Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday 6 May 2019

Kikombe Cha Asubuhi ;Zaburi 118...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Haleluyah ni siku/wiki/mwezi   mwingine tena Mungu wetu ametuchagua

na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Si kwamba sisi tumetenda mema sana wala si kwa nguvu zetu
si kwa utashi wetu wala si kwa akili zetu si kwamba sisi
ni wazuri mno si kwa uwezo wetu sisi kuwa hivi tulivyo leo hii
Ni kwa rehema/neema zake ni kwa mapenzi yake Mungu wetu....

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu
Sifa na Utukufu tunakurudshia Mungu wetu....!!

Yeye huwaporomosha wakuu wenye nguvu, watawala wa dunia huwafanya kuwa si kitu. Mara tu wanaposimikwa na kuanza kuota, hata kabla hawajatoa mizizi kama miti udongoni, Mwenyezi-Mungu akiwapulizia hunyauka, kimbunga huwapeperusha kama makapi!
Tazama jana imepita ee Mungu wetu leo ni siku mpya na kesho ni siku nyingine Jehovah tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
 Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Jehovah usitutie majaribu Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote
Yahweh tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona
Kwakupigwa kwake sisi tumepata kupona...

Mungu Mtakatifu auliza hivi: “Nani basi, mtakayemlinganisha nami? Je, kuna mtu aliye kama mimi?” Inueni macho yenu juu mbinguni! Je, ni nani aliyeziumba nyota hizo? Ni yule aziongozaye kama jeshi lake, anayeijua idadi yake yote, aziitaye kila moja kwa jina lake. Kwa sababu yeye ni mwenye nguvu nyingi, hakuna hata moja inayokosekana.
Yahweh tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe

Baba wa Mbinguni tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu
Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu
Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

Enyi watu wa Israeli wazawa wa Yakobo, kwa nini mnalalamika na kusema: “Mwenyezi-Mungu hatujali sisi! Mungu wetu hajali haki yetu!” Je, nyinyi bado hamjui? Je, hamjapata kusikia? Mwenyezi-Mungu ndiye Mungu wa milele; yeye ndiye Muumba wa kila kitu duniani. Yeye hafifii kamwe wala kuishiwa nguvu. Maarifa yake hayachunguziki. Yeye huwapa uwezo walio hafifu, wanyonge huwapa nguvu. Hata vijana watafifia na kulegea; naam, wataanguka kwa uchovu. Lakini wote wanaomtumainia Mwenyezi-Mungu, watapata nguvu mpya. Watapanda juu kwa mabawa kama tai; watakimbia bila kuchoka; watatembea bila kulegea.
Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu,wote wanaopotia magumu/majaribu mbalimbali
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
 kila mmoja na mahitaji yake 
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe
Baba wa Mbinguni ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako
wakasimaie Neno lako nalo likaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kuomba kwetu
Mungu wetu ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina...!!

Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami
Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea 
kama inavyompendeza yeye....
Nawapenda.

Sala ya shukrani
1 Taz Zab 100:5; 106:1; 136:1 Mshukuruni Mwenyezi-Mungu, kwa kuwa ni mwema,
kwa maana fadhili zake zadumu milele.
2Watu wa Israeli na waseme:
“Fadhili zake zadumu milele.”
3Wazawa wa Aroni na waseme:
“Fadhili zake zadumu milele.”
4Wote wamchao Mwenyezi-Mungu na waseme:
“Fadhili zake zadumu milele.”
5Katika taabu yangu nilimwomba Mwenyezi-Mungu,
naye akanisikia na kuniweka huru.
6 Taz Ebr 13:6 Mwenyezi-Mungu yuko nami, siogopi kitu;
binadamu ataweza kunifanya nini?
7Mwenyezi-Mungu yuko nami, kunisaidia;
nami nitawaona maadui zangu wameshindwa.
8Afadhali kukimbilia usalama kwa Mwenyezi-Mungu,
kuliko kumtumainia mwanadamu.
9Afadhali kukimbilia usalama kwa Mwenyezi-Mungu,
kuliko kuwatumainia viongozi wa dunia.
10Mataifa yote yalinizingira,
lakini kwa jina la Mwenyezi-Mungu nikayaangamiza!
11Yalinizunguka kila upande,
lakini kwa jina la Mwenyezi-Mungu, nikayaangamiza!
12Yalinizunguka, mengi kama nyuki,
lakini yakateketea kama kichaka motoni;
kwa jina la Mwenyezi-Mungu niliyaangamiza!
13Nilishambuliwa mno karibu nishindwe,
lakini Mwenyezi-Mungu alinisaidia.
14Mwenyezi-Mungu ni nguvu yangu kuu;
yeye mwenyewe ndiye wokovu wangu.
15Sauti za furaha ya ushindi zasikika hemani mwao waadilifu:
“Mkono wa Mwenyezi-Mungu umetenda mambo makuu!
16Mkono wa nguvu wa Mwenyezi-Mungu umeleta ushindi!
Mkono wa Mwenyezi-Mungu umetenda mambo makuu!”
17Sitakufa, bali nitaishi,
na kusimulia matendo ya Mwenyezi-Mungu.
18Mwenyezi-Mungu ameniadhibu sana,
lakini hakuniacha nife.
19Nifungulie milango ya watu waadilifu,
niingie na kumshukuru Mwenyezi-Mungu!
20Huu ndio mlango wa Mwenyezi-Mungu,
watu waadilifu watapitia humo.
21Nakushukuru, ee Mungu kwa kunijibu;
kwa sababu wewe ni wokovu wangu.
22 Taz Luka 20:17; Mate 4:11; 1Pet 2:7 Jiwe walilokataa waashi,
limekuwa jiwe kuu la msingi. Taz Mat 21:42; Marko 12:10-11
23Hiyo ni kazi yake Mwenyezi-Mungu
nayo ni ya ajabu sana kwetu.
24Hii ndiyo siku aliyoifanya Mwenyezi-Mungu;
tushangilie na kufurahi.
25 Taz Mat 21:9; Marko 11:9; Yoh 12:13 Tafadhali utuokoe, ee Mwenyezi-Mungu!
Tafadhali utufanikishe, ee Mwenyezi-Mungu!
26 Taz Mat 21:9; 23:39; Marko 11:9; Luka 13:35; 19:38; Yoh 12:13 Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Mwenyezi-Mungu!
Twawabariki kutoka nyumbani mwa Mwenyezi-Mungu
27Mwenyezi-Mungu ni Mungu;
yeye ametujalia mwanga wake
Shikeni matawi ya sherehe,
mkiandamana mpaka madhabahuni.
28Wewe ni Mungu wangu, nami ninakushukuru;
ninakutukuza, ee Mungu wangu.
29Mshukuruni Mwenyezi-Mungu kwa kuwa ni mwema,
kwa maana fadhili zake zadumu milele.


Zaburi118;1-29

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: