Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday 22 November 2012

jikoni Leo;Tupike Pamoja-Mapishi ya Puréed Vegetables - Recipe of (In Swahili)!!!!!



Waungwana; "Jikoni Leo" ni  Puréed vegetables (a special meal for children from 18 months to 4 years old)

 Mpishi si Wengine ni da'Sophi wa "Tupike Pamoja". Mmmhhh Tamu Saaaana!!!!! 

Kwa kujua zaidi ingia;Tupike Pamoja  au www.tupikepamoja.com

"Swahili NA Waswahi" Pamoja Daima.

East Africa Ultimate Frisbee Tournament Arusha, Tanzania


East Africa Ultimate Frisbee Tournament
Arusha, Tanzania
November 23-24,  

Arusha Ultimate Frisbee Association is pleased to announce the East Africa Ultimate Frisbee Tournament which will be held in Arusha, Tanzania on November 23-24, 2012, Four teams will be participating in game  played at Arusha Technical College:-

The teams that will be participating:
1)  MOSHI KILL KILLERS  -Captain: Frank Mushi
2)  MWANZA TOSSERS  -Captain: Andrew Bergman
3)  ARUSHA ULTIMATE FRISBEE  -Captain: Silau Ole Nyasi
4)   NAIROBI ULTIMATE  -Captain: Aaron Colverson

For any additional information and request, please call one of The Organizers Oli - 0684082908 or 0752216040

Tuesday 20 November 2012

DR SHABANI KACHUA APATA MSIBA: AFIWA NA MTOTO WAKE KIPENZI.!!!!!!!


Mke wa Dr Shabani Kachua, Jemima akiwa na mtoto wao kipenzi Mary wakati wa uhai wake.
Dr Shabani Kachua
Mama Shabani Kachua akiwa amembeba mtoto wake kipenzi marehemu Mary wakati wa uhai wake.
Mtandao wako unaungana pamoja na familia ya Dr Shaban Kachua katika kipindi hiki kigumu cha majonzi, kwa heshima kubwa tunampa pole sana kwa msiba huu mkubwa ambao wameupata.
Mtoto Mary amefariki Dunia Nchini Canada jana alipokuwa anaishi na wazazi wake, mazishi yatafanyika huko huko.
"BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE

Monday 19 November 2012

Kisa Cha Leo na Mswahili Emu-3-Uchungu wa Mwana Aujuaye Mzazi;Sehemu ya 25!!!!!!



Kwa marejeo: Kais alipohisi kuwa huyo mwanaume, aliyemuona na yule mwanamke, ni askari wa mzee Hasim, alikimbia….., je alikimbilia wapi, na huko alipokwenda aliishia wapi, ukumbuke kuwa binti huyo alikuwa mja mzito, je ujauzito wake uliishia wapi….tuendelee sehemu hiyo ya Kaisi……..

Kais, alipozindukana alijikuta yupo kwenye kitanda, na wakati hupo tumbo lilikuwa likimuuma sana, na harufu aliyoisikia hakuwahi kusikia kabla, akageuza kichwa huku na kule, lakini hakuona mtu kwa upeo wa mcho yake. Akainua kichwa na , kwa mbali akaona watu wamevaa nguo nyeupe, moyoni akajua ni malaika, akakumbuka hadithi alizowahi kusimuliwa za malaika kuwa ni wao ni weupe, na kwasababu hawana dhambi, kila kitu chao ni cheupe.

‘Ina maana nimeshakufa nipo mbinguni,…nipo peponi na malaika’akawaza na kabla hajaweza kuinua kichwa vyema, mara akahisi kuna watu wameshikilia miguuni yake, na sauti zikawa zinaongea, mmoja akasema,;

‘Huyu tusipomfanyia upasuaji, tunaweza tusiwaokoe wote’

Kais akawaza hawa malaika wanataka kumfanya nini, kumfanyia upasuaji, haiwezekani, kwao hakuna kitu kama hicho, wanaamini kuzaa ni kwa njia ya kawaida tu, kuna dawa unakunywa, na haichukui muda kujifungua, na kabla hajajua nini kinachoendelea, akahisi tumbo likaanza kumuua, liliuma sana, maumivui ambayo hakuweza kuyavumilia akaanza kupiga ukulele.

Mmoja wa wale, watu ambao yeye aliwaona kama malaika, wakaja na kumshika vyema, na mmoja akawa kashika sindano,..Kais aliogopa sana, lakini hakuweza hata kujitetea, kwani mwili ulikuwa hauna nguvu hata ya kuinua mkono, kutokana nay ale maumivu, akapigwa sindano, ambayo ilimfanya atulie, na kuzama kwenye giza, …alipozindukana akasikia kitoto kikilia..

‘Mtoto wako mnzuri ana afya njema,..’ akaambiwa, na alipogeuza kichwa pembeni, akaona kitoto kimelazwa kwenye kitanda kidogo pembeni yake. Kilikuwa cheupe, kizuri, akatabasamu, na akainua mkono na kukishika. Baadaye aliwageukia wale watu ambao kipindi cha nyuma aliwaona kama malaika, lakini sasa akili ilikuwa imetulia, na ile hali ya mwanzo aliiona kama ndoto, akasema; kusoma zaidi ingiahttp://miram3.blogspot.co.uk/


"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima

Sunday 18 November 2012

Nawatakia J'Pili yenye Nuru;Burudani-Bahati Bukuku - Yehova na Nyingine Nyingiii!!!!!



Wapendwa;Nawatakia J'Pili yenye Nuru na Neema.

Ondoka,uangaze;kwa kuwa Nuru yako imekuja,Na utukufu wa BWANA umekuzukia.

Neno La Leo ISAYA:60:1-6;Maana tazama,giza litafunika Dunia,Na giza kuu litazifunika kabila za watu;Bali BWANA atakuzukia wewe,Na utukufu wake utaonekana juu yako.


"Swahili NA Waswahili" Mbarikiwe Woooote.

Friday 16 November 2012

Jikoni Leo;Tupike Pamoja-Mapishi ya Country salad - Recipe of (Swahili)!!!!!!

Waungwana;"Jikoni leo" si wengine ni "Tupike Pamoja," Walipotea kidogo lakini waswahili wanasema kinya kingi kina.............basi wamerudi tena kwa kishindo.

Nisiwachoshe kwa maneno meeengi.Fuatana nasi katika Pishi la Leo ni "Country Salad" ...

Haya mambo hayo...ukitaka kujua zaidi usisite ingiaTupike Pamoja au www.tupikepamoja.com            

"Swahili NA Waswahili"Karibuni Woote!!!
 

Thursday 15 November 2012

Wa-Afrika na Sherehe zao;Leo Ma-Arusi wa Leo wanavyo Jimwaga!!!!!

S n W
Waungwana; vipi Maarusi wa leo wanavyojimwaga/cheza,changamka? inapendeza au inachukiza? 

Ma-Arusi wa Leo wanafuraha sana na wanajimwaga vilivyo, yaani wanaonyesha furaha zao kabisa na ukichukulia siku kama hizi hazijirudii.
Unafikiri kwanini wanakuwa hivi jee, wamechaguana wenyewe,wanakwenda na wakati,hawana Aibu,wamengojea kwa muda mrefu kuwa MKE/MUME au............?

Vipi wa zamani ni kilio mtindo mmoja jee wengi wao wamelazishwa,Upweke wa kuwa mbali na familia,Furaha iliwazidi,Kutojuana/kuchaguliwa,wali-Olewa/Oa wakiwa wadogo  Au......?

"Swahili na Waswahili" Karibuni woooote!!!!!!