Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 19 June 2011

Leo ni Siku ya wa BABA!!!!!!!!

                                  Sandra & Tracey na Baba yao.[Faraja Yangu ].
                                        Joel & Jolen na Baba yao.
                                         Arianna na BABA!!.
.
                                     Baba Paulina.
                                        Sabrina na BABA.
                                      Jawahiri na BABA.
                                       Anna-Harrieth na BABA.
Nawatakia Kheri wa BABAWote popote mlipo, Mungu awabariki sana.
Tuwe bega kwa bega katika malezi ya watoto,Kama si Baba tusingeitwa mama.
Pia Shukrani kwa baba yangu Mpendwa [R.I.P]


Kama una Picha au salamu kwa BABA  yeyote Rukhsaaaaaa!!!! Tuma kupitia Rasca@hotmail.co.uk


Wapendwa kina BABA wa leo/kisasa  na Wazamani,  Kundi lipi linaongoza Kutelekeza Watoto/Familia?
Na Sababu ni nini, Nyumba ndogo, Ulevi,Ujana,Umimi au...........

8 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Asante kwa kututakia mema.

Kuhusu swali lako ni gumu. Kabla sijatoa jibu pengine nami niulize (sina jibu!). Ulishawahi kujiuliza kwa undani kama pengine na nyie wanawake pia mnachangia kwa sisi akina baba kutelekeza familia. Mfano, kwa nini mumeo awe na nyumba ndogo? Kuna nini anachokipata kule nyumba ndogo ambacho kwako hakipo?

Hii ni siku yetu na kwa vile umeamua kutuchokoza nami nimeamua kuwatetea akina baba. Tuyatazame mambo katika usarafu wake (yaani pande zote mbili)....

Simon Kitururu said...

Akina BABA oyeeeeeee!

Halafu nikakaa na kufikiria na kujikuta sina uhakika na mshangilio hapo juu!:-(

Goodman Manyanya Phiri said...

Labda TZ mna bahati, lakini Afrika Kusini tunashuhudia watoto wachanga waliotupwa jalalani baada tu ya kuzliwa.


Mama gani hao wanaofanya hivyo?

Haya, nimesahau: lawama apewe mwanamme aliempa mimba mwanamke wa kutosa kitoto!!!


Kifupi, nakubaliana na MMN Mkuu: tuache lawama. Jamii zetu dhaifu. tufanye nini wanaume kwa wanawake ili tusaidiane kupata tiba.

Juzi tu nilisikia uchungu nusu kulia kuona mtoto wakike wenye miaka kama 6 hivi: MZURI LAKINI MCHAFU WA KUPINDUKIA TENA ANATEMBEA NUSU UCHI NA BARIDI LOTE LA SASA HIVI AFRIKA KUSINI.

Mtoto huyo analelewa na bibi yake (bila babu), kwani mama yake alikufa labda ukimwi labda nini hakika Mungu anajuwa! Cha mhimu mtoto huyo anahitaji malezi; tena ningekuwa na uwezo ningemchukua kama dada yake Tamara wangu wa miezi 8. Lakini lawama kwa ukweli haisaidii mtu! THE BLAME GAME IS A SHAME!

Goodman Manyanya Phiri said...

Nilisahau hapo juu kuomba msaada. Mababa wengine wanene!!!(LOL!!) Jamaani, nipendi dawa ya kunenepesha mtu. Mie nazidi kukauka tu!!! Au Unyasa umeniponza??!!!!

emu-three said...

Hongera siku ya Mababa,...kazi kubwa kweli kutimiza `ubaba' kwani lawama nyingi kwa baba..., lakini vyovyote iwavyo...HONGERA AKINA BABA DUNIANI KOTE!

Rachel Siwa said...

Ahsante sana wapendwa!

@kaka Matondo hahahahhha umeniua kwa kicheko.Duhhh swali juu ya swali, ni kweli kaka Matondo kunawakati na kina mama wanahusika, lakini nitaliweka ili wanawake wengine na kina baba wengine pamoja na wewe na mimi.Ili tujua tatizo kubwa ni nini.nimefurahi kukuona tena my kaka.

@kaka wa mimi Kitururu kwanini umejutia ushangiriaji wako?

Jamini inatia uchungu na simanzi kuona starehe ikijibu matunda yake ni mtoto asiye na hatia kuuliwa/kutelekezwa,@ kaka Manyanya hata bongo/TZ yapo hayo,Sijui nini kifanyike?.

Kuhusu unene kaka unaupendea nini mbona naona kama karaha?au unaona ukiwa mwembamba Heshima ya BABA haipo,yaani hutishi?kwikwikwi.Jamani eehhhhhh wa BABA msaidieni ndugu yetu afanyeje ili anenepe?

Ndugu yangu emu-3 ubaba nao unagharama yake au siyooooooooo!!.

Pamoja watu wangu!! hapa kila siku ni Siku muhimu kwa kina baba unaweza kuendelea kusheherekea nasi hata sasa hujachelewa!!!!!!!!!

Goodman Manyanya Phiri said...

Miaka minne iliepita niliwahi kuchumbia hapa kwetu baada ya kumuona mke wangu wa kwanza anakataa katakata kutoka Iringa na kuja kwangu. Adai sisi Wasoweto tunachinjana kama kuku na anaongopa kuja.


Haya basi nikakutana na mwanamama umri kama wa kwangu. Anamtoto mmoja; kabila lake kutoka Lesotho.

Nikachumbia kabisa na mambo ya kutoa mahali ya kamalizwa jinsi yatakavyofanyika.


Basi babamkwe akaanza mikwala. Akamwambia mwanae mbona mimi sio tumbotumbo kama kanali wote wa jeshi? Mbona mimi simnene? akamwuliza mwanae. Akaongezea kwa kusema labda nina ukimwi!!!!


Kwanzia hapo nikaona unene ni mali na natafuta mguu juu nipate nami jinsi ya kupata!

Rachel Siwa said...

Duhh kazi ipo mpaka uwe mnene ndiyo upose!!jamani Segito ameogopa kufa huko kwenu, hahahahaha. Pole kaka Manyanya kwa mikasa hiyo.