Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Sherehe Za Wa Afrika. Show all posts
Showing posts with label Sherehe Za Wa Afrika. Show all posts

Wednesday 2 April 2014

Wa Afrika Na Sherehe zao Leo Tupo ;RWANDA: TWIN BROTHERS MARRY TWIN SISTERS!!!!!!
Mwenzangu umeonaje hii Arusi?
Mimi nimeona kama hawana Furaha..sijui wamelazimishwa au Utiifu/Heshima...
Tunawatakia kila la kheri na Baraka.

Mengi sina karibu kwa Maoni Yako.

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Sana.

Friday 5 July 2013

Wa-Afrika na Sherehe zao;Zambian Kitchen Party!!!!!!!
Waungwana;Wa-Afrika na Sherehe zao..hii Kitchen Party ya Wa Zambia na wanaume walikuwepo....
za Waswahili/Tanzania nyingi wanaume hawaingizwi. Nilisikia Waziri Mkuu  Mizengo Pinda aliingia kwenye K/party ya mtoto wake..jee alikosea?
Unafikiri ni kwa nini wanaume hawaingii? kuna sababu za msingi au wanaonewa na kukosa UHONDO? 
 Jee Kichen Party zina faida kwenye maisha ya ndoa au nikutaka kukusanya Zawadi ,Kupata Nafasi ya Wanawake Kujimwaga peke yao au Kuna siri zao?
 Jee kwanini Wanaume hawafanyiwi Kitchen Party/Party za Kufundwa? Au wao wanajua kila kitu kabla ya ndoa?

Swali la Kizushi;Kwanini Wanawake wanapenda Party za Peke yao kuliko Wanaume?

 Karibuni wote kwa Maoni/Ushauri,Tujifunze pamoja na Kuelimishana kwa Upendo

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Sana.

Wednesday 8 May 2013

Wa-Afrika Na Sherehe Zao Leo;Kenya wedding!!!

Waungwana; Leo tupo Kenya na Shrehe zao za Arusi..nini kimekuvutia/kupenda na kipi kimechukiza/kutokipenda...

Ni Kweli Kwa Afrika Mashariki na Kati Kenya wanaongoza kwa uwandaaji wa Sherehe, Kuanzia Mapambo,Uvaaji,Burudani,picha na Yotemuhimu yahitajiwayo?

  Jee wewe unapicha,Video, za Arusi,Pati za jikoni,Kuagwa,Kipa imara na nyinginezo..za Miaka mitano Nyuma na kuendelea na ungependa kushiriki nasi?
 Unaweza kututumia ili tukumbuke/kumbushane ilikuwaje wakati huo au wewe ulivaaje/ulitokelezeaje na siku yako ilikuwaje.
  
Tuma kupitia Email;rasca@hotmail.co.uk


Nawe unayefunga Ndoa sasa usisite kututumia...Wewe unayetafuta Mwenza/Mchumba usikate  Tamaa..Mshirikishe MUNGU yupo nawe wala Hajakusahau/kukuacha.

     Swahili-Matukio/Events
          Pamoja Sana.

Thursday 15 November 2012

Wa-Afrika na Sherehe zao;Leo Ma-Arusi wa Leo wanavyo Jimwaga!!!!!

S n W
Waungwana; vipi Maarusi wa leo wanavyojimwaga/cheza,changamka? inapendeza au inachukiza? 

Ma-Arusi wa Leo wanafuraha sana na wanajimwaga vilivyo, yaani wanaonyesha furaha zao kabisa na ukichukulia siku kama hizi hazijirudii.
Unafikiri kwanini wanakuwa hivi jee, wamechaguana wenyewe,wanakwenda na wakati,hawana Aibu,wamengojea kwa muda mrefu kuwa MKE/MUME au............?

Vipi wa zamani ni kilio mtindo mmoja jee wengi wao wamelazishwa,Upweke wa kuwa mbali na familia,Furaha iliwazidi,Kutojuana/kuchaguliwa,wali-Olewa/Oa wakiwa wadogo  Au......?

"Swahili na Waswahili" Karibuni woooote!!!!!!

Tuesday 26 June 2012

DORIS KASAKA (KAPINGA) AMEREMETA KWENYE KITCHEN PARTY YAKE ILIYOFANYIKA KWENYE UKUMBI WA TBS - UBUNGO !!!!!!


