Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 21 June 2011

Wanaume na Mitindo,Leo wenye Rasta Eti!!!!!!!

                                           Simon wa Kitutruru [kitururu Mawazoni ,Blog]
                                         Bob Sankofa [Fotobaraza blog]
                                     Arba wa Manillah [Kukaye moto Blog/Mziki]
                                   Mrisho Mpoto [Muziki,blog]


Wapendwa Kufuga nywele ni kupenda si kama vinyozi hakuna!!!Kumekuwa na mtazamo wa baadhi ya watu kuhusu Rasta.Watu waonaopenda kuwa na Mtindo huo kuonenakana kama Wahuni,Wavuta bangi,hawatakiwi kula Nyama na Si heshima kwa jamii. Labda nisimalize yote nawe kama unayo  unayoyajua mengi.


Je Unasemaje kuhusu haya?
Karibuni sana kwa kuelimishana na Kutoa mawazo, maoni,Ushauri wako!!!!.

9 comments:

Simon Kitururu said...

Kwa BABA yangu MZAZI kama huchani nywele na huchomekei shati wewe MHUNI!

Na kama unasikiliza reggea ambayo ni baadhi ya miziki ambayo haipendi -basi wewe unavuta bangi!:-( Ingawa ukiwa chekibobu na na hata bonge la wei anaweza kuwa akialikwa mahalia nataka uvae suti na uende nae huko kujichekelesha kwa marafiki zake.:-(

Mie kilevi changu nahisi mnakijua kama mmeshawahi kunitembelea kwenye blogu yangu ! Nacho kinahusisha glasi au chupa ! Ila kwenye moshi wowote sipo!:-(

Nyama inaenda kisawasawa! Mbogamboga pia kwa hiyo nahisi mavejeteriani nawapiga bao kwa kuwa vyao nala na vyangu NI vyangu hasa kama hivyo ni kitimoto!:-(

Na nikiwa BONGO mpaka leo Bia yangu ni SAFARI! Ingawa BIA ya kwanza niliyoinywa mpaka nikalewa utotoni ni Stela Atois.:-(

Na kuhusu nywele! Sipendi kuchana nywele na mpaka umri huu baada ya High School Mazengo Dodoma , sijapata sababu ya kukata nywele.

Na ndio nishawahi kuwa na Kalikiti, nishawahi kusuka mabutu, twende kilioni nk. Ila staili hizo hazikuwahi kuishi kichwani mwangu wiki na ni enzi hizo!

Ingawa nakumbuka kila staili niliyokuwa nayo ENZI hizo kabla ya kuacha kuchana nywele (kwa mfano ile ya kalikiti )ilikuwa inanifanya nipendwe na mademu tofauti (tukifanya kipimo ni ndoano ya nani anakuchekeachekea NA KUNASA katika kukugawia unyumba ukiwa unashidanao ).

Na haki ya nani baada ya kuacha kuchana nywele kuna masista duu walinitenga!:-(


ILA kwa kipimo kingine!

Naudhaifu wakujisikia KISAIKOLOJIA bonge la MUAFRIKA SANA saa nyingine kisa SICHANI NYWELE na from ten MILES utajua tu kuwa JAMAA ambaye unayemkaribia kakaa KIAFRIKA .

Na kakaa kiafrika hata katika shughuli zangu ambazo hufanya KARIBU kila siku KWA KAWAIDA navaa suti karibu mwaka MZIMA hata kishughuli!:-(

Mzee wa Changamoto said...

UKWELI ni kuwa NAMNA UNAVYOONA TATIZO NI TATIZO.
Yaani yule anayeonekana anapenda wanawake anaonekana anafanya dhambi ya uzinzi kuliko yule "mtakatifu" anayejichua kila akimuona mwanamnke.
Yaani kuna wanaoonekana wahuni kwa kuwa wana mtazao wa nje ulio tofauti na wa kwetu, hata kama hiyo ndiyo tofauti pekee tuliyonayo.
Ati wapo wanaoamini kuwa RASTA zamaanisha kitu fulani. Wapo wanaodhani kwa mtu kufuga nywele kichwa itamaanisha anaamini hivi ama vile. Anatenda hili ama lile, ana mtazamo huu ama ule na / ama anakula hiki ama kile.
HAPANA.
Morgan Heritage waliwahi kusema "You DON'T have to dread to be rasta. This is NOT the dreadlock thing, but divine conception of the heart"
Yote juu ya yote ni kuwa BINADAMU NIM'BINAFSI SANA kiasi kwamba anataka aamini kuwa anachoamini ndicho sahihi hata kama imani yake ni kinyume na ukeli wa imani ya ajaribuye kumtafsiri.
Ni ubinafsi huo unaomfanya Kitururu asione sababu ya kukata nywele hata kama MCHUNGAJI wake alikuwa akihimiza hilo na hata Baba yake kupenda "wei".
Ni ubinafsi huo unanifanya niamini kuwa aaminiye tofauti nao ni M'BINAFSI nami ni-sahihi.
SUALA KUU NI KUJIAMINI TULIVYO. Juzi nimeona T-SHIRT ikisema "I am one of the best people i know"
Hahahahahahahahahaaaaaaaaaaaa
Labda mimi sikuwa na sababu yoyote ya kuwa na rasta nilipokuwa nazo, na labda sikuwa na sababu ya kuzikata na kuwa nilivyo.
Ndio maana bad naamini kuwa NAMNA TUONAVYO TATIZO NDIO TATIZO

Teuvo Vehkalahti said...

Greetings from Finland. This, through a blog is a great get to know other countries and their people, nature and culture. Come take a look Teuvo images and blog to tell all your friends that your country flag will stand up to my collection of flag higher. Sincerely, Teuvo Vehkalahti Finland

chib said...

Mzungu wa Finland naye, ha ha haaa

emu-three said...

Mzungu anatafuta marafiki ...mwambieni `TUPO PAMOJA, AJE BONGO AWEKEZE, KWANI RANGI YAKE INATOSHA KUPEWA KIPAUMBELE...lol
Ama kwa swala la rasta, mimi sijui, labda tusema ni `hisia' za kila mtu...nakumbuka tukiwa jeshini ulitakiwa usiwe na nywele, ..nakumbuka tukiwa shule halikadhalika...! Kwahiyo huo ni utashi wa mtu, lakini wahenga wanasema `ukifika kwa wenye chongo na wewe fumba jicho...' sio mbaya,...Mzee wetu mpenzi wa watu alitumabia RUHUSA' UKITAKAA HIKI RUHUSA...akaitwa mzee wa Rukhusa!

Rachel Siwa said...

Ahsanteni sana wapendwa wangu! @Kaka Kitururu na Kaka Mubelwa,Nimewapata sana na kuwaelewa, na maelezo yenu yamenifunza mengi mimi na wote waliopita hapa wakuwa wamefaidika.

@ndugu yangu Emu-3 pamoja,@ Chib naona Mthungu amekufurahisha sana!@Mthungu/Teuvo asante pia/Thanks!!!

Unknown said...

Arrooo.

Ras choyo said...

hizo sio Rasta, hivyo ni vishungi/vifundo ama dread kwa kizungu. Rasta ni kifupisho cha Rastafarian ambayo ni imani inayoamini kwamba mfalme Haile Selasie ndiye Masihi/masiya (Ras Tafar ni jina halisi la Haile selasie kabla ya kuwa mfalme, alipewa jina la haile selasie lenye maana ya 'nguvu ya utatu mtakatifu' mara baada ya kushika ufalme wa ethiopia, hii ni sawa na mapapa wa kanisa katoliki hupewa majina mengine kama vile John, benedict, baada ya kupewa u-papa). Rastafarians huamini kwamba bustani ya Eden iko ethiopia kwani ufafanuzi wake kwenye kitabu cha MWANZO unatoa ushahidi kuwa ni ethiopia kwani jina KUSH limetajwa (soma Mwanzo kwa uhakika zaidi) vile vishungi vya nywele hufugwa muumini wa Rastafari anapoingia kwenye nadhiri ya kumtumikia Mungu kwenye maisha yake yote (rejea jinsi samson wa kwenye biblia alivyowekewa nadhiri ya kumtumikia Mungu na kuamriwa kutonyoa nywele)

Ras choyo said...

hizo sio Rasta, hivyo ni vishungi/vifundo ama dread kwa kizungu. Rasta ni kifupisho cha Rastafarian ambayo ni imani inayoamini kwamba mfalme Haile Selasie ndiye Masihi/masiya (Ras Tafar ni jina halisi la Haile selasie kabla ya kuwa mfalme, alipewa jina la haile selasie lenye maana ya 'nguvu ya utatu mtakatifu' mara baada ya kushika ufalme wa ethiopia, hii ni sawa na mapapa wa kanisa katoliki hupewa majina mengine kama vile John, benedict, baada ya kupewa u-papa). Rastafarians huamini kwamba bustani ya Eden iko ethiopia kwani ufafanuzi wake kwenye kitabu cha MWANZO unatoa ushahidi kuwa ni ethiopia kwani jina KUSH limetajwa (soma Mwanzo kwa uhakika zaidi) vile vishungi vya nywele hufugwa muumini wa Rastafari anapoingia kwenye nadhiri ya kumtumikia Mungu kwenye maisha yake yote (rejea jinsi samson wa kwenye biblia alivyowekewa nadhiri ya kumtumikia Mungu na kuamriwa kutonyoa nywele)