Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday 28 April 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Kutoka 22...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Tushuke mbele za Mungu tukishukuru na kusifu..
Mtakatifu..!!Mtakatifu..!!Mtakatifu..!! Baba wa Mbinguni,Mungu wetu na Muumba wetu, Muumba wa  Mbingu na Nchi na vyote vilivyomo ni mali yako, hata sisi Baba ni Mali yako, Hatuna Mungu mwingine zaidi yako, Hakuna wa kuabudiwa kama wewe, Hakuna Mlinzi na Muamuzi katika maisha yetu zaidi yako..Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..
Tunakushukuru na kukusifu daima, Asante kwa ulinzi wako Usiku mzima..
Asante kwa Fadhili na wema wako Baba,Asante kwa Kibali chako na  Kutuchagua tena  kuendela kuiona siku hii..si kwanguvu zetu au ujuzi wetu Baba ni kwa Neema/Rehema zako Mfalme wa Amani..

Tazama Jana imepita Baba Leo ni siku mpya na Kesho ni siku nyingine Jehovah..!!
Tunajiachilia mikononi mwako tukijinyenyekeza na kuomba Utamalaki na kutuatamia Yaweh... katika Nyumba zetu,watoto wetu,familia zetu na maisha yetu yapo mikononi mwako Jehovah..!


Yesu Mchungaji Mwema..!!
Basi, akasema tena, “Kweli nawaambieni, mimi ni mlango wa kondoo. Wale wengine wote waliokuja kabla yangu ni wezi na wanyanganyi, nao kondoo hawakuwasikiliza. Mimi ni mlango. Anayeingia kwa kupitia kwangu ataokolewa; ataingia na kutoka, na kupata malisho. Mwizi huja kwa shabaha ya kuiba, kuua na kuharibu. Mimi nimekuja mpate kuwa na uhai – uhai kamili. “Mimi ni mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo wake. Mtu wa kuajiriwa ambaye si mchungaji, na wala kondoo si mali yake, anapoona mbwamwitu anakuja, huwaacha kondoo na kukimbia, kisha mbwamwitu huwakamata na kuwatawanya. Yeye hajali kitu juu ya kondoo kwa sababu yeye ni mtu wa mshahara tu. Mimi ni mchungaji mwema. Nawajua walio wangu, nao walio wangu wananijua mimi, kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Mimi nayatoa maisha yangu kwa ajili yao. Tena ninao kondoo wengine ambao hawamo zizini humu. Inanibidi kuwaleta hao pia, nao wataisikia sauti yangu, na kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja. “Baba ananipenda kwani nautoa uhai wangu ili nipate kuupokea tena. Hakuna mtu anayeninyanganya uhai wangu; mimi nautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa na uwezo wa kuuchukua tena. Hivi ndivyo Baba alivyoniamuru nifanye.” Kukawa tena na mafarakano kati ya Wayahudi kwa sababu ya maneno haya. Wengi wao wakasema, “Ana pepo; tena ni mwendawazimu! Ya nini kumsikiliza?” Wengine wakasema, “Haya si maneno ya mwenye pepo. Je, pepo anaweza kuyafumbua macho ya vipofu?”


Karibu kwenye mioyo yetu  utawale na kutuongoza katika yote,utupe macho ya rohoni Mfalme wa Amani tupate kutambua na kujitambua..Tukawe chombo chema na tukatumike sawasawa na mapenzi yako, tusiwe watu wa kujisifu wala kujitapa,tukawatendee wengine wema na tuwapende kama unavyotupenda sisi,tukawe na kiasi na utuokoe na kisasi Baba wa Mbinguni..
Tunaomba utusamehe pale tulipokwenda kinyume nawe Mfalme wa Amani kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua au kutojua..
Tunaomba utupe  na sisi Neema ya kuweza kuwasamehe waliotukosea..
Baba tunaomba ukawaguse na kuwaponya wote wanaopitia majaribu/magumu,wenye shida/tabu, wagonjwa, wafiwa ukawe mfariji wao..ukawafungue walio kwenye vifungo mbali mbali Baba..wapate kupona kimwili na kiroho pia..
Yahweh..!! tunaomba ubariki kazi zetu, Biashara,Masomo,Vilaji/vinywaji,vyombo vya usafiri, tutembeapo hatua zetu ziwe nawe.. ututakase Miili yetu na Akili zetu na vyote tunavyoenda kugusa kutumia ukavitakase kwa Damu ya mwanao mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti..yeye aliteseka ili sisi tupate kupona.
Tunayaweka haya mikononi mwako tukiamini na kukusifu daima..Tunashukuru na kukuabudu tukiamini wewe ni Mungu wetu Leo kesho na hata Milele..
Amina..!
Mungu awabariki sana na Asanteni sana kwa kupitia hapa
Nawapenda.



Maagizo juu ya malipo

1“Mtu akiiba ng'ombe au kondoo na kumchinja au kumwuza, atatozwa ng'ombe watano kwa kila ng'ombe, na kondoo wanne kwa kila kondoo. 2Mwizi akipatikana anavunja nyumba, akapigwa hata akafa, aliyemuua hana hatia ya mauaji. 3Lakini mwizi huyo akishikwa wakati jua limechomoza na kuuawa, aliyemuua atakuwa na hatia. Huyo mwizi anapaswa kulipa. Ikiwa hana kitu cha kulipa, basi, yeye mwenyewe atauzwa ili kulipia wizi wake. 4Kama mnyama aliyeibiwa atapatikana kwa huyo mwizi akiwa hai, basi, mwizi atalipa mara mbili, awe ni ng'ombe, punda au kondoo.
5“Mtu akiwalisha wanyama wake katika shamba la mizabibu au kumwachia mnyama wake kula katika shamba la mtu mwingine, atalipa hasara hiyo kwa mazao bora ya shamba lake mwenyewe au shamba lake la mizabibu.
6“Mtu akiwasha moto nao ukachoma miti ya miiba na kusambaa hadi kuteketeza miganda ya nafaka, au nafaka ya mtu mwingine ambayo bado haijavunwa, au shamba lote likateketea, aliyewasha moto huo lazima alipe hasara hiyo yote.
7“Mtu akimwachia mwenzake fedha au mali nyingine amtunzie, kisha ikaibiwa nyumbani mwake, mwizi akipatikana lazima alipe thamani yake mara mbili. 8Lakini mwizi asipopatikana, mwenye nyumba atakaribia mbele za Mungu ili kuthibitisha kwamba hakuhusika na wizi wa mali ya mwenzake.
9“Pakiwa na ubishi juu ya ng'ombe, au punda, au kondoo, au mavazi, au kitu chochote kilichopotea ambacho kila mmoja anadai ni chake, wanaohusika wataletwa mbele za Mungu. Yule ambaye Mungu ataamua amekosa, atamlipa mwenzake mara mbili.
10“Mtu akimkabidhi mwenzake punda, ng'ombe, kondoo au mnyama mwingine yeyote amtunzie, na mnyama huyo akafa au akaumia au akachukuliwa bila mtu yeyote kushuhudia, 11kiapo mbele ya Mwenyezi-Mungu kitaamua kati yao, kuonesha kwamba huyo aliyekabidhiwa hakuhusika na wizi wa mali ya mwenzake. Mwenye mnyama huyo atakubali hicho kiapo, na huyo mwenzake hatalipa malipo yoyote. 12Lakini kama aliibiwa kwake, ni lazima amlipe mwenyewe. 13Kama huyo mnyama aliraruliwa na wanyama wa porini, huyo mtu aliyekuwa amekabidhiwa lazima amlete kama ushahidi. Hatalipa malipo yoyote kwa ajili ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama wa porini.
14“Mtu akiazima mnyama kwa mwenzake, kisha mnyama huyo akaumia au akafa wakati mwenyewe hayuko, aliyeazima mnyama huyo ni lazima alipe kikamilifu. 15Lakini kama mwenyewe alikuwako, basi aliyemwazima hatalipa chochote. Kama alikuwa ni mnyama aliyekodishwa, mwenyewe ataikubali tu bei ya kukodisha.

Sheria za maadili

16 Taz Kumb 22:28-29 “Mtu akimshawishi bikira ambaye hajaposwa, akalala naye, lazima atoe mahari na kumwoa msichana huyo. 17Baba wa huyo msichana akikataa katakata kumwoza binti yake, mtu huyo atalipa fedha ya mahari inayostahili msichana aliye bikira.
18“Usimwache mwanamke mchawi aishi.
19“Anayezini na mnyama lazima auawe.
20“Anayemtolea tambiko mungu mwingine badala ya Mwenyezi-Mungu pekee, lazima aangamizwe kabisa.
21“Msimdhulumu mgeni wala kumtesa, maana nanyi pia mlikuwa wageni nchini Misri. 22Msimtese mjane au yatima. 23Kama mkiwadhulumu hao nao wakanililia, hakika nitakisikiliza kilio chao, 24na hasira yangu itawaka, nami nitawaueni kwa upanga, na wake zenu watakuwa wajane na watoto wenu yatima.
25“Ukimkopesha fedha mtu yeyote miongoni mwa watu wangu walio maskini, usiwe kwake kama mdai, wala usimtoze riba. 26Ukilichukua vazi la mwenzako kuliweka rehani, lazima umrudishie kabla ya jua kutua, 27kwa kuwa hiyo ndiyo nguo yake ya pekee; ndiyo atakayojifunika nayo. Au wadhani atalalia nini? Akinililia nitamsikiliza, maana mimi ni mwenye huruma.
28“Usimtukane Mungu, wala kumlaani mkuu wa watu wako.
29“Usikawie kunitolea sehemu yangu kutokana na wingi wa mazao yako na divai yako. Mtanipa wazaliwa wenu wa kwanza wa kiume. 30Mtafanya vivyo hivyo kuhusu wazaliwa wa kwanza wa ng'ombe na kondoo wenu. Mtamwacha kila mzaliwa wa kwanza na mama yake kwa siku saba, na siku ya nane mtanitolea. 31Nyinyi mtakuwa watu waliowekwa wakfu kwangu. Kwa hiyo hamtakula nyama ya mnyama aliyeuawa na mnyama wa porini. Nyama hiyo mtawatupia mbwa.

Kutoka22;1-31

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: