Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday 18 May 2015

Ana kwa Ana na Nape Nnauye Pt I


Karibu kwenye sehemu ya kwanza kati ya mbili za mahojiano yetu na Katibu Uenezi na Itikadi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania.
Ameeleza mengi akianza na Hali ya chama hivi sasa.
KARIBU

Sunday 17 May 2015

Natumaini Jumapili Inaendelea Vyema;Iwe yenye Baraka Na Fanaka,Burudani- Jamaican Gospel Mix....


Natumaini Jumapili inaendelea Vyema,Iwe yenye Hekima,Busara,Heri,Fanaka,Utii,Uaminifu,
Imani na Matumaini...Utukufu tumrudishie Mungu...!!!



1Mwanangu, usiyasahau mafundisho yangu,
bali kwa moyo wako uzishike amri zangu.
2Maana yatakupa wingi wa siku,
maisha marefu na fanaka kwa wingi.
3Utii na uaminifu visitengane nawe.
Vifunge shingoni mwako;
viandike moyoni mwako.


Neno La Leo;Methali 3:1-35

Mawaidha kwa vijana

4 Hivyo utakubalika na kusifika,
mbele ya Mungu na mbele ya wanadamu.
5Mtumaini Mwenyezi-Mungu kwa moyo wako wote,
wala usitegemee akili zako mwenyewe.
6Umtambue Mungu katika kila ufanyalo,
naye atazinyosha njia zako.
7 Usijione wewe mwenyewe kuwa mwenye hekima;
mche Mwenyezi-Mungu na kujiepusha na uovu.
8Hiyo itakuwa dawa mwilini mwako,
na kiburudisho mifupani mwako.
9Mheshimu Mwenyezi-Mungu kwa mali yako,
na kwa malimbuko ya mazao yako yote.
10Hapo ghala zako zitajaa nafaka,
na mapipa yako yatafurika divai mpya.
11 Mwanangu, usidharau adhabu ya Mwenyezi-Mungu,
wala usiudhike kwa maonyo yake;
12 maana Mwenyezi-Mungu humwonya yule ampendaye,
kama baba amwonyavyo mwanawe mpenzi.
13Heri mtu anayegundua hekima,
mtu yule anayepata ufahamu.
14Hekima ni bora kuliko fedha,
ina faida kuliko dhahabu.
15Hekima ina thamani kuliko johari,
hamna unachotamani kiwezacho kulingana nayo.
16Kwa mkono wake wa kulia Hekima atakupa maisha marefu;
kwa mkono wake wa kushoto atakupa mali na heshima.
17Njia zake ni za kupendeza,
zote zaelekea kwenye amani.
18Hekima ni mti wa uhai kwa wote wampatao;
wana heri wote wanaoshikamana naye.
19Kwa hekima Mwenyezi-Mungu aliweka misingi ya dunia,
kwa akili aliziimarisha mbingu.
20Kwa maarifa yake vilindi vilipasuka,
na mawingu yakadondosha umande.

21Mwanangu, zingatia hekima safi na busara;
usiviache vitoweke machoni pako,
22navyo vitakuwa uhai nafsini mwako,
na pambo zuri shingoni mwako.
23Hapo utaweza kwenda zako kwa usalama,
wala mguu wako hautajikwaa.



24Ukiketi hutakuwa na hofu;
ukilala utapata usingizi mtamu.
25Usiogope juu ya tishio la ghafla,
wala shambulio kutoka kwa waovu,
26Maana Mwenyezi-Mungu ndiye atakayekutegemeza;
atakuepusha usije ukanaswa mtegoni.
27Usimnyime mtu anayehitaji msaada,
ikiwa unao uwezo wa kufanya hivyo.
28Usimwambie jirani yako aende zake hadi kesho,
hali wewe waweza kumpa anachohitaji leo.
29Usipange maovu dhidi ya jirani yako,
anayeishi karibu nawe bila wasiwasi.
30Usigombane na mtu bila sababu
ikiwa hajakudhuru kwa lolote.
31Usimwonee wivu mtu mkatili,
wala usiige mwenendo wake.
32Maana waovu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu;
lakini yeye huwafanya marafiki zake wale walio wanyofu.
33Mwenyezi-Mungu huapiza nyumba za waovu,
lakini huyabariki makao ya waadilifu.
34 Yeye huwadharau wenye dharau,
lakini huwafadhili wanyenyekevu.
35Wenye hekima watavuna heshima,
lakini wapumbavu watapata fedheha.
Bible Society of Tanzania




"Swahili Na Waswahili" Mbarikiwe Sana.

Thursday 14 May 2015

Balozi mpya wa Malawi nchini Marekani atembelea Ubalozi wa Tanzania Washington DC


 Mhe balozi mpya wa Malawi Nector Mhura akipokelewa na Afisa ubalozi Swahiba Mndeme alipotembelea ubalozi.
 Mhe, balozi Liberata Mulamula kwenye picha ya pamoja na mgeni wake balozi wa Malawi Nector Mhura.
 Mhe, balozi wa Malawi nchini Marekani akiweka saini kwenye kitabu maalum cha wageni.
 Mhe, balozi wa Malawi nchini Marekani Nector Mhura akimsikiliza kwa makini mwenyeji wake balozi Liberata Mulamula alipokua akijitambulisha.
  Mhe, balozi wa Malawi nchini Marekani Nector Mhura akiwa ameambata na mkuu wa utawala wa ubalozi wa Malawi bi, Jane Nankwenya.
 Mhe, balozi wa Malawi nchini Marekani Nector Mhura akiwa ameambata na mkuu wa utawala wa ubalozi wa Malawi bi, Jane Nankwenya, kulia ni balozi wa Tanzania nchini Marekani Liberata Mulamula na Afisa wa ubalozi Swahiba Mndeme.

                   PICHA ZOTE KWA HISANI YA CAMERA YA UBALOZI.

Monday 11 May 2015

Mahojiano na Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi kuhusu KISWAHILI‏


Kiswahili inaaminika kuwa lugha asili ya Afrika inayozungumzwa na watu wengi zaidi kusini mwa jangwa la Sahara.

Ni lugha ya taifa kwa nchi za Kenya na Tanzania na pia yazungumzwa kwenye nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi, Rwanda, Uganda, Visiwa vya Comoro na nchi nyingine

Ikizungumzwa na watu wanaokadiriwa kufikia milioni 100 hivi sasa, Kiswahili ndio lugha pekee ya kiAfrika iliyo miongoni mwa lugha rasmi za Umoja wa Afrika.

Ni lugha muhimu katika habari, shule, kazi za kiofisi, kidiplomasia na hata usalama miongoni mwa mataifa. Lakini , licha ya ukubwa wake, lugha hii inakabiliwa na changamoto mbalimbali.

Hivi karibuni, Chama cha Ukuzaji Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) kilifanya mkutano wake wa nne, ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Ali Hassan Mwinyi. Na amekuwa mkarimu sana kujiunga nasi kuzungumzia juu ya lugha ya Kiswahili na changamoto zake.

KARIBU


Sunday 10 May 2015

TIMU TANZANIA YASHIRIKI MATEMBEZI YA SUSAN G. KOMEN WASHINGTON, DC




Timu Tanzania ikipata picha ya pamoja kabla ya kuanza matembezi ya saratani ya matiti ya Susan G. Komen yaliyofanyika Washington, DC siku ya Jumamosi May 9, 2015.


Wanusurika wa saratani ya matiti wakipata picha ya pamoja.


Matembezi yakianza.


Kushoto ni msaniii toka uingereza Matt Goss aliyeimba wimbo maalum wa Strong kwa ajili ya matembezi haya ya Susan G. Komen ambaye mwaka jana mama yake mzazi alifariki kutokana na maradhi ya saratani ya matiti akipeana mkono na watembeaji wa saratatani ya titi. Kati ni Nancy G. Brinker mdogo wake Susan G. Komen akipeana mkono na watembeaji siku ya maadhimisho ya matembezi ya saratani ya matiti kwa kumuenzi dada yake kwa kuanzisha oganaizesheni ya kupigana na gonjwa hili hatari mwaka 1982 kama ahadi aliyomwekea dada yake.


Mmoja ya watembeaji na mnusurika wa saratani ya titi akipatiwa huduma ya kwanza na watembeaji wenzake baada ya kuanguka na kupata majeraha kwenye paji la uso huku wakisubili gari la wagonjwa.


Timu Tanzania ikichanja mbuga kwenye matembezi hayo.


Mwanahabari wa Kwanza Production na Vijimambo Media Mubelwa Bandio(kulia) akiwa sambamba na mwimbaji Matt Goss na Nancy G. Brinker CEO wa Susan G. Komen


Timu Tanzania ikiwa imemaliza matembezi yao ya maili 3 takribani na kilomita 5


Watoto wa wazazi Watanzania wakipata picha ya pamoja baada ya kumaliza matembezi hayo na wazazi wao.


Picha ya pamoja ya kumaliza matembezi hayo pamoja na mmoja wa kikosi cha zima moto wa TDF aliyejumuika kupiga picha na timu Tanzania.

Picha zote na Kwanza Production na Vijimambo Media & Entertainment.
Kwa picha zaidi bofya HAPA

Friday 8 May 2015

Miaka 90 ya Rais Ali Hassan Mwinyi


Leo, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Ali Hassan Mwinyi anatimiza miaka 90.
Tulipata fursa ya pekee kuketi naye akatueleza mambo machache kuhusu maisha yake
UNGANA NASI