Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 3 April 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Kutoka 3...Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Tuanze na Mungu katika siku/wiki hii,Tumshukuru kwa yote mema aliyotutendea/anayotundea...Yeye ndiye aliyetupa kibali cha kuiona leo hii..Yeye alituchagua sisi kuendelea kuiona siku hii..Yeye ni Muumba wetu na Muumba mbingu na Nchi,Yeye awezaye yote akisema ndiyo nani aseme hapana,Yeye ni Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..Yeye atupeae ridhiki zetu na yeye tunaomba azibariki ziingiapo/zitokapo..
Upendo,Furaha,Amani, wema na Fadhili zipo kwake..
Namngojea Mungu peke yake kwa utulivu; kwake naliweka tumaini langu. Yeye peke yake ndiye mwamba na wokovu wangu, yeye ni ngome yangu, sitatikisika. Wokovu na fahari yangu vyatoka kwa Mungu; mwamba wangu mkuu na kimbilio langu ni Mungu. Enyi watu, mtumainieni Mungu daima; mfungulieni Bwana yaliyo moyoni mwenu. Mungu ndiye kimbilio la usalama wetu. Binadamu wote ni kama pumzi tu; wote, wakubwa kwa wadogo, hawafai kitu. Tena ukiwapima uzito hawafikii kilo, wote pamoja ni wepesi kuliko pumzi. Msitegemee dhuluma, msijisifie mali ya wizi; kama mali zikiongezeka, msizitegemee. Mungu ametamka mara moja, nami nimesikia tena na tena: Kwamba enzi ni mali yake Mungu; naam, nazo fadhili ni zake Bwana; humlipa kila mtu kadiri ya matendo yake.


Asante Mungu Baba wa Mbinguni kwa nafasi hii..Tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza na kujiachilia mikononi mwako..Tukiomba na kulisifu jina lako lilo kuu..Mungu Baba tunaomba utubariki Tuingiapo/Tutokapo,Vyombo vya usafiri,tutembeapo hatua zetu ziwe nawe Yahweh..Baba ukabariki kazi zetu,Biashara,Masomo na vyote tunavyoenda kugusa/kutumia ukavitakase kwa Damu ya mwanao Bwana wetu na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti aliteseka ili sisi tupate kupona..Roho Mtakatifu akatuongoze kwenye kunena/kutenda, tupate kujitambua/kutambua..
Baba tunaomba utusamehe pale tulipokwenda kinyume nawe..
nasi utupe Neema ya kuweza kusameheana..
Jehovah...! uwaponye wote wanaopitia Magumu,Majaribu, Shida/Tabu,Wagonjwa,Wafiwa ukawe mfariji wao,Baba tazama walio magerezani pasipo na hatia,pia waliofungwa na mwovu..tunaomba ukawaguse na kuwaponya kimwili na kiroho..
Sema nasi Baba..!!Sema na mioyo yetu Baba..!!Sema nasi tupate kupona..!!Ilikuwa jioni ya siku hiyo ya Jumapili. Wanafunzi walikuwa wamekutana pamoja ndani ya nyumba, na milango ilikuwa imefungwa kwa sababu waliwaogopa viongozi wa Wayahudi. Basi, Yesu akaja, akasimama kati yao, akawaambia, “Amani kwenu!” Alipokwisha sema hayo, akawaonesha mikono yake na ubavu wake. Basi, hao wanafunzi wakafurahi mno kumwona Bwana. Yesu akawaambia tena, “Amani kwenu! Kama vile Baba alivyonituma mimi, nami nawatuma nyinyi.” Alipokwisha sema hayo, akawapulizia na kuwaambia, “Pokeeni Roho Mtakatifu. Mkiwasamehe watu dhambi zao, wamesamehewa; msipowasamehe, hawasamehewi.” Thoma, mmoja wa wale kumi na wawili (aitwaye Pacha), hakuwa pamoja nao wakati Yesu alipokuja. Basi, wale wanafunzi wengine wakamwambia, “Tumemwona Bwana.” Thoma akawaambia, “Nisipoona mikononi mwake alama za misumari na kutia kidole changu katika kovu hizo, na kutia mkono wangu ubavuni mwake, sitasadiki.” Basi, baada ya siku nane hao wanafunzi walikuwa tena pamoja mle ndani, na Thoma alikuwa pamoja nao. Milango ilikuwa imefungwa, lakini Yesu akaja, akasimama kati yao, akasema, “Amani kwenu!” Kisha akamwambia Thoma, “Lete kidole chako hapa uitazame mikono yangu; lete mkono wako ukautie ubavuni mwangu. Usiwe na mashaka, ila amini!” Thoma akamjibu, “Bwana wangu na Mungu wangu!” Yesu akamwambia, “Je, unaamini kwa kuwa umeniona? Heri yao wale ambao hawajaona, lakini wameamini.” Yesu alifanya mbele ya wanafunzi wake ishara nyingine nyingi ambazo hazikuandikwa katika kitabu hiki. Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mpate kuwa na uhai kwa nguvu ya jina lake.
Tunarudisha Shukrani na Utukufu ni kwao..Tunayaweka haya yote mikononi mwako Baba yetu..Tukiamini wewe ni Bwana na Mwokozi wetu,Leo na Hata milele..!!
Amina.
Mungu ni Pendo.

