Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday, 5 July 2013

Wa-Afrika na Sherehe zao;Zambian Kitchen Party!!!!!!!
Waungwana;Wa-Afrika na Sherehe zao..hii Kitchen Party ya Wa Zambia na wanaume walikuwepo....
za Waswahili/Tanzania nyingi wanaume hawaingizwi. Nilisikia Waziri Mkuu  Mizengo Pinda aliingia kwenye K/party ya mtoto wake..jee alikosea?
Unafikiri ni kwa nini wanaume hawaingii? kuna sababu za msingi au wanaonewa na kukosa UHONDO? 
 Jee Kichen Party zina faida kwenye maisha ya ndoa au nikutaka kukusanya Zawadi ,Kupata Nafasi ya Wanawake Kujimwaga peke yao au Kuna siri zao?
 Jee kwanini Wanaume hawafanyiwi Kitchen Party/Party za Kufundwa? Au wao wanajua kila kitu kabla ya ndoa?

Swali la Kizushi;Kwanini Wanawake wanapenda Party za Peke yao kuliko Wanaume?

 Karibuni wote kwa Maoni/Ushauri,Tujifunze pamoja na Kuelimishana kwa Upendo

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Sana.

2 comments:

emu-three said...

Ni muhimu sana kwa wanaume kuwepo, ili wote waelimike na hilo somo, cha muhimu, ni kuwa na muda muafaka wa kufundishana. Na somo la ndoa kabla ya ndoa ni kitu hakitiliwi maanani na watu wanaoana hawajui ni nini maana ya ndoa, matokea yake wanaishia kufarakana. Tupo pamoja ndugu wa mimi

Rachel Siwa said...

Asante sana ndugu wa mimi kwa mchango wako.