Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday 27 June 2012

SHEREHE YA SENDOFF YA DORIS KASAKA (KAPINGA) ILIVYOFANA USIKU WA JANA NDANI YA DELUXE HALL SINZA!!!!!!!!!!


Doris Kasaka (Kushoto) akiwa na mpambe wake jana ndani ya Deluxe Hall Sinza wakati wa sherehe ya kumuaga (Sendoff) na kumpongeza kwa kufanya maamuzi mazuri.

Mama Mkubwa wa Doris Mama Angelina Mwami akiwakaribisha wageni wakati wa sherehe ya Binti yake ndani ya ukumbi wa Deluxe Sinza.

Baba Mkubwa wa Doris Mzee Njelu Kasaka akiwakaribisha wageni katika sherehe ya kumuaga Binti yake ndani ya Ukumbi wa Deluxe Sinza jana usiku.

Meza kuu ya wazazi wa Doris kutoka kulia ni Mama Njelu Kasaka, Mzee Njelu Kasaka, Dr Mwami na mwisho kushoto ni Mama Mwami.
Doris akipiga picha ya kumbukumbu na wafanyakazi wenzake kutoka Zantel.


"Swahili na Waswahili" Tunakutakia Safari njema na kila lililo jema na Maandalizi mema ya Ndoa.


Pamoja sana KapingaZ!!!!!!!



Watoto na Malezi-Tatizo la Ndoa za Watoto;Pata Video!!!!!!!

Waungwana "WATOTO NA MALEZI".
Wazazi/Walezi leo Tuangalie NDOA ZA UTOTONI.


Kwanza nikuulize swali;Jee wewe ulilazimishwa kuolewa/Kuoa?jee Mume/Mke uliyenaye ni chaguo lako? .Jee wewe Umekeketwa?.


Sasa turudi kwa Watoto wetu ndugu zetu,wadogo zetu,Jee unafikiri kukeketwa kunawafaa?
Jee Unaushauri,Maoni,Ujumbe gani kwa Wazazi/Walezi na Jamii kwa ujumla kuhusina na Ndoa hizi za Watoto?.


Karibuni sana Tuelimishane kwa Upendo.
"SWAHILI na WASWAHILI" Pamoja sana.

Tuesday 26 June 2012

DORIS KASAKA (KAPINGA) AMEREMETA KWENYE KITCHEN PARTY YAKE ILIYOFANYIKA KWENYE UKUMBI WA TBS - UBUNGO !!!!!!


Doris akiwa katika pozi mwanana huku akiwaangalia wageni waalikwa waliokuja kumpongeza katika KITCHEN PARTY yake 
Doris akiwa mbele ya wageni waalikwa ukumbini kabla ya kuanza sherehe yake ya KITCHEN PARTY yake .

Mama Mkubwa wa Doris, Angelina Mwami (Kapinga) akiwakaribisha wageni waalikwa na kuwashukuru kwa kufika kwao kwenye sherehe ya KITCHEN PARTY ya Binti yake mpendwa.

Mama Mkubwa wa Doris kwa upande wa Baba, Mama Njelu Kasaka naye hakuwa nyuma kumpongeza binti yake na kuwakaribisha wageni waalikwa wote waliokuja kwenye sherehe ya KITCHEN PARTY.
Mama Mchungaji naye alifungua sherehe ya KITCHEN PARTY ya Doris kwa Sala nzuri na kukemea mapepo yote yenye nia mbaya "YASHINDWE NA YALEGEE"
KEKI YA AINA YAKE ILIYOANDALIWA KIUSTADI NA UTAALAM ALIYOANDALIWA DORIS.

Doris akikata Keki yake ya KITCHEN PARTY ikiwa ni ishara ya upendo kwa wageni wote walioshiriki katika sherehe hiyo na kula nao pamoja


Swahili NA Waswahili tunakutakia kila lililojema,Tunasubiri mnuso wa kuagwa na Ndoa.

Monday 25 June 2012

Da'Rahifah Jamaldin Atimiza Mwaka Mmoja!!!!!!!!!

Mwenyewe  da'Rahifah!!
Akitafakari aanzie wapi kuikata keki!!!
Dada na Kakazz, Wapambe muhimu
Hehehheeh!!! kweli kulea kazi, kaka mtu Bob Malikh yupo bithe kumtengeneza dada yake
Baharia Malikh ..Leo lazima kitakaa hiki, kinanichezea mie ?Dada naye katulia mpaka macho kafumba,utafanyaje na kaka kasema?Hahahahah watu wa Ilala mbona mtakatwa mitama mkimsogelea huyu binti,Chezeya wewe Mchezaji wa kulipwa wa BOMU..............

Baba na mwana,Pole da'Sulhiya[mama mtoto] yeye alikuwa mpiga picha siku hiyo,hatukupata picha yake.
Wakisikiliza Nasaha kutoka  kwa Wazazi  hahahaha
                                                         Dada Rahifah, Akiwashukuru Wazazi,Ndugu, Jamaa na Marafiki.


Da'Rahifah Tunakutakia kila lililojema,Baraka, Amani,Upendo na Makuzi mema.Uwe Baraka kwa Wazazi na Watu wote.
Hongereni sana Bibi na Bwana Jamal.M.Jamaldin[Minanasi].Kwakukuza, Mungu awape Hekima na Maarifa katika Malezi Yenu.


Swali la kizushi;Waungwana kuna aliye na picha za kutimiza mwaka  1-5?.
Au wewe Wazazi wako Hawakuweka Kumbukumbu,Hawakuwa na Tamaduni hizi za mambo ya siku kuu yako ya kuzaliwa?


"Swahili NA Waswahili" Karibuni Wooote!!!!!!

Sunday 24 June 2012

Nawatakia J'Pili Njema,Burudani-Rose Muhando: Pasipo Maono,Ndivyo Ulivyo na Woga wako....!!!!!!

Nawatakia J'Pili yenye Amani,Upendo na Baraka.
Maana ninyi,ndugu,mliitwa mpate uhuru;Kakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili,bali tumikianeni kwa Upendo.Neno la Leo;Wagalatia:5:13-26.

Mungu atubariki sote!!!!!!

Saturday 23 June 2012

Chaguo la Mswahili Leo;DDC Mlimani Park na Tancut Almasi!!!!!!!!!

Waungwana "CHAGUO LA MSWAHILI LEO"
Turudi Nyuma kidogo Tuangalie/Tusikilize Nyimbo hizi kutoka kwenye Bendi zetu..
Jee unauonaje Mziki wa Bendi za sasa na Zamani?
Karibuni sana katika Yote!!!!!
"Swahili NA Waswahili" Twende Soteeeeeee.