Mungu anamwita Mose

1Siku moja, Mose alikuwa anachunga kundi la kondoo la baba mkwe wake, Yethro, kuhani wa Midiani. Mose alilipeleka kundi hilo upande wa magharibi wa jangwa, akaufikia mlima Horebu,3:1 Horebu: Jina lingine la mlima Sinai. Hapa waitwa mlima wa Mungu, kwani Mungu atajidhihirisha hapa; Taz sura 19. mlima wa Mungu. 2Basi, malaika wa Mwenyezi-Mungu akamtokea katika mwali wa moto katikati ya kichaka. Mose akaangalia, akashangaa kuona kichaka kinawaka moto na wala hakiungui. 3Basi, akajisemea, “Hiki ni kioja! Kichaka kuwaka moto na kisiungue? Hebu nitazame vizuri.”
4Mwenyezi-Mungu alipoona kwamba Mose amegeuka kukiangalia kichaka, akamwita pale kichakani, “Mose! Mose!” Mose akaitika, “Naam! Nasikiliza!” 5Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Usije karibu! Vua viatu vyako kwa sababu mahali unaposimama ni mahali patakatifu.” 6Kisha Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu wa baba yako; Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo.” Mose akaufunika uso wake kwa kuwa aliogopa kumwangalia Mungu.
7Kisha Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Nimeyaona mateso ya watu wangu walioko nchini Misri na nimekisikia kilio chao kinachosababishwa na wanyapara wao. Najua mateso yao, 8na hivyo, nimeshuka ili niwaokoe mikononi mwa Wamisri. Nitawatoa humo nchini na kuwapeleka katika nchi nzuri na kubwa; nchi inayotiririka maziwa na asali,3:8 nchi inayotiririka maziwa na asali: Ni nchi yenye rutuba na wingi wa mifugo (maziwa) na mavuno (asali). nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi na Wayebusi. 9Naam, kilio cha Waisraeli kimenifikia; nimeona jinsi Wamisri wanavyowatesa. 10Sasa, nitakutuma kwa Farao ili uwatoe watu wangu, watu hao wa Israeli, kutoka nchini Misri.”
11Lakini Mose akamwambia Mungu, “Mimi ni nani hata nimwendee Farao na kuwatoa Waisraeli nchini Misri?” 12Mungu akamwambia, “Mimi nitakuwa pamoja nawe. Utawatoa watu wa Israeli na kuja kuniabudu mimi Mungu juu ya mlima huu. Hiyo itakuwa ishara kwamba ni mimi Mungu niliyekutuma wewe.”
13 Taz Kut 6:2-3 Hapo, Mose akamwambia Mungu, “Sasa, nikiwaendea Waisraeli na kuwaambia, ‘Mungu wa babu zenu amenituma kwenu,’ nao wakiniuliza, ‘Jina lake ni nani,’ nitawaambia nini?” 14Taz Ufu 1:4,8 Mungu akamjibu, “MIMI NDIMI NILIYE.3:14 MIMI NDIMI NILIYE: Au, NIKO KAMA NILIVYO au NITAKUWA KAMA NITAKAVYOKUWA. Waambie hivi watu wa Israeli: Yule anayeitwa, NDIMI NILIYE, amenituma kwenu. 15Waambie hivi Waisraeli: Mwenyezi-Mungu,3:15 Tafsiri hii mpya ya Kiswahili kila mara jina la Kiebrania Yahweh linapotumika limewekwa katika Kiswahili jina la kawaida la Mungu kama anavyotajwa katika lugha yetu, yaani, Mwenyezi-Mungu. Mungu wa babu zenu, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenituma kwenu. Hili ndilo jina langu milele, na hivyo ndivyo nitakavyokumbukwa katika vizazi vyote. 16Nenda ukawakusanye wazee wa Israeli na kuwaambia: Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zenu: Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenitokea na kusema, ‘Nimewachunguzeni na kuyaona mambo mnayotendewa nchini Misri! 17Naahidi kuwa nitawatoa katika mateso yenu huko Misri na kuwapeleka katika nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi na Wayebusi; nitawapeleka katika nchi inayotiririka maziwa na asali.’
18“Wao watakusikiliza, nawe pamoja na wazee wa Waisraeli mtamwendea mfalme wa Misri na kumwambia, ‘Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Waebrania, ametutokea. Sasa, uturuhusu tuende safari ya mwendo wa siku tatu jangwani, tukamtambikie Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.’ 19Najua kuwa mfalme wa Misri hatawaacha mwende asipolazimishwa kwa mkono wenye nguvu. 20Kwa hiyo nitaunyosha mkono wangu na kuipiga nchi ya Misri kwa maajabu ambayo nitayafanya huko. Baadaye mfalme atawaacha mwondoke. 21Taz Hek 10:17 Tena nitahakikisha Wamisri wanawapendelea Waisraeli, na mtakapoondoka Misri, hamtatoka mikono mitupu. 3:21 Taz Kut 12:35-36 22Kila mwanamke Mwebrania atamwomba jirani yake Mmisri, au mgeni wake aliye nyumbani kwake, ampe vito vya fedha na dhahabu pamoja na nguo. Hivyo mtawavisha watoto wenu wa kiume na wa kike. Ndivyo mtakavyowapokonya Wamisri mali yao.”

Kutoka3;1-21

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: