Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Mitindo. Show all posts
Showing posts with label Mitindo. Show all posts

Saturday 2 January 2016

ASYA IDAROUS KHAMSINI ANOGESHA MKESHA WA MWAKA MPYA DMV


Mlimbwende akipita mbele ya mashabiki wa mitindo kuoka kwa gwiji la mitindo Tanzania mama Asya Idarous Khamsini aliponogesha mkesha wa mwaka mpya 2016 uliofanyika Lahnam, Maryaland nchini Marekani. PICHA NA KILIMANJARO STUDIO
Mlimbwende akipita mbele ya mashabiki.
Ni vivazi vya mama wa mitindo Asya Idarous Khamisni.
Mtoto manshallah akiwa ndani ya vazi la mama wa mitindo Asya Idarous Khamsini.
Mlimbwende akipita mbele ya mashabiki wa vivazi.
Ilikua ni vivazi kwa kwenda mbele.
Kijana akijitanashati na kivazi cha Asya Idarous Khamsini.
Gwiji la mitindo na walimbwende wake.
Kwa picha zaidi bofya HAPA

Wednesday 8 June 2011

Wanawake na Urembo!!!!!!!!Haya wapendwa Urembo wakati mwingine unataka Moyo! Kama unavyoona kwenye picha.
Wewe mwanamke/dada unapenda kujiremba na unapendelea nini kuongezea Urembo wako?

Wewe baba/kaka unapenda wanawake/kina dada wanaojiremba na unapenda nini waongezee katika Urembo wao?.

Na jee kwenye Picha hizo nini kimekuvutia na nini Kimekuchukiza?.
Kwa wanaopenda kujiremba, Wanajiremba ili iweje? Ni kujiweka nadhifu,kumfurahisha mpenzi,kujipenda au.......
Na wasiopenda kujiremba, Nini sababu, Nikujiamni, kutojipenda,wapenzi wao hawapendi,kuona Aibu au.....

Karibuni sana Waungwana kwa kuelimishana.

Monday 21 March 2011

Wanaume na Mitindo!!!!!!!!!!!

Leo sina la kusema wapendwa!!! Naicha hii mada mikononi mwenu!! Inaweza kuwa nzuri kwako/mbaya kwa mwenzio.Je wewe Mwanamke/dada unapenda Mumeo aweke vipi Nywele zake au atoke vipi?Haya na Wanaume jee ukiwananywele zipi au mtindo gani  unajiona ukobomba?  Karibuni waungwana ,Raha jipe mwenyewe au?.

Saturday 26 February 2011

Zilipendwa!!!!!!!!

Haya wapendwa vipi mitindo ya zamani  bado inamvuto?.Je wewe  unaikubali, unaweza kuirudia au itabaki kwenye kumbukumbu!!! karibuni sana  waungwana!!!!!!

Wednesday 9 February 2011

Wanawake na Mitindo!!!!!!!!!!!!!!!!Haya wapendwa!Mitindo hii wewe unaionaje au ndiyo kwenda na wakati?.
Je mitindo inatakiwa iendane na sehemu usika? Yaani kama kwenye, Harusi,sokoni,bar na kwingineko.
Wewe unamawazo gani na Mitindo ya kina mama//dada? Tuhabarishane  wapendwa!!!!!!!!

Tuesday 25 January 2011

Wanaume na mitindo!!!!!!!!!


Kumekuwa na mitindo mingi ya wanaume kama,kusuka,kunyoa kipara,kuweka rasta,kuvaa hereni na mingine mingi!jee mitindo hii inaendana na umri wa mtu?