Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday 29 May 2019

Kikombe Cha Asubuhi ;Zaburi 135...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante  Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Neema yako yatutosha  Mungu wetu..!

Nyinyi mlijaliwa kuyaona mambo hayo, ili mpate kutambua kwamba Mwenyezi-Mungu, ndiye peke yake Mungu na wala hakuna mwingine. Aliwafanya muisikie sauti yake kutoka mbinguni ili aweze kuwafunza nidhamu; na hapa duniani akawafanya mwone moto wake mkubwa na kusikia maneno yake kutoka katikati ya moto huo.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa  Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Kwa kuwa aliwapenda wazee wenu, yeye amewateua nyinyi wazawa wao, akawatoa yeye mwenyewe nchini Misri kwa nguvu yake kuu. Aliyafukuza mbele yenu mataifa makubwa na yenye nguvu kuliko nyinyi, ili awalete na kuwapeni nchi yao iwe urithi wenu, kama ilivyo hadi leo!
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe

Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu  wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo 

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...


Basi, kumbukeni leo na kuweka mioyoni mwenu, kwamba Mwenyezi-Mungu ndiye Mungu juu mbinguni na chini duniani; hakuna mwingine. Kwa hiyo shikeni masharti yake na amri zake ambazo ninawapeni leo ili mfanikiwe, nyinyi pamoja na wazawa wenu, na kuishi siku nyingi katika nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, anawapeni iwe yenu milele.”
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba
 ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....

Nawapenda.

Sifa kwa Mungu
1Msifuni Mwenyezi-Mungu!
Lisifuni jina la Mwenyezi-Mungu,
msifuni enyi watumishi wake.
2Msifuni enyi mkaao katika nyumba yake,
ukumbini mwa nyumba ya Mungu wetu!
3Msifuni Mwenyezi-Mungu kwa kuwa ni mwema;
mtukuzeni kwa nyimbo maana inafaa.135:3 maana inafaa: Au Maana ni mwema.
4Mwenyezi-Mungu amemchagua Yakobo kuwa wake,
nyinyi watu wa Israeli kuwa mali yake mwenyewe.
5Najua hakika kuwa Mwenyezi-Mungu ni mkuu;
Bwana wetu ni mkuu juu ya miungu yote.
6Mwenyezi-Mungu hufanya chochote anachotaka,
mbinguni, duniani, baharini na vilindini.
7Ndiye aletaye mawingu kutoka mipaka ya dunia;
afanyaye gharika kuu kwa umeme,
na kuvumisha upepo kutoka ghala zake.
8Ndiye aliyewaua wazaliwa wa kwanza huko Misri,
wazaliwa wa watu na wanyama kadhalika.
9Ndiye aliyefanya ishara na maajabu kwako, ee Misri,
dhidi ya Farao na maofisa wake wote.
10Ndiye aliyeyaangamiza mataifa mengi,
akawaua wafalme wenye nguvu:
11Kina Sihoni mfalme wa Waamori,
Ogu mfalme wa Bashani,
na wafalme wote wa Kanaani.
12Alichukua nchi zao na kuwapa watu wake;
naam, ziwe riziki ya watu wake Israeli.
13Jina lako, ee Mwenyezi-Mungu, ladumu milele,
utakumbukwa kwa fahari nyakati zote.
14Mwenyezi-Mungu atawatetea watu wake;
na kuwaonea huruma watumishi wake.
15 Taz Zab 115:4-8; Ufu 9:20 Miungu ya uongo ya mataifa ni fedha na dhahabu,
imetengenezwa kwa mikono ya binadamu.
16Ina vinywa, lakini haisemi;
ina macho, lakini haioni.
17Ina masikio, lakini haisikii;
wala haiwezi hata kuvuta pumzi.
18Wote walioifanya wafanane nayo,
naam, kila mmoja anayeitegemea!
19Enyi watu wa Israeli, mtukuzeni Mwenyezi-Mungu!
Enyi makuhani, mtukuzeni Mwenyezi-Mungu!
20Enyi Walawi, mtukuzeni Mwenyezi-Mungu!
Enyi wachaji wa Mwenyezi-Mungu, mtukuzeni!
21Atukuzwe Mwenyezi-Mungu katika Siyoni,
atukuzwe katika makao yake Yerusalemu.
Msifuni Mwenyezi-Mungu!

Zaburi135;1-21

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: