Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Msiba/Maombelezo. Show all posts
Showing posts with label Msiba/Maombelezo. Show all posts

Sunday, 23 September 2018

Nawatakia Jumapili Njema;Neno la Faraja kwa Ajali ya Mv Nyerere,Fanuel Sedekia-Tuonane Bandari- Yupo Mfariji Omba," Nani Kama Wewe "


Wapendwa/Waungwana;Niungane na Familia,Ndugu,Jamaa na Wa Tanzania wote
katika wakati huu mgumu kwetu wa Ajali ya Mv Nyerere...
Mungu akawafariji wafiwa  wote na akawape uvumilivu na imani...
Mungu akawaguse kwa mkono wake wenye nguvu na wakapate kupona 
haraka wale wanaondelea na Matibabu....
 waliopatikana wakiwa Hai na kuendelea vyema Mungu aendelee kuwalinda
na wakapate nafasi ya kushukuru na kutafakari mapito haya....
Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Afrika,Mungu  akatubariki popote tulipo
na akabariki Nchi na mahali tulipo....
Amina.


Neno La Leo;1Wathesalonike 4:13-18 na
 1Wathesalonike5:1-11Bwana anakuja
13Ndugu, twataka mjue ukweli kuhusu wale ambao wamekwisha fariki dunia, ili msipatwe na huzuni kama watu wengine wasio na matumaini. 14Sisi tunaamini kwamba Yesu alikufa, akafufuka; na hivyo sisi tunaamini kwamba Mungu atawaleta pamoja na Yesu wale wote waliofariki wakiwa wanamwamini.
15Hili tunalowaambieni ni fundisho la Bwana, kwamba sisi tulio hai, ambao tutakuwa tumebaki wakati Bwana atakapokuja, hakika hatutawatangulia wale waliokwisha fariki dunia. 16Maana patatolewa amri, sauti ya malaika mkuu, sauti ya tarumbeta ya Mungu, naye Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni. Ndipo wale waliokufa wakiwa wanamwamini Kristo watafufuliwa kwanza. 17Kisha sisi tulio hai wakati huo tutakusanywa pamoja nao katika mawingu kumlaki Bwana hewani. Na hivyo tutakuwa daima pamoja na Bwana. 18Basi, farijianeni kwa maneno haya.
Muwe tayari kwa siku ya Bwana
1Ndugu, hakuna haja ya kuwaandikieni juu ya nyakati na majira ya mambo haya yatakapotukia. 2Maana nyinyi wenyewe mwajua kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwizi ajavyo usiku. 3Watu watakapokuwa wanasema: “Kila kitu ni shwari na salama”, ndipo uharibifu utakapowaangukia ghafla! Mambo hayo yatatukia ghafla kama uchungu wa uzazi unavyomjia mama anayejifungua, wala watu hawataweza kuepukana nayo. 4Lakini nyinyi, ndugu, hamko gizani, na siku hiyo haipaswi kuwajieni ghafla kama vile mwizi. 5Nyinyi nyote ni watu mnaoishi katika mwanga, watu wa mchana. Sisi si watu wa usiku, wala wa giza. 6Basi, tusilale usingizi kama wengine; tunapaswa kukesha na kuwa na kiasi. 7Wanaolala hulala usiku, na walevi hulewa usiku. 8Lakini sisi ni watu wa mchana na tunapaswa kuwa na kiasi. Tunapaswa kuvaa imani na upendo kama vazi la kujikinga kifuani, na tumaini letu la wokovu kama kofia ya chuma. 9Maana Mungu hakututeua ili tuangamizwe na ghadhabu yake, bali tuupate wokovu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo 10ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, iwe tu hai au tumekufa. 11Kwa hiyo farijianeni na kusaidiana nyinyi kwa nyinyi, kama mnavyofanya sasa.
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.Thursday, 13 July 2017

Msiba Wa Mtanzania Prof Henslay Kabisama Nchini MarekaniWaTanzania nchini Marekani wanaomboleza msiba wa Profesa Henslay Kabisama aliyefariki huko California mwishoni mwa mwezi June
Mjane wa Marehemu pamoja na wadau kadhaa waliungana na Mubelwa Bandio katika kipindi cha NJE-NDANI kuongelea mipango ya mazishi ilipofikia sasa.

Unaweza kushiriki kusaidia gharama za kuusafirisha mwili kupitia akaunti HII ya GoFundME

Karibu uwasikilize


Monday, 8 May 2017

Neno la Faraja;Mungu atupe uvumilivu Ndugu/Familia yangu kwa kuondokewa na Ndugu yetu Christopher-Hamisi Mbegete na Watanzania kwa kuondokewa na Watoto wetu wanafunzi wa Lucky Vicent..

Pichani ni ndugu yetu,Kaka na Mpendwa wetu Christopher-Hamisi Mbegete
Naungana na Ndugu/ familia yangu huko nyumbani kwa wakati huu mgumu sana kwa kuondokewa na mpenzi ndugu yetu..
Daima tutakukumbuka, Sina Neno zuri  la kuweza kusema zaidi ya kumshukuru Mungu kwa maisha yako na kuwa nasi na sasa umetangulia..Mungu akatupe faraja na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu..Mungu akawasimamie na kuwaongoza  wote wanaoshiriki katika maandalizi ya kuulaza mwili wako.Na akawabariki na kuwaongezea zaidi ya walipojitoa, kwa Muda, Faraja na yote..
Ulale kwa Amani.


Niungane na familia, wanafunzi /walimu  na Watanzania wenzangu huko nyumbani na popote walipo kwa wakati huu mgumu kwenye Taifa letu
kwakuondokewa na watoto wetu,wadogo zetu wapendwa wetu Walimu na Wafanya kazi..
Mungu Baba akawape nguvu na uvumilivu kwa wakati huu mgumu,Poleni sana wazazi/ndugu na Watanzania..
Mungu akawafariji na kuwaongoza katika yote.
Mlale kwa Amani malaika  wetu,watoto wetu wapendwa..
ni kipindi kigumu sana lakini tumshukuru Mungu katika yote..


Shukrani kwa Mungu
3Atukuzwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba mwenye huruma na Mungu mwenye kuleta faraja yote. 4Yeye hutufariji sisi katika taabu zetu zote, ili nasi tupate kuwafariji wengine katika kila taabu kwa faraja hiyohiyo tunayopokea kutoka kwa Mungu. 5Naam, kadiri mateso ya Kristo yanavyozidi ndani yetu, ni kadiri hiyohiyo tunazidi kufarijiwa naye. 6Ikiwa tunapata taabu, basi ni kwa ajili ya faraja na wokovu wenu. Tukifarijika, ni kwa ajili ya kuwafariji nyinyi na kuwaunga mkono mpate nguvu ya kustahimili mateso yaleyale tunayoteseka sisi. 7Tena, matumaini tuliyo nayo kwa ajili yenu ni imara; tunajua kwamba mkishiriki mateso yetu, mtashiriki pia faraja yetu.[2wakorintho 1;3-7]


Bwana anakuja
13Ndugu, twataka mjue ukweli kuhusu wale ambao wamekwisha fariki dunia, ili msipatwe na huzuni kama watu wengine wasio na matumaini. 14Sisi tunaamini kwamba Yesu alikufa, akafufuka; na hivyo sisi tunaamini kwamba Mungu atawaleta pamoja na Yesu wale wote waliofariki wakiwa wanamwamini.
15Hili tunalowaambieni ni fundisho la Bwana, kwamba sisi tulio hai, ambao tutakuwa tumebaki wakati Bwana atakapokuja, hakika hatutawatangulia wale waliokwisha fariki dunia. 16Maana patatolewa amri, sauti ya malaika mkuu, sauti ya tarumbeta ya Mungu, naye Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni. Ndipo wale waliokufa wakiwa wanamwamini Kristo watafufuliwa kwanza. 17Kisha sisi tulio hai wakati huo tutakusanywa pamoja nao katika mawingu kumlaki Bwana hewani. Na hivyo tutakuwa daima pamoja na Bwana. 18Basi, farijianeni kwa maneno haya.[1Wathesalonike 4;13-18]


Wapendwa/Waungwana leo tuungane na wenzetu katika kuombeleza Msiba huu..
Mniwie Radhi kesho kwa Neema ya Mungu tutaendelea.
Muwe na wakati mwema na msisahau kuwaweka katika maombi/sala/dua wote wanaopitia mapito haya.

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe sana.

Tuesday, 6 December 2016

TANZIA: MAREHEMU FELIX KAPINGA ATAZIKWA LEO TAREHE 06/12/2016 MKOANI NJOMBE


Marehemu Felix Kapinga enzi za uhai wake. 

Wanajumuia ya wanafunzi waliosoma Tumaini University - Iringa, Songea Boys High School na Lugalo Secondary School wanasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa mwanafunzi mwenzao Marehemu Felix Kapinga kilichotokea Usiku wa Tarehe 3/12/2016 katika Hospitali ya Ikonda Mission Mkoa wa Njombe baada ya kuugua kwa muda mfupi. 
Tunachukua fursa hii kutoa pole kwa Mke wa marehemu, Mtoto wa marehemu, Mama mzazi wa marehemu, wafanyakazi wenzake kutoka Njombe community Bank, Ndugu, jamaa, Marafiki na wana familia kiujumla kwa msiba huu walioupata, tunaungana nao katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. 

Mazishi yanatarajiwa kufanyika leo tarehe 06/12/2016 huko huko Njombe katika eneo la kijiji kinachotambulika kwa jina la Ramadhani  ambako Mama mzazi wa marehemu ndiko anakoishi, shighuli za Mazishi zinategemewa kufanyika kuanzia saa 6.00 Mchana. Kwa taarifa zaidi unaweza ukawasiliana kwa namba 
+255 713 254553

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE
AMIN.

Friday, 6 December 2013

Dunia yaomboleza kifo cha Mandela;Tanzania imetangaza siku tatu za maombolezo.

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela
Tanzania imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia tarehe 6 hadi 8 Desemba, 2013, kufuatia kifo cha rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.
Rais Jakaya Kikwete wa nchi hiyo pia ameagiza kuwa katika kipindi hicho cha siku tatu bendera zote zitapepea nusu mlingoti.
Kufuatia kifo hicho Rais Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini na kupitia kwake kwa mkewe Bi Graca Machel, wanafamilia wote na wananchi wote wa Afrika ya Kusini kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela kilichotokea tarehe 5 Desemba, 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Rais ameuelezea msiba huu kuwa ni msiba mkubwa kwetu sote.
"Afrika ya Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na shujaa mkubwa wa Karne ya 20 na 21.Tunaelewa machungu waliyonayo wananchi wa Afrika ya Kusini kwa kupoteza kiongozi shupavu, jasiri, mwana mapinduzi , mvumilivu na mstahimilivu". Ameongeza Rais Kikwete.
Rais amemuelezea Mzee Mandela kuwa ni kielelezo cha aina yake kwa wanadamu kwa moyo wake wa kusamehe, huruma na upendo uliomwezesha kuwaunganisha wananchi wa Afrika ya Kusini kuwa taifa moja baada ya kipindi kirefu cha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.
"Mandela ni mfano bora kwa wanadamu wa jinsi binadamu muungwana anavyopaswa kuwa . Ni wajibu wa wana Afrika Kusini, Afrika na dunia kuiga mfano wake hasa moyo wake wa uzalendo, kujitolea hata maisha yake kwa ajili yake na wananchi wenzake". Rais ameongeza kusema, "Tuzidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mzee Mandela mahali pema peponi".
Mandela amefariki huko Johannesburg akiwa na umri wa miaka 95 na yeye ndiye aliyeiongoza Afrika Kusini kutoka mikononi mwa watawala wa ubaguzi wa rangi baada ya kufungwa jela kwa miaka 27.
Mandela alikuwa anatibiwa homa ya mapafu nyumbani kwake baada ya kulazwa hospitalini kwa miezi mitatu.
Katika taarifa yake kwa watu wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, alisema kuwa Mandela amewaaga lakini yuko mahali salama.
Rais Zuma amesema kuwa taifa limepoteza mtu waliyemjua kama mtoto wa taifa hilo.
Mandela aliwahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel, na kutambulika kama rais aliyeheshimika sana hasa kwa kupatanisha watu wa Afrika Kusini baada ya kutoka gerezani.

Habari Na;http://www.bbc.co.uk/swahili/