Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 14 May 2019

Kikombe Cha Asubuhi ;Zaburi 124...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu katika yote....

Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana
Mungu wa walio hai,Mungu  mwenye huruma,Mungu wa upendo
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu

Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!

Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Ole wao watoto wanaoniasi, wanaotekeleza mipango yao na si mipango yangu, wanaofanya mikataba kinyume cha matakwa yangu! Naam, wanarundika dhambi juu ya dhambi. Bila kunitaka shauri, wanafunga safari kwenda Misri, kukimbilia usalama katika ulinzi wa Farao, kupata mahali pa usalama nchini Misri.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote 
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Lakini ulinzi wa Farao utakuwa aibu yenu, na usalama nchini Misri utakuwa fedheha yenu. Maana ingawa maofisa wao wamefika Soani, na wajumbe wao mpaka Hanesi, wote wataaibishwa na hao wasioweza kuwasaidia, watu ambao hawawezi kuwapa msaada au faida, ila tu kuwapa aibu na fedheha.”
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomna ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe...

Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Yahwe ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii..
Baba wa Mbinguni  tunaomba ukatupe neema ya kufuata
njia zako,tukasimamie Neno lako,amri na sheria zako
siku zote za maisha yetu...
Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukatufanye chombo chema
ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....

Kauli ya Mungu juu ya wanyama wa pande za Negebu: “Wajumbe wanapita katika nchi ya taabu na shida, yenye simba, nyoka wa sumu na majoka. Wamewabebesha wanyama wao mali zao, kuwapelekea watu wasioweza kuwafaa kitu. Maana msaada wa Misri ni bure, haufai kitu; kwa hiyo nimeipanga Misri jina: ‘Joka lisilo na nguvu!’”
Tazama watoto wako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
kila mmoja na mahitaji yake
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipo kwenda kinyume nawe
Yahweh tunaomba ukawape neema ya kuweza kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru...
Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele...
Amina...!!


Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake...
Nawapenda.

Mungu kinga yetu
(Wimbo wa Kwenda Juu, wa Daudi)
1“Kama Mwenyezi-Mungu asingalikuwa upande wetu
Semeni nyote mlio katika Israeli:
2“Kama Mwenyezi-Mungu asingalikuwa upande wetu,
wakati ule tuliposhambuliwa na maadui,
3hakika tungalimezwa tukiwa hai,
wakati hasira zao zilipotuwakia.
4Tungalikumbwa na gharika,
tungalifunikwa na mto wa maji,
5mkondo wa maji ungalituchukua!”
6Atukuzwe Mwenyezi-Mungu,
ambaye hakutuacha makuchani mwao.
7Tumeponyoka kama ndege mtegoni;
mtego umeteguliwa, nasi tukaokoka.
8Msaada wetu watoka kwa Mwenyezi-Mungu,
aliyeumba mbingu na dunia.


Zaburi124;1-8

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: