Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday 30 May 2019

Kikombe Cha Asubuhi ;Zaburi 136...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu katika yote....

Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana
Mungu wa walio hai,Mungu  mwenye huruma,Mungu wa upendo
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu

Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!

Ndipo Mose akatenga miji mitatu mashariki ya mto Yordani, ambamo mtu ataweza kukimbilia na kujisalimisha, kama ameua mtu ambaye si adui yake kwa bahati mbaya. Mtu kama huyo ataweza kukimbilia katika mji mmojawapo na kuyaokoa maisha yake.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizo zifanya
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Alitenga mji wa Beseri katika tambarare ya jangwa kwa ajili ya kabila la Reubeni; mji wa Ramothi katika nchi ya Gileadi kwa ajili ya kabila la Gadi, na mji wa Golani katika nchi ya Bashani kwa ajili ya kabila la Manase.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe....
Yahweh  tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni

Yahweh ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu
Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama
inavyokupendeza wewe

Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

Hii ndiyo sheria ambayo Mose aliwapa Waisraeli. Haya ndiyo maamuzi, masharti na maagizo ambayo Mose aliwaambia Waisraeli walipotoka Misri,
Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu,
wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Jehovah ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu kila mmoja na mahitaji yake...
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe
Yahweh tunaomba ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru...
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao....
Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako,
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele....
Amina..!

Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,
Mungu Baba aendelee kuwatendea sawasawa na mapezni yake...

Nawapenda.

Wimbo wa shukrani
1 Taz Zab 100:5; 106:1; 107:1; 118:1 Mshukuruni Mwenyezi-Mungu kwa kuwa ni mwema;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
2Mshukuruni Mungu wa miungu;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
3Mshukuruni Bwana wa mabwana;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
4Ndiye peke yake atendaye makuu ya ajabu;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
5Ndiye aliyeziumba mbingu kwa hekima;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
6Ndiye aliyeitengeneza nchi juu ya vilindi vya maji;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
7Ndiye aliyeumba jua, mwezi na nyota;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
8Jua liutawale mchana;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
9Mwezi na nyota vitawale usiku;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
10Ndiye aliyewaua wazaliwa wa kwanza wa Misri;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
11Akawaondoa watu wa Israeli kutoka huko;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
12Kwa mkono wake wenye nguvu na enzi;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
13Ndiye aliyeigawa Bahari ya Shamu sehemu mbili;
kwa maana fadhili zake zadumu milele,
14akawapitisha watu wa Israeli humo;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
15Lakini akawazamisha humo Farao na jeshi lake;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
16Ndiye aliyewaongoza watu wake jangwani;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
17Ndiye aliyewapiga wafalme wenye nguvu;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
18Akawaua wafalme maarufu;
kwa maana fadhili zake zadumu milele;
19akamuua Sihoni, mfalme wa Waamori,
kwa maana fadhili zake zadumu milele;
20na Ogu, mfalme wa Bashani;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
21Akachukua nchi zao akawapa watu wake;
kwa maana fadhili zake zadumu milele;
22ziwe riziki ya Israeli, mtumishi wake;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
23Ndiye aliyetukumbuka wakati wa unyonge wetu;
kwa maana fadhili zake zadumu milele;
24akatuokoa kutoka maadui zetu;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
25Ndiye akipaye kila kiumbe chenye uhai chakula;
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
26Mshukuruni Mungu wa mbinguni;
kwa maana fadhili zake zadumu milele!


Zaburi136;1-26

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: