Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 3 May 2015

Natumai Jumapili Inaendele Vyema;Burudani-Freedom-Eddie James,Worshiping You - Deluge,Phil Wickham - At Your Name...


Wapendwa;Natumaini Jumapili inaendelea vyema,Iwe yenye Imani,Tumaini,Uponyaji,Faraja,
Shukrani na Utukufu tumrudishie MUNGU....

At Your name, the mountains shake and crumble At Your name, the oceans roar and tumble At Your name, angels will bow, the earth will rejoice Your people cry out Lord of all the earth We shout Your name, shout Your name Filling up the skies With endless praise, endless praise Yahweh, Yahweh We love to shout Your name, oh Lord
1 Mpeni Mwenyezi-Mungu heshima enyi viumbe vya mbinguni,
semeni Mwenyezi-Mungu ni mtukufu na mwenye nguvu.
2Semeni jina la Mwenyezi-Mungu ni tukufu.
Mwabuduni katika mahali pake patakatifu.

Neno La Leo Zaburi 29;1-11
Sauti ya Mungu katika dhoruba
(Zaburi ya Daudi)

3Sauti ya Mwenyezi-Mungu yasikika juu ya maji;
Mungu mtukufu angurumisha radi,
sauti ya Mwenyezi-Mungu yasikika juu ya bahari!
4Sauti ya Mwenyezi-Mungu ina nguvu,
sauti ya Mwenyezi-Mungu imejaa fahari.
5Sauti ya Mwenyezi-Mungu huvunja mierezi;
Mwenyezi-Mungu avunja mierezi ya Lebanoni.
6Huirusha milima ya Lebanoni kama ndama,
milima ya Sirioni kama mwananyati.
7Sauti ya Mwenyezi-Mungu hutoa miali ya moto.
8Sauti ya Mwenyezi-Mungu hutetemesha jangwa,
Mwenyezi-Mungu hutetemesha jangwa la Kadeshi.
9Sauti ya Mwenyezi-Mungu huitikisa mivule,
hukwanyua majani ya miti msituni,
na hekaluni mwake wote wasema:
“Utukufu kwa Mungu!”

10Mwenyezi-Mungu ameketi juu ya gharika;
Mwenyezi-Mungu ni mfalme atawalaye milele.
11Mwenyezi-Mungu na awape watu wake nguvu!
Mwenyezi-Mungu na awabariki watu wake kwa amani!
            Bible Society of Tanzania








"Swahili Na Waswahili"Muwe na Wakati Mwema.

Wednesday 29 April 2015

RAIS KIKWETE KATIKA MAZIKO YA LUTENI KANALI Mst KITENGA MOROGORO




Shukrani;ikulu mawasiliano


"Swahili Na Waswahili"Inawapa Pole Ndugu,Jamaa na Marafiki.

Makala ya JK katika ibada ya kusimikwa Askofu jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu




Shukrani;ikulu mawasiliano


"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

BALOZI WA UMOJA WA AFRIKA AMINA SALUM ALI ATOA RAMBI RAMBI KWA KIFO CHA BRIGEDIA JENERALI HASHIM MBITA


Balozi Amina Salum Ali

Na mwandishi wako, Washington, DC

Balozi wa kudumu wa Umoja wa Afrika, Mhe. Amina Salum Ali leo ametoa salamu za rambi rambi kwa Brigedia Jenerali mstaafu Hashim Mbita aliyefariki siku ya siku ya Jumapili April 26, 2015 asubuhi na kuzikwa siku ya Jumanne April 28, 2015 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.



Balozi Amina Salum Ali alisema amepokea kwa majonzi na simanzi kubwa taarifa za kifo cha mmoja wa watumishi wa miaka mingi wa Serikali, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TPDF), aliendelea kwa kusema Brigedia Jenerali msataafu Hashim Mbita atakumbukwa Tanzania, bara nzima la Afrika na dunia kwa jumla kama mmoja wa makamanda mahiri aliyeshiriki kikamilifu katika uondoshaji wa utawala wa ukoloni barani Afrika, hususan utawala wa kidhalimu wa makaburu Zimbabwe na Afrika ya Kusini na hatimaye kuachiwa huru kwa aliyekuwa Rais mzawa wa kwanza nchini Afrika Kusini, hayati Nelson Mandela.



Mzee Mbita alijitoa mhanga kuongoza mapambano ya ukombozi wa Afrika, Atakumbukwa milele kwa kurudisha heshima ya Muafrika.


Brigedia Jenerali msataafu Hashim Mbita ni mfano uliotukuka kwa watanzania na Afrika.Aliiongoza vizuri sana kamati ya ukombozi ya Umoja wa Afrika Mungu amlaze pema peponi, Amin.


Balozi Amina Salum Ali yupo safarini kuelekea Tanzania.

Monday 27 April 2015

Mahojiano na mbunifu mavazi Linda Bezuidenhout (LB) Pt II


Karibu katika sehemu ya pili na ya mwisho ya mahojiano na mbunifu wa kimataifa wa mitindo mwenye asili ya Tanzania, Linda Bezuidenhout

 Ameeleza mengi kuhusu kazi yake na familia kwa ujumla.

Anavyokabiliana na kazi zake, changamoto za afanyalo, tuzo alizopata nk

Na pia, kaeleza kuhusu mtazamo wake juu ya waTanzania (hasa wa Diaspora) na ushauri kwa kinamama wote

KARIBU

Sunday 26 April 2015

Tumalizie Jumapili hii kwa Furaha na Baraka..Burudani;Rebecca Magamba Na Sarah K.....



Wapendwa; Natumai Jumapili Imeisha/Inaendelea vyema...
Mungu Baba azidi kuwalinda na kuwatendea,,Furaha,Amani,Tumaini,Vitawale Nyumbani mwenu..
1Nyinyi mlikuwa mmekufa kwa sababu ya makosa na dhambi zenu. 2Wakati ule mliishi kufuatana na mtindo mbaya wa ulimwengu huu, mkawa mnamtii mtawala wa pepo wenye nguvu wa anga, pepo ambao huwatawala sasa watu wasiomtii Mungu. 3Na hata sisi sote tulikuwa kama wao; tuliishi kufuatana na tamaa zetu za kidunia na kufanya tu mambo yale yaliyoipendeza miili na akili zetu. Kidunia, sisi kama vile pia wao, tulistahili ghadhabu ya Mungu. 4Lakini Mungu ni mwenye huruma nyingi. Alitupenda kwa mapendo yasiyopimika, 5hata, ingawa tulikuwa tumekufa kwa sababu ya dhambi, alitufanya hai pamoja na Kristo. Kwa neema ya Mungu nyinyi mmeokolewa.

 6Kwa kuungana na Kristo Yesu, Mungu alitufufua pamoja naye, tukatawale pamoja naye mbinguni. 7Ndivyo alivyopenda kuonesha kwa watu wa nyakati za baadaye ukuu wa neema yake aliyotujalia kwa ukarimu katika kuungana kwetu na Kristo Yesu. 8Maana, kwa neema ya Mungu mmekombolewa kwa njia ya imani. Jambo hili si matokeo ya juhudi zenu, bali ni zawadi ya Mungu. 9Wala halitokani na matendo yenu wenyewe, asije mtu akajivunia kitu. 10Sisi ni viumbe vyake Mungu, na kwa kuungana na Kristo Yesu, alituumba kwa ajili ya kuishi maisha ya matendo mema aliyotutayarishia tuyatende.

11Nyinyi mlio kwa asili watu wa mataifa mengine – mnaoitwa, “Wasiotahiriwa” na Wayahudi ambao hujiita, “Waliotahiriwa,” (kwa sababu ya kile wanachoifanyia miili yao) – kumbukeni mlivyokuwa zamani. 12Wakati ule nyinyi mlikuwa bila Kristo; mlikuwa nje ya jamii ya Israeli; mlikuwa wageni na hamkuwa na sehemu katika yale maagano aliyoahidi Mungu. Mlikuwa bila matumaini na kama watu wasiomjua Mungu hapa duniani. 13Lakini sasa, kwa kuungana na Kristo Yesu, nyinyi ambao hapo awali mlikuwa mbali, mmekaribishwa kwa njia ya damu yake Kristo. 14Maana Kristo mwenyewe ametuletea amani kwa kuwafanya Wayahudi na watu wa mataifa mengine kuwa jamii moja. Kwa mwili wake yeye mwenyewe aliubomoa ule ukuta uliowatenganisha na kuwafanya maadui. 15Aliiondoa ile sheria pamoja na amri zake na kanuni zake, ili kutokana na jamii hizo mbili aumbe jamii moja mpya katika umoja naye na hivyo kuleta amani. 16Kwa mwili wake, Kristo aliuangamiza uadui wao; kwa msalaba wake aliziunganisha jamii hizo kuwa moja na kuzipatanisha na Mungu.
Neno La Leo;Waefeso 2: 1-22
Kutoka kifo na kuingia katika uhai
Umoja katika Kristo


17Basi, Kristo alikuja akahubiri Habari Njema ya amani kwenu nyinyi watu wa mataifa mengine mliokuwa mbali na Mungu, na pia kwa Wayahudi ambao walikuwa karibu na Mungu. 18Hivyo, kwa njia yake, sisi sote, Wayahudi na watu wa mataifa mengine, tunaweza kumwendea Baba kwa Roho mmoja. 19Basi, nyinyi si wageni tena, wala si watu wa nje. Nyinyi ni raia pamoja na watu wa Mungu, na ni watu wa jamaa ya Mungu. 20Mmejengwa juu ya msingi uliowekwa na mitume na manabii, naye Kristo mwenyewe ndiye jiwe kuu la msingi. 21Yeye ndiye mwenye kuliunganisha jengo lote na kulikuza hata liwe hekalu takatifu kwa ajili ya Bwana. 22Katika kuungana naye, nyinyi pia mnajengwa pamoja na wote wengine, muwe makao ya Mungu kwa njia ya Roho wake.
Bible Society of Tanzania









"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Mno.