Doris akiwa katika pozi mwanana huku akiwaangalia wageni waalikwa waliokuja kumpongeza katika KITCHEN PARTY yake 
Doris akiwa mbele ya wageni waalikwa ukumbini kabla ya kuanza sherehe yake ya KITCHEN PARTY yake .

Mama Mkubwa wa Doris, Angelina Mwami (Kapinga) akiwakaribisha wageni waalikwa na kuwashukuru kwa kufika kwao kwenye sherehe ya KITCHEN PARTY ya Binti yake mpendwa.

Mama Mkubwa wa Doris kwa upande wa Baba, Mama Njelu Kasaka naye hakuwa nyuma kumpongeza binti yake na kuwakaribisha wageni waalikwa wote waliokuja kwenye sherehe ya KITCHEN PARTY.
Mama Mchungaji naye alifungua sherehe ya KITCHEN PARTY ya Doris kwa Sala nzuri na kukemea mapepo yote yenye nia mbaya "YASHINDWE NA YALEGEE"
KEKI YA AINA YAKE ILIYOANDALIWA KIUSTADI NA UTAALAM ALIYOANDALIWA DORIS.

Doris akikata Keki yake ya KITCHEN PARTY ikiwa ni ishara ya upendo kwa wageni wote walioshiriki katika sherehe hiyo na kula nao pamoja


Swahili NA Waswahili tunakutakia kila lililojema,Tunasubiri mnuso wa kuagwa na Ndoa.

Monday 18 June 2012

Wa Afrika na Sherehe zao,LeoTupo Malawi ni-Kachitsa na Farayi;Tradditional Wedding!!!!


Mwenyewe bi Arusi Mtarajiwa,da'Farayi
Bwana Arusi Mtarajiwa kaka Willy Kachitsa,Huingii hapo mmpaka utoe pesa!!!
MmePendeza sana Wapendwa!!!!!
Mmmmhh Mapenzi Motomoto!!!!
Waungwana Leo Tupo Malawi, kaka KACHITSA na da'FARAYI wanatarajia kuwa mwili mmoja hivi karibuni.
Nasi tunawatakia kila lililojema katika maandalizi yao.Mungu asimamie kila hatua na Twasubiri kwa Hamu siku yenyewe!!!!!.

Waungwana; Sherehe hizi za WaAfrika zinafanana eehh? vipi kuhusu mambo ya kutoa pesa/Kufichua kabla ujaingia kwa wakwe na Mengine Meengi, Mila/Tamaduni za ndoa. zipi ninyi mnatumia/mlitumia?
 jee bado zina nguvu/Kufaa/Kufuatwa au mmezitupa?.

Jee wewe una Maoni ,Ushauri,gani kuhusu Tamaduni/Mila hizo nivyema kuzitunza na kuzifuata au Zimepitwa na Wakati?.

[To; Willy&farayi;May Good bless you!!!
We are still waiting for the big day!!
With Love From Isaac's Family.]


"SWAHILI na WASWAHLI"Pamoja sana!!!

Tuesday 29 May 2012

Wa Afrika na Sherehe zao;Leo ni Wadigo wedding , Kenya!!!!!!

Hahhahahhah Kadala,Mwanamke wa shoka, Mwanakwetu,Kadoda,Ndugu wa mimi na Waungwana Woooote,
Mambo hayo ya kupetipeti!!
Sina lazaidi Mengi Mnayo Wenyewe Yakheeeeee!!!!


Karibuni sana. "Swahili na Waswahili".Pamoja sana tuu.

Tuesday 22 May 2012

Wa Afrika na Sherehe Zao;Nigerian Bride (Traditional Wedding) and Gele Styles!!!!

Swali; Jee WaTanzania tunaweza kuvaa nini kwenye Ndoa,Siku ya Posa,Siku ya kuagwa, K/party au Sherehe yoyote inayotakiwa Kuonyesha Utanzania Wetu?

Nimeshaona wengi wakivaa kimasi, Jee Vazi hili linaweza kututambulisha?

Waungwana karibuni sana katika Kuelimishana,Kushauriana  na Mapenzi yako katika Vazi la Nyumbani.
Pamoja sana .Swahili na Waswahli!!!!!