Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday 30 March 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Tuanze Kitabu Cha Kutoka 1...



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Tunamshukuru Mungu kwa Kutuwezesha kumaliza kitabu cha Mwanzo na Leo tunaanza kitabu cha "KUTOKA"
Nimatumaini yangu kuna mtu amaeguswa na amepata/amejifunza chochote katika mwendelezo wa kitabu cha Mwanzo..Mungu andelee kutuongoza na kutupa Neema ya kumtafuta yeye kwa bidii..Leo tunapoanza kitabu hiki Mungu akaonekane na kutupa shauku ya kusoma/kujifunza zaidi..Ninaimani kuna watu tutakuwa pamoja mpaka mwisho na hawatoondoka hivihivi pasipo na faida..Faida si kufanikiwa kipesa tuu..Hata kuongeza ufahamu na kujifunza zaidi,kutafakari Neno la Mungu na kumjua zaidi ni faida kubwa pia..
Karibu Mpendwa/Muungwana tuungane pamoja katika Kujifunza zaidi
yeye atutiaye nguvu nakutupa  Neema hii akatubariki na kutupa macho ya rohoni.Asanteni wote kwa kuwapamoja..
Injili na iende mbele..!!!

Tuombe..Mtakatifu Mtakatifu, Mtakatifu...!!Baba wa Mbinguni,Mungu wetu,Muumba wetu, Muumba Mbingu na Nchi na Vyote vilivyomo ni mali yako,Hata sisi Baba ni Mali yako..Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..
Baba wa Yatima,Mume wa wajane,Mungu usiye sinzia wala kulala,Mungu unayejibu,Wewe ni mwamzo na wewe ni Mwisho..
Asante kwa kutucghagua tena Baba umetupa Kibali cha kuiona tena Leo hii..Tazama Jana imepita Baba.. Leo ni siku mpya na Kesho ni siku nyingine Jehovah...!!!Tunajinyenyekeza na kujiachilia mikononi mwako Mfalme wa Amani..Tunakuja mbele zako Baba wa Mbinguni,Tunaomba Utubariki na kubariki siku hii na siku zote Yahweh..!!
Ikawe yenye Amani,Furaha,Upendo na tukakupendeze wewe..
Tulinde Tuingiapo/Tutokapo,Vyombo vya usafiri,Tutembeapo,Hatua zetu ziwe nawe Yahweh..Ukabariki Kazi zetu,Biashara,Masomo,Vilaji/Vinywaji Mfalme wa Mbinguni..Roho Mtakatifu akatuongoze kwenye Kunena na Kutenda,Kutambua/Kujitambua..Ukatufanye Chombo chako chema na tukatumike sawasawa na Mapenzi yako..
Ukabariki Ridhiki zetu ziingiazo na zitokazo..
Baba utusamehe pale tulipokwenda kinyume nawe,Nasi utupe Neema ya kuweza kusamehena..
Yahweh.. ukawaguse na kuwaponya wote wanaopitia Magumu/majaribu, Wagonjwa,Wafiwa ukawe mfariji wao, Wenye shida/Tabu, waliomagerezani pasipo na hatia Baba ukawaguse na haki ikatendeke...
Waliovifungoni mwa mwovu Baba ukawaponye na kuwaokoa..
Kwakuwa Ufalme ni Wako Nguvu na Utukufu Hata Milele...
Amina...!!!!
Tuanze na Bwana..Mungu wabariki sana.

Waisraeli wanateswa nchini Misri
1Haya ndiyo majina ya watoto wa kiume wa Israeli,1:1 Israeli: Jina jingine la Yakobo (taz Mwa 32:29) jina ambalo baadaye lilikuwa jina la wazawa wa Yakobo: Waisraeli. Linganisha 1:1-4 na Mwa 46:8-27. ambao walikwenda Misri, kila mmoja na jamaa yake: 2Reubeni, Simeoni, Lawi, Yuda, 3Isakari, Zebuluni, Benyamini, 4Dani, Naftali, Gadi na Asheri. 5Wazawa wote wa Yakobo walikuwa watu 70.1:5 sabini: Tafsiri ya Kigiriki: Sabini na watano; kadhalika na hati moja ya Kiebrania iliyopatikana kule Kumrani. Idadi hiyo pia yatajwa katika Mate 7:14 (taz pia Mwa 46:27). Wakati huo Yosefu alikuwa amekwisha tangulia kukaa huko Misri.
6Baadaye, Yosefu alifariki, hali kadhalika ndugu zake na kizazi kile chote. 7Taz Mate 7:14 Lakini wazawa wa Israeli waliongezeka sana, wakawa wengi na wenye nguvu mno, wakaenea kila mahali nchini Misri.
8Basi, akatokea mfalme mwingine1:8 mfalme mwingine: Huenda huyo alikuwa Farao Ramesesi II (1304-1238 Kabla ya Kristo). huko Misri ambaye hakumjua Yosefu. 9Naye akawaambia watu wake, “Tazameni jinsi Waisraeli walivyo wengi na wenye nguvu kuliko sisi. 10Ni lazima tutafute hila ya kuwapunguza na kuzuia wasiongezeke; la sivyo, kama vita vikitokea watajiunga na adui zetu na kuitoroka1:10 kuitoroka: Au Kuitawala. nchi.”
11Basi, Wamisri wakawateua wanyapara wawasimamie Waisraeli na kuwatesa kwa kazi ngumu. Waisraeli wakafanya kazi ya kumjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi. 12Lakini kadiri walivyoteswa ndivyo Waisraeli walivyozidi kuongezeka na kuenea nchini. Hivyo Wamisri wakawaogopa sana watu wa Israeli. 13Basi, Wamisri wakawatumikisha Waisraeli kikatili, 14wakayafanya maisha yao kuwa magumu kwa kazi ngumu ya kutengeneza chokaa na kufyatua matofali, na kazi zote za shambani. Katika kazi hizo zote, Waisraeli walitumikishwa kwa ukatili.
15Kisha, mfalme wa Misri akawaambia wakunga wa Misri, Shifra na Pua, ambao waliwahudumia wanawake wa Kiebrania, 16“Mnapowahudumia wanawake wa Kiebrania wanapojifungua, ikiwa mtoto anayezaliwa ni wa kiume, muueni. Lakini ikiwa ni wa kike, mwacheni aishi.” 17Lakini kwa kuwa wakunga hao walimcha Mungu, hawakufanya kama walivyoamriwa na mfalme wa Misri, bali waliwaacha watoto wa kiume wa Waisraeli waishi. 18Basi, mfalme wa Misri akawaita wakunga hao, akawauliza, “Kwa nini mmefanya hivyo? Mbona mmewaacha watoto wa kiume waishi?” 19Wao wakamjibu Farao, “Wanawake wa Kiebrania si sawa na wanawake wa Misri. Wao ni hodari; kabla mkunga hajafika, wao huwa wamekwisha jifungua.”
20Basi, Mungu akawajalia mema wakunga hao, nao Waisraeli wakazidi kuongezeka na kuwa na nguvu sana. 21Na kwa vile wakunga hao walimcha Mungu, Mungu akawajalia kupata jamaa zao wenyewe. 22Taz Mate 7:20; Ebr 11:23 Kisha Farao akawaamuru watu wake wote hivi, “Kila mtoto wa kiume atakayezaliwa kwa Waebrania mtupeni mtoni Nili. Lakini kila mtoto wa kike, mwacheni aishi
Kutoka1;1-22


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: