Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday 31 May 2018

Kikombe Cha Asubuhi ; 1Mambo ya Nyakati 16...




Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

haleluyah Mungu wetu yu mwema sana
Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu

Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni
Uabudiwe Jehovah,Uhimidiwe Yahweh,Matendo yako ni makuu mno,
Matendo yako ni ya ajabu,Matendo yako yanatisha
Hakuna kama wewe ee Mungu wetu,Neema yako yatutosha
Baba wa Mbinguni...!!




Sala ya nabii Habakuki: Ee Mwenyezi-Mungu, nimesikia juu ya fahari yako, juu ya matendo yako, nami naogopa. Uyafanye tena mambo hayo wakati wetu; uyafanye yajulikane wakati huu wetu. Ukasirikapo tafadhali ukumbuke huruma yako! Mungu amekuja kutoka Temani, Mungu mtakatifu kutoka mlima Parani. Utukufu wake umetanda pote mbinguni, nayo dunia imejaa sifa zake. Mng'ao wake ni kama wa jua; miali imetoka mkononi mwake ambamo nguvu yake yadhihirishwa. Maradhi yanatangulia mbele yake, nyuma yake yanafuata maafa. Akisimama dunia hutikisika; akiyatupia jicho mataifa, hayo hutetemeka. Milima ya milele inavunjwavunjwa, vilima vya kudumu vinadidimia; humo zimo njia zake za kale na kale.


Jehovah tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha
na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizo zifanya
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Usitutie majaribu Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona

Kwakupigwa kwake sisi tumepata kupona...




Niliwaona watu wa Kushani wakiteseka, na watu wa Midiani wakitetemeka. Ee Mwenyezi-Mungu, je, umeikasirikia mito? Je, umeyakasirikia maji ya bahari, hata ukaendesha farasi wako, na magari ya vita kupata ushindi? Uliuweka tayari uta wako, ukaweka mishale yako kwenye kamba. Uliipasua ardhi kwa mito. Milima ilikuona, ikanyauka; mafuriko ya maji yakapita humo. Vilindi vya bahari vilinguruma, na kurusha juu mawimbi yake. Jua na mwezi vilikaa kimya katika makazi yao, vilipoona miali ya mishale yako ikienda kasi, naam, vilipouona mkuki wako ukimetameta. Kwa ghadhabu ulipita juu ya nchi, uliyakanyaga mataifa kwa hasira yako. Ulitoka kwenda kuwaokoa watu wako, kumwokoa yule uliyemweka wakfu kwa mafuta. Ulimponda kiongozi wa jamii ya waovu, ukawaangamiza kabisa wafuasi wake.


Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji

Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni
ukatupe kama inavyokupendeza wewe....




Mungu wetu tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu wetu tunaomba ukatupe akili ya kutambua mema na mabayaBaba wa Mbinguni ukaonekane katika maisha yetu
Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi




Sala ya nabii Habakuki: Ee Mwenyezi-Mungu, nimesikia juu ya fahari yako, juu ya matendo yako, nami naogopa. Uyafanye tena mambo hayo wakati wetu; uyafanye yajulikane wakati huu wetu. Ukasirikapo tafadhali ukumbuke huruma yako! Mungu amekuja kutoka Temani, Mungu mtakatifu kutoka mlima Parani. Utukufu wake umetanda pote mbinguni, nayo dunia imejaa sifa zake. Mng'ao wake ni kama wa jua; miali imetoka mkononi mwake ambamo nguvu yake yadhihirishwa. Maradhi yanatangulia mbele yake, nyuma yake yanafuata maafa. Akisimama dunia hutikisika; akiyatupia jicho mataifa, hayo hutetemeka. Milima ya milele inavunjwavunjwa, vilima vya kudumu vinadidimia; humo zimo njia zake za kale na kale.


Mungu Baba tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu
wote wanaopotia magumu/majaribu mbalimbali
watoto wako wanaokuomba kwa bidii na imani
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
 kila mmoja na mahitaji yake 
Yahweh tunaomba ukaonekane katika maisha yao
Jehovah tunaomba ukawaokoe,ukawavushe salama na  kuwalinda
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe
Baba wa Mbinguni ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako
wakasimaie Neno lako nalo likaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kuomba kwetu
Baba wa Mbinguni ukapokee sala/maombi yetu
Mungu wetu ukawatendee  kama inavyokupendeza wewe
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina...!!

Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami
Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea 
kama inavyompendeza yeye....

Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na Upendo 
wa Mungu Baba ukae nanyi daima....
Nawapenda.




1Kisha waliliingiza sanduku la Mungu, na kuliweka ndani ya hema ambayo Daudi alikuwa ameitayarisha. Halafu wakatoa tambiko za kuteketezwa na za amani mbele ya Mungu. 2Daudi alipomaliza kutoa tambiko hizo za kuteketezwa na za amani, aliwabariki watu katika jina la Mwenyezi-Mungu, 3na akawagawia Waisraeli wote, wanaume kwa wanawake, kila mmoja akapewa mkate, kipande cha nyama na mkate wa zabibu.
4Zaidi ya hayo, Daudi aliwateua baadhi ya Walawi wawe wahudumu wa sanduku la Mwenyezi-Mungu, wamtukuze, wamtolee shukrani na wamsifu Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli. 5Alimchagua Asafu kuwa kiongozi wao, akisaidiwa na Zekaria. Yeieli, Shemiramothi, Yehieli, Metithia, Eliabu, Benaya, Obed-edomu na Yehieli, aliwachagua wawe wapiga vinanda na vinubi. Asafu alipiga matoazi, 6nao makuhani Benania na Yaharieli, walichaguliwa wawe wakipiga tarumbeta mfululizo mbele ya sanduku la agano la Mungu.
7Basi, hiyo ikawa siku ambayo kwa mara ya kwanza, Daudi alimpa Asafu na ndugu zake Walawi wajibu wa kumwimbia Mwenyezi-Mungu nyimbo za shukrani.

Wimbo wa Sifa

(Zab 105:1-15; 96:1-13; 106:47-48)

8Mpeni shukrani Mwenyezi-Mungu,
tangazeni ukuu wake,
yajulisheni mataifa mambo aliyoyatenda!
9Mshangilieni, mwimbieni Mungu sifa;
simulieni matendo yake ya ajabu!
10Jisifieni jina lake takatifu;
wenye kumcha Mwenyezi-Mungu na wafurahi.
11Mwendeeni Mwenyezi-Mungu mwenye nguvu;
mwendeeni Mwenyezi-Mungu daima.
12Kumbukeni matendo ya ajabu aliyotenda,
maajabu yake na hukumu alizotoa,
13enyi wazawa wa Abrahamu, mtumishi wake,
enyi wazawa wa Yakobo, wateule wake.
14Yeye Mwenyezi-Mungu, ndiye Mungu wetu;
hukumu zake zina nguvu duniani kote.
15Yeye hulishika agano lake milele,
hutimiza ahadi zake kwa vizazi elfu.
16Hushika agano alilofanya na Abrahamu,
na ahadi aliyomwapia Isaka.
17Alimthibitishia Yakobo ahadi yake,
akamhakikishia agano hilo la milele.
18Alisema: “Nitawapeni nchi ya Kanaani,
nayo itakuwa mali yenu wenyewe.”
19Idadi yenu ilikuwa ndogo,
mlikuwa wachache na wageni katika nchi ya Kanaani,
20mkitangatanga toka taifa hadi taifa,
kutoka nchi moja hadi nchi nyingine,
21Mungu hakumruhusu mtu yeyote awadhulumu;
kwa ajili yao aliwaonya wafalme:
22“Msiwaguse wateule wangu;
msiwadhuru manabii wangu!”
23Mwimbieni Mwenyezi-Mungu, ulimwengu wote.
Tangazeni kila siku matendo yake ya wokovu.
24Yatangazieni mataifa utukufu wake,
waambieni watu wote matendo yake ya ajabu.
25Maana Mwenyezi-Mungu ni mkuu, anasifika sana
anastahili kuheshimiwa kuliko miungu yote.
26Miungu yote ya mataifa mengine si kitu;
lakini Mwenyezi-Mungu aliziumba mbingu.
27Utukufu na fahari vyamzunguka,
nguvu na furaha vyajaza hekalu lake.
28Mpeni Mwenyezi-Mungu, heshima enyi jamii zote za watu,
naam, kirini utukufu na nguvu yake.
29Mpeni Mwenyezi-Mungu heshima ya utukufu wa jina lake;
leteni tambiko na kuingia nyumbani mwake.
Mwabuduni Mwenyezi-Mungu patakatifuni pake.16:29 patakatifuni pake: Au Kwa mavazi ya ibada; au anapotokea.
30Ee dunia yote; tetemeka mbele yake!
Ameuweka ulimwengu imara, hautatikisika.
31Furahini enyi mbingu na dunia!
Yaambieni mataifa, “Mwenyezi-Mungu anatawala!”
32Bahari na ivume, pamoja na vyote vilivyomo!
Furahini enyi mashamba na vyote vilivyomo!
33Ndipo miti yote msituni itaimba kwa furaha
mbele ya Mwenyezi-Mungu anayekuja
naam, anayekuja kuihukumu dunia.
34Mshukuruni Mwenyezi-Mungu kwa kuwa ni mwema,
kwa maana fadhili zake zadumu milele!
35Mwambieni Mwenyezi-Mungu:
Utuokoe, ee Mungu wa wokovu wetu,
utukusanye pamoja na kutuokoa kutoka kwa mataifa,
tupate kulisifu jina lako takatifu,
kuona fahari juu ya sifa zako.
36Asifiwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli,
tangu milele na hata milele!
Kisha watu wote wakasema, “Amina!” Pia wakamsifu Mwenyezi-Mungu.

Ibada huko Yerusalemu na Gibeoni

37Hivyo, mfalme Daudi akawaacha Asafu na nduguze Walawi mahali walipoliweka sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu, kwa ajili ya huduma zinazotakiwa mbele ya sanduku kila siku. 38Obed-edomu, mwana wa Yeduthuni, pamoja na wenzake sitini na wanane waliwasaidia. Obed-edomu mwana wa Yeduthuni na Hosa walikuwa walinzi wa malango. 39Mfalme Daudi akawaweka kuhani Sadoki na makuhani wenzake kuwa wahudumu wa hema ya Mwenyezi-Mungu iliyokuwa mahali pa kuabudu huko Gibeoni 40ili kutolea Mwenyezi-Mungu sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya sadaka za kuteketezwa daima asubuhi na jioni, kulingana na yote yaliyoandikwa katika sheria ya Mwenyezi-Mungu aliyowaamuru Waisraeli. 41Pamoja nao walikuwa Hemani na Yeduthuni na wale wote waliochaguliwa, waliotajwa majina yao, ili kumshukuru Mwenyezi-Mungu kwa kuwa fadhili zake ni za milele. 42Hemani na Yeduthuni walikuwa na tarumbeta na matoazi kwa ajili ya muziki na ala za muziki kwa ajili ya nyimbo takatifu. Wana wa Yeduthuni walichaguliwa kuyalinda malango. 43Kisha, kila mtu aliondoka kwenda nyumbani kwake; naye Daudi akaenda nyumbani kwake kuibariki jamaa yake.




1Mambo ya Nyakati16;1-43


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: