Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday 23 March 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mwanzo46...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Tuende Mbele za Mungu kwa Shukrani na Utukufu..
Mtakatifu,Mtakatifu, Mtakatifu Baba wa Mbinguni, Muumba wetu,Muumba Mbingu na Nchi, Baba yetu ,Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo, Yeye ni mwanzo na yeye ni mwisho,Hakuna wa kufanana naye..
Muweza wa Yote..Sifa na Utukufu ni kwako Daima..
Asante Baba kwa kutupa nafasi hii ya kuendelea kuiona leo hii..
Jana imepita Baba Leo ni siku mpya na kesho ni siku nyingine Mfalme wa Amani Tunaomba Utubariki katika Kazi zetu,Biashara,Masomo.Tuingiapo/Tutokapo,Vyombo vya usafiri na tutembeapo,Hatua zetu ziwe nawe Yahweh..!!
Roho Mtakatifu akatuongoze kwenye kunena/kutenda na maamuzi/kuamua Baba Ukabariki Vilaji/vinywaji na Ukavitakase na Damu ya Bwana wetu Mwokozi wetu Yesu Kristo vyote tunavyoenda kugusa/kutumia,ukatutakase Akili na Miili yetu Jehovah..
Utusamehe pale tulipoenda kinyume nawe Baba wa Mbinguni..
Nasi utupe Neema ya kuweza kusameheana Mfalme wa Mbingu..
Baba ukawaguse na kuwaponya wote wanaopitia Magumu/majaribu,Wenye Shida/Tabu, Wagonjwa,Wafiwa ukawe mfariji wao..Waliovifungoni Baba ukawaweke huru na kuwaokoa Baba..
Utupe Ridhiki zetu sawasawa na Mapenzi yako Baba wa Mbinguni Uzibariki ziingiapo/zitokapo...
Utukufu ni wako,Sifa na Fadhili zako zadumu Milele..

Tunajiachilia Mikononi Mwako Baba wa Mbinguni,Tukishukuru na Kuamini wewe ni Bwana na Mwokozi wetu..
Amina..!!!
Solomoni alipomaliza kusema sala hiyo yote na ombi lake kwa Mwenyezi-Mungu aliinuka kutoka pale mbele ya madhabahu ya Mwenyezi-Mungu, mahali alipokuwa amepiga magoti akiinua mikono yake juu. Alisimama, akawabariki Waisraeli wote waliokuwa wamekusanyika hapo, akisema kwa sauti kubwa, “Atukuzwe Mwenyezi-Mungu ambaye amewapatia starehe watu wake Israeli, kulingana na ahadi yake. Ametimiza ahadi zake zote njema alizozitoa kupitia kwa mtumishi wake Mose. Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, awe nasi, kama alivyokuwa na babu zetu; tunaomba asituache, wala asitutupe. Yeye aelekeze mioyo yetu kwake, ili tufuate njia zake, tukishika amri zake, maongozi yake na maagizo yake aliyowapa babu zetu. Basi, maneno yangu haya ambayo ni ombi langu mbele ya Mwenyezi-Mungu, yawe karibu na Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, mchana na usiku, naye amjalie mtumishi wake, na watu wake Israeli, ili wafanikiwe katika haja zao za kila siku. Nayo mataifa yote ulimwenguni yatajua kwamba kweli Mwenyezi-Mungu ndiye Mungu; wala hakuna mwingine. Nanyi, muwe waaminifu kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, mkifuata masharti yake na kutii amri zake zote kama mnavyofanya hivi leo.”
Mungu awabariki katika yote.


