Je ndiyo maendeleo,kuwapatia nafasi wajimwage au?Nasubiri mawazo yako ili tujifunze na kuelimishana katika malezi ya watoto wetu, karibuni sana!!!!!!!!!!!!!

Wednesday 9 February 2011

Wanawake na Mitindo!!!!!!!!!!!!!!!!



Haya wapendwa!Mitindo hii wewe unaionaje au ndiyo kwenda na wakati?.
Je mitindo inatakiwa iendane na sehemu usika? Yaani kama kwenye, Harusi,sokoni,bar na kwingineko.
Wewe unamawazo gani na Mitindo ya kina mama//dada? Tuhabarishane  wapendwa!!!!!!!!