Yakobo anasafiri kwenda Misri


1Basi, Israeli akaanza safari yake pamoja na mali yake yote. Alipofika Beer-sheba, akamtolea tambiko Mungu wa Isaka, baba yake. 2Mungu akaongea na Israeli katika maono usiku, akamwita, “Yakobo! Yakobo!” Yakobo akaitika, “Naam nasikiliza.” 3Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu, Mungu wa baba yako. Usiogope kwenda Misri; utakapokuwa huko, nitakufanya uwe taifa kubwa. 4Mimi mwenyewe nitakwenda pamoja nawe huko Misri na kukurudisha huku. Utakapofariki, mkono wa Yosefu ndio utakaoyafumba macho yako.”
5Basi, Yakobo akaondoka Beer-sheba. Wanawe wakamchukua yeye, watoto wao wachanga pamoja na wake zao katika magari ambayo Farao alipeleka kumchukua. 6Walichukua pia mifugo na mali yao yote waliyokuwa wamechuma katika nchi ya Kanaani, wakaenda Misri. Yakobo aliwachukua wazawa wake wote: 7Wanawe, wajukuu wake wa kiume na wa kike, wote akawaleta Misri.
8Wazawa wa Israeli ambao walikwenda Misri pamoja naye walikuwa Reubeni, mzaliwa wake wa kwanza, 9pamoja na wana wa Reubeni: Henoki, Palu, Hesroni na Karmi. 10Simeoni na wanawe: Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Sohari na Shauli, aliyezaliwa na mwanamke Mkanaani. 11Lawi na wanawe: Gershoni, Kohathi na Merari. 12Yuda na wanawe: Eri, Onani, Shela, Peresi na Zera. (Lakini Eri na Onani walifariki katika nchi ya Kanaani). Wana wa Peresi walikuwa Hesroni na Hamuli. 13Isakari na wanawe: Tola, Puva, Yashubu46:13 Yashubu: Au Yobu. na Shimroni. 14Zebuluni na wanawe: Seredi, Eloni na Yaleeli. 15Hao ndio wana ambao Lea alimzalia Yakobo kule Padan-aramu, pamoja na Dina binti yake. Jumla ya wanawe, binti zake na wajukuu wake walikuwa watu thelathini na watatu.
16Gadi na wanawe: Sifioni, Hagi, Shuni, Esboni, Eri, Arodi na Areli. 17Asheri na wanawe: Imna, Ishva, Ishvi, Beria na Sera, dada yao. Beria na wanawe: Heberi na Malkieli. 18Hawa kumi na sita ni watoto na wajukuu wa Yakobo na Zilpa, mjakazi ambaye Labani alimpa Lea, binti yake.
19Raheli alimzalia Yakobo wana wawili: Yosefu na Benyamini. 20Huko Misri, Asenathi, binti Potifera, aliyekuwa kuhani wa mji wa Oni, alimzalia Yosefu wana wawili: Manase na Efraimu. 21Wana wa Benyamini walikuwa Bela, Bekeri, Ashbeli, Gera, Naamani, Ehi, Roshi, Mupimu, Hupimu na Ardi. 22Watu hao kumi na wanne ni watoto na wajukuu wa Yakobo na Raheli, mkewe.
23Dani na Hushimu, mwanawe. 24Naftali na wanawe: Yaseeli, Guni, Yeseri na Shilemu. 25Hao saba ni watoto na wajukuu wa Yakobo na Bilha, mjakazi ambaye Labani alimpa binti yake Raheli.
26Jumla ya wazawa wa Yakobo aliokwenda nao Misri, bila kuwahesabu wake za wanawe, ilikuwa watu sitini na sita. 27Huko nchini Misri Yosefu alikuwa amepata wana wawili. Kwa hiyo watu wote wa jamaa ya Yakobo walioingia Misri walikuwa sabini.

Yakobo anafika Misri

28Yakobo akamtanguliza Yu
da kwa Yosefu kumwomba waonane huko Gosheni; nao wakafika katika eneo la Gosheni. 29Yosefu akapanda gari lake la farasi, akaenda kumlaki Israeli, baba yake, huko Gosheni. Alipomfikia baba yake, alimkumbatia na kulia kwa kitambo kirefu. 30Israeli akamwambia Yosefu, “Hata nikifa sasa si kitu kwa kuwa nimeuona uso wako na kujua kwamba wewe u hai!” 31Yosefu akawaambia ndugu zake na jamaa yote ya baba yake, “Nakwenda kumwarifu Farao kwamba ndugu zangu na jamaa yote ya baba yangu waliokuwa katika nchi ya Kanaani wamekuja kwangu. 32Nitamweleza kwamba nyinyi ni wachungaji kwani mmekuwa mkichunga mifugo, na kwamba mmewasili pamoja na mbuzi, kondoo, ng'ombe na mali yenu yote. 33Basi, Farao akiwaita na kuwaulizeni, ‘Kazi yenu ni nini?’ 34Semeni: ‘Bwana, sisi watumishi wako, ni wafugaji wa mifugo tangu utoto wetu mpaka leo, kwani ndivyo walivyokuwa babu zetu’; semeni hivyo ili mruhusiwe kukaa katika eneo la Gosheni.” Yosefu alisema hivyo kwa sababu kwa Wamisri wachungaji wote wa kondoo ni chukizo.
Mwanzo46;1-34

Bible Society of Tanzania